Monday, August 23, 2010

Kumbe walilipwa kuhudhuria mkutano wa CCM Dar!


Wananchi wengi katika umati mkubwa wa watu waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM kule Jangwani siku ya Jumamosi iliyopita walifika hapo baada ya kuliupwa kufanya hivyo.Baadhi ya watu niliozungumza nao wanaotoka sehemu za Mbagala Rangi Tatu na Mbande wanasema mabasi ya daladala yalikodishwa na CCM kusomba watu kuwaleta jijini kuhudhuria mkutano na waliokubali kupanda walilipwa Sh 5,000 kwamba hizo fedha ni za usumbufu na nauli yao ya kurudi baada ya mkutano.Kila moja ya mabasi haya yaliyokodishwa yalikuwa yanalipwa mapato yao ya siku mbili.

WanaJF, hizi habari ni za uhakika nilizopata kutoka kwa watu watatu waliopanda mabasi hayo na kulipwa kutoka sehemu hizo mbili nilizotaja. Wanasema tangu asubuhi majira ya saa 3 mabasi yalifika maeneo hayo na kuegesha huku viongozi na makada wa CCM wakihamasisha watu kuingia. Sh 5,000 ni nyingi sana katika sehemu hizo.Hali hii bila shaka ilijitokeza katika sehemu nyingi tu pembezoni mwa Jiji siku hiyo – watu kulipwa na kutafutiwa usafiri ili wahudhurie mkutano.Mapesa yaliyotumika ni mengi kwa tafsiri yoyote ile, na bila shaka ni kati ya zile Sh Bilioni 50 ambazo CCM imetenga kwa ajili ya kampeni mwaka huu.Tatizo langu hapa si uhalali au la kwa CCM kulipa watu kuhudhuria mkutano wao wa kampeni, ingawa pengine ni suala linaloweza kutazamwa kama ni njia mojawapo ya kuwahonga wapiga kura.Tatizo langu hasa ni ile dhana inayojengwa kwamba CCM bado ina wafuasi wengi, dhana ambayo siyo kweli kwani iwapo wananchi wangeachwa kufika hiari yao, mkutano ule ungehudhuriwa labda na nusu tu ya watu waliojitokeza.Wanachofanya CCM ni kujenga muonekano wa ufuasi mkubwa katika mikutano yao kwa nguvu fedha walizonazo – na siyo kwa hiari ya wananchi wenyewe bila kushawishia kwa njia ya pesa.
Mmepoteza Ubunge kwanini bado ninyi mawaziri?


Tangu wiki iliyopita mwishoni na hata leo nimeendelea kusikia ati "Waziri" fulani kafanya jambo hili au lile. Hivi Mwanasheria Mkuu hawezi hata kutoa maelekezo kuwa sasa hivi nchi haina mawaziri au waziri mkuu? Baada ya Bunge kuvunjwa rasmi kwa kuanza kampeni ya uchaguzi Augusti 20 wabunge wote walipoteza ubunge wao na hivyo waliokuwa mawaziri nao wamepoteza uwaziri wao. Haijalishi kama baadhi yao wamepita bila "kupingwa" lakini siyo wabunge hadi siku watakapoapishwa.Hivyo, aidha Rais Kikwete awateua baadhi yao na kuwaapisha kuwa mawaziri sasa kwa mujibu wa katiba (japo sioni haja ya kufanya hivyo) ama wale wote wanajiona ni bado "mawaziri" wapigwe makonzi na kuambiwa waondokane na fikra hizo kwani wao siyo mawaziri na uhondo wote na madaraka yao ya uwaziri hayapo sasa na wizara zao ziko chini ya Makatibu Wakuu.So.. sitaki kusikia chombo cha habari kinatuambia ati "Waziri wa Ulinzi na JKT Dr. Hussen Mwinyi" amefanya hili au lile au "Waziri wa Nishati Bw. William Ngeleja amefungua". Hawa watu SIYO MAWAZIRI!!!!!!!!!!!!!!!
Waimbaji wa makundi ya dini kushiriki kampeni


Hivi karibuni kwenye hutuba ya kuvunja Bunge Rais Kikwete aliwatahadharisha wananchi juu ya kuwatumia dini wakati wa kampeni. Lakini cha kustaabisha makundi ya dini yamekuwa yakiripotiwa kushiriki kikamilifu katika kampeni hizo. Hoja ni kwamba, hivi Chama fulani cha upinzani, kikitumia hivi vikundi vya dini kwenye kampeni tafsiri yake itakuwa ipi? Ni kwanini basi CCM yenye kujinadi kutenganisha siasa na dini isionyeshe hilo kwenye kampeni? Kwanini watu wanajifanya hawalioni hili? Na hawa jamaa walivyostrategic vikundi hivi vya dini hutumiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi, ni kwanini wasitumie mikoa yoote mpaka Zenji? Tuanzie hapo...
JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao


NA MWANDISHI WETU

7th June 2010Rais Jakaya Kikwete amesema matukio ya mimba kwa wanafunzi wa kike nchini yanasababishwa na viherehere vya wanafunzi wenyewe.Aidha, Rais Kikwete amekiri kwamba matukio ya mauaji ya vikongwe pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), yanalidhalilisha taifa.Rais Kikwete alitoa kauli hizo katika kijiji cha Kisesa wilayani Magu jana wakati akihutubia wananchi kwenye ufunguzi wa mashindano ya ngoma kwa kabila la Wasukuma; ngoma ambazo zinajulikana kama 'Bulabo'." Kila anayepata Ukimwi anaufuata mwenyewe na wengine ni viherehere vyao; kwa mfano watoto wa shule," alisema Rais Kikwete wakati akijibu risala ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Bujola, Fadha Frasince Sandhu, ambaye alisema ujumbe wa mashindano hayo mwaka huu ni vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.Kwa mujibu wa Rais Kikwete, suala la zinaa kwa bianadamu, siyo la lazima hivyo binadamu anaweza kujizuia ama kujikinga kwa kutumia kondomu." Na kwa bahati mbaya shughuli ile (uzinzi) binadamu hana dharura nayo, hivyo unaweza kutumia kondomu kama unaona kwamba huwezi kutii amri ya sita ama huwezi kuwa mwaminifu katika ndoa yako," alisema kauli ambayo ilizua vicheko miongoni mwa watu waliohudhuria ufunguzi huo. Aliwashauri wananchi watakaoshiriki kwenye mashindano hayo wawe na tahadhari dhidi ya maambukizi ya Ukimwi." ...katika mambo yanayolitia aibu taifa hasa kwa watani wangu Wasukuma, ni pamoja na mauaji ya albino na vikongwe eti tu kwa sababu wana macho mekundu. Ni mambo ya fedheha sana ingawa yanakwenda yanapungua lakini yanalidhalilisha taifa," alisema.Aliwataka washiriki wa mashindano hayo walisaidie taifa katika kupiga vita mauaji ya aina hiyo.Rais Kikwete alifuatana na wabunge kadhaa akiwemo Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (CCM) pamoja na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM).Aidha, Rais Kikwete amepewa jina la Mungubabu, ikiwa na maana busara na uwezo wa kuongoza nchi kama Mungu.Mashindano ya 'bulabo' yalianza mwaka 1954 kupitia Kanisa Katoliki Bujola, lengo likiwa ni kuweka burudani mara baada ya mavuno.CHANZO: NIPASHE
Majimbo kumi tayari kwa ccm


Ukerewe seat MP, Gertrude Mongela. Bahi constituency in Dodoma Region, a CCM candidate, Badwel Omar, Singida Urban Davi Bulala. na mengine mengi..Muimi naulizaa Hawa Wapinzani wapo serious na wanachokifanya,, Kwa mfanio Chadema Wanafikiria nini kwa kuto msimamisha mgombea uraisi Zanzibar,, hawa hawafikirii kuwa wanajipunguzia max za kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu huu?Kwasababu kwa mtindo huo, sisi wananchi tunabaki kugundua udhaifu wa chama chao, kuwa kama huna wagombea katika kipande kingine cha nchi yetu maana yake hauna msaada kwetu kwisha habali,, kama unataka kutoa Msaada Simamisha wagombea sehemu zote ili hata ukishindwa basi tunaangalia idadi ya seets bungeni,, kama vingi vyako ukisema umeibiwa kura watu tuaamini na si kuwa na viti sita then unasema nimeibiwa kura atakae amini hivi ni mpuuzi na mjinga,,,Tuwe serious na tunacho kifanya Majimbo mengi sana Chadema hawajasimamisha Wagombea nna wanatangaza RAISI atatokea kwenye majimbo sita muliyo simamisha wagombea,,,kuweni serious mimi mumenivunja moyo kabisaaaaaaaaaa
Urais ni kazi tukufu na Ikulu ni mahali patakatifu


Urais ni kazi ya watu, kazi yoyote ya kuhudumia watu ni kazi ya kumtumikia Mungu!Hii ni kazi tukufu na Ikulu ni mahali patukufu hapataki kuwa sehemu ya mzaha, uongo, ulaghai na unyang'anyi ambao tunauona leo ukisimamiwa na watawala wetu tuliowaamini na kuwapa idhini wakae Ikulu.

Kama Ikulu ingelisema wale wote waliohusika na wizi wa EPA, Deep Green Finance, Mwananchi Gold, IPTL, RITES, n.k wawajibishwe kwa mjibu wa SHERIA bila woga wala upendeleo na kwa dhati, idara husika zingelihakikisha wahusika wa Kagoda wanashughulikiwa, wahusika wote waliolitumia jeshi letu tukufu kwa manufaa yao ya kifedhuri wangewajibishwa na wala hakuna mwanajeshi ambaye angelileta fujo kupinga kwa sababu hili ni jeshi la wananchi kwa ajili ya wananchi. Wale wote waliohusika na mikataba mibovu ilitufikisha hapa tulipo wangelikuwa viranja katika magereza yetu na si kwenye majukwaa ya kuomba kuwatumikia watu..... wengine wakiwawekea watanzania safi vipingamizi ili wasiweze kupambana na hasira za wananchi katika masanduku ya kura... hawa wote wangelikuwa wanawajibika kadri ya matendo yao na Tanzania yetu ingelikuwa na matumaini makubwa na amani kama waasisi wa taifa hili walivyotaka Tanzania iwe.Wale wote ambao wanatufanyia mzaha katika zoezi muhimu la uchaguzi wasingefanya vile wanavyofanya, wasingelithubutu!Tunataka mtu atakayeomba kwenda Ikulu afanye hivyo kwa manufaa yetu sote na si kulinda maslahi ya wachache, vinginevyo malaika wa watanzania maskini wanaopoteza maisha kwa kukosa huduma za msingi (kwa sababu haki yao imetwaliwa na hao wachache wanaolindwa na watawala wetu) itawaandama na kuwafanya waweweseke na kuaibika mbele ya dunia.Mungu Ibariki Tanzania na Nguvu zako kuu zishuke kwa wale wote wanaoifanyia mzaha kazi yako
Hongereni Wana-Upinzani Tz, mtakumbukwa kama Mashujaa wa Taifa hili.....


Ni nani asiyejua kuwa wapinzani wanatumia muda, rasilimali na jasho lao kwa kipindi kikubwa sana ili kuikomboa nchi yetu kutoka katika madudu ya wasioipendea mema nchi na wananchi wake bali waliotayari kujineemesha wao na familia zao?Tuchukue mfano mrahisi, wakati mimi na wewe tukienda kazini kwa ajili ya familia zetu na maisha yetu binafsi, kuna wakina Freeman Mbowe, Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe, na wengine weeeengi ambao wanatumia muda wao mwingi kuzunguka huku na huko kuwaamsha watanzania wengi waliolala waone jinsi gani wanadhulumiwa haki zao.Cha kushangaza, hatuwaungi mkono watu hawa, inafika kipindi watu hawa wanaingia mifukoni kutoa chochote kwa ajili ya mpambano huu. Badala yake wengi wetu tunawakejeli na kuona ni haki yao na ni wajibu wao kufanya hivi!Hii ni aibu kabisa! Itakuwaje wao nao wakaamua kutundika daluga na kuamua vision zao ziwe kwenye familia na maslahi yao binafsi? What if wakiamua upinzani sasa basi, kama ndo imekuwa hivi basi acha iwe kila mmoja afe na lake? Unafikiri katika miaka kumi kutakuwa na Tanzania tena?Mmeliona hili?

What if na wenyewe wangeamua: Sasa basi, acha na wao wakubali fulana za kijani na njano na wapokee hizo takrima za chini chini washabiki wa ccm wanazopewa kwa sasa?Cha ajabu sana, watanzania wanasahau mapema kweli kweli. Juzi tu hapa, wapinzani hawa tunaowakejeli leo wamefanya kazi nzuri sana bungeni hatimaye tukaona kilichokuwapo EPA na RichMond, leo hii watanzania wanajidai wamesahau. TUCTA nao watu wa ajabu sana, juzi walikuwa na mwelekeo huu, leo out of blue wanamwelekeo wa kiaina fulani. Media na yenyewe, juzi juzi ilikuwa na uzalendo, leo hii naona wameanza kuwa na mwelekeo wa U-CCM.Ninajiuliza, unafikiri tunawakomoa wapinzani? Unafikiri ni wajibu wa wapinzani kumwagika jasho ili nchii hii iwe ya neema hapo baadaye?Wangapi leo hii mnashabikia tu sera ya kilimo kwanza na ongezeko la bajeti ya kilimo wakati ki-uhalisia ukichambua hicho kitu hakipo? (Dr Slaa aliwachambulia vizuri - mchango mwingine wa upinzani makini kwa hatima ya nchi hii)Kama watanzania wanafikiri ni muda wa kuwakomoa wapinzani, basi wajiaandae na maumivu zaidi.

CCM ni wataalamu wa kuuma na kupuliza, leo wanapuliza, ngoja uchaguzi upite tuwaone!

Leo hii fedha ya Tanzania inashuka thamani kila kukicha, kwenye mzunguko wa fedha leo hii, Tsh. elfu kumi na Elfu tano (noti kubwa) zimekuwa za kawaida kuwepo kwenye mzunguko wa kawaida kabisa wa maisha hata yale ya kawaida sana. Ndio maana hadi kesho, watanzania mishahara haitatosha na gharama za maisha zitazidi kwenda juu kila kukicha.Wizi wizi wa mali za umma, na ubadhirifu utazidi kuongezeka, tusitegemee mapya kutoka kwa CCM.

na sitashangaa sana, ifikapo mwaka kesho katikati, watu wataanza kulalamika tena kuwa serikali ni mbovu ilhali katika uchaguzi walikubali kurubuniwa.Angalia wasanii majuukwaani wanavyoimba kinafiki? Mimi sina jingine zaidi ya kusikitika. Ni lini watu hawa wooote watafunguka macho na kuona magumu na mazito yanayoikabili nchi yetu chini ya CCM?Akili ipo kichwani mwako, fanya maamuzi sahihi mwananchi
Vituko vya kampeni vyaanza


• Mkutano wa Mrema TLP wavurugwa

na Mwandishi wetu

VITUKO vya kampeni za uchaguzi mkuu vimeanza kujitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoani Kilimanjaro kuelezea kukerwa na mwenendo wa viongozi wake walioamua kumpigia debe mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Philemon Ndesamburo, katika jimbo la Moshi Mjini.

Hatua ya viongozi wa CCM kumpigia kampeni inaelezwa na wanachama wake kuwa ni kutokubaliana na maamuzi yaliyofanywa Halmashauri Kuu ya (CCM) kumwengua mshindi wa kura za maoni Athuman Ramole.Chama hicho kimesema kiko tayari kuwafukuza wanachama na viongozi wote watakaobainika kutokana na utovu wa nidhamu kwa kushindwa kukubaliana na maamuzi ya NEC.Katibu wa chama hicho mkoani hapa, Steven Kazidi, aliyasema hayo juzi wakati akimnadi mgombea ubunge wa chama hicho , Justine Salakana, kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni zake kwenye viwanja vya Manyema.Alisema kuna wanachama ambao ni viongozi ndani ya CCM, wamekuwa wakizunguka usiku wakitumia usafiri wa pikipiki wakidai wameonewa kwa kuwa mgombea waliyemtaka Buni hakuteuliwa licha ya kushinda, hivyo kuwashawishi wana CCM wampigie kura mgombea wa CHADEMA.MAREALENaye Kamanda wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Manispaa Moshi Aggrey Mareale, alisema itakuwa vigumu katika kampeni zinazoendelea kusimama jukwaani na kuacha kumsifia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemoni Ndesamburo.Marealle aliyasema hayo jana katika uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo uliofanywa katika viwanja vya Manyema vilivyoko mjini hapa.Alisema hata kama mbunge huyo aliweza kujenga madarasa 10 ya shule ndiyo jitihada zake, lakini huenda ameshindwa kutosheleza mahitaji ambayo yalikuwa yanahitajika katika jimbo zima.MOSHIHabari zaidi kutoka Moshi, zinasema wakati kampeni zikiwa zinaendelea katika maeneo mbalimbali, juzi katika mkutano wa wa mgombea ubunge wa jimbo la Vunjo, Agustine Mrema, uliingia dosari baada ya Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kahe kusababisha vurugu zilizosabisha mkutano wake kusimama kwa muda.Vurugu hizo, ambazo zilidumu kwa takriban dakika 15 na kupelekea wananchi waliohudhuria mkuatano huo kupoteza usikivu, wakati Mrema alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Kahe na hivyo kulazimika kutoa fursa kwa wasimamizi wa mkutano kufanya jitihada za makusudi kutuliza vurugu hizo.Akizungumza baada ya kutokea kwa vurugu hizo, Anael Mmamyi ambaye anawania nafasi ya udiwani kupitia TLP kata ya kahe, alisema kuwa ni vyema kama vyama vya siasa vinafanya mikutano yake na kuhudhuriwa na upinzani; ni vyema wakawa na nidhamu ili kuepuka vurugu inayoweza kupelekea kuwepo kwa uvunjifu wa amani.Katika mkutano huo, Mrema alisisitiza kuwa lengo la kujitokeza kuwania kiti cha ubunge kwenye jimbo hilo ni kuhakikisha aliahidi kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo kwa kufufua mifeji ya zamani kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji pamoja na kuweka kipaumbele katika sula la elimu.KAHAMAPingamizi la mgombea ubunge katika jimbo la Msalala kwa tiketi ya CCM, Ezekiel Maige, alilomwekea mgombea wa CHADEMA, Edward Mlolwa, limegonga mwamba baada ya Kamati ya Maadili ya Jimbo la Kahama na Msalala kumthibitisha ni mgombea halali.Kwa mujibu wa barua ya Agosti 21 aliyoandikiwa Maige na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kahama na Msalala, Eliza Bwana, na nakala kupatiwa mgombea wa CHADEMA ambayo Tanzania Daima imepata nakala yake, ilieleza baada ya kupitia maelezo ya pingamizi, Kamati ya Maadili imejiridhisha kuwa Mlolwa ni mgombea halali wa nafasi ya ubunge katika Jimbo la Msalala kwa tiketi ya CHADEMA.Maige ambaye ni mbunge aliyemaliza muda wake na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na ambaye hakupata mpinzani katika mchakato wa kura za maoni za chama chake, aliwakilisha pingamizi lenye vipengele 12 dhidi ya mgombea huyo.Miongoni mwa mapingamizi hayo ambayo kamati hiyo imeyapitia na kuyathibitisha kuwa hayana dosari ya kumzuia Mlolwa kuwania ubunge ni juu ya kutodhaminiwa na chama chake, uanachama wake wa CHADEMA, kudhaminiwa na wapiga kura, kutowasilisha tamko la kisheria na kutowasilisha mchanganuo wa gharama za uchaguzi.Kwa mujibu wa barua ya msimamizi wa uchaguzi, tume ilimfafanulia Maige kuwa Mlolwa amedhaminiwa na chama chake cha siasa kwa kujaza fomu ya uteuzi iliyosainiwa na katibu wa chama chake.Ni mwanachama halali wa chama chenye usajili ambaye amedhaminiwa na wapiga kura walioandikishwa katika madaftari ya wapiga kura wa jimbo, pia aliwasilisha tamko la kisheria lililosainiwa na hakimu Agosti 19, mwaka huu.SINGIDAHabari zilizopatikana wakati tunakwenda mitamboni, zinasema mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo la Singida, Mohamed Dewji, amepita bila kupingwa.Taarifa iliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Yohana Lucas Maki, ilisema pingamizi lililokuwa limewekwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Josephat Isango Hadu, limetupwa.Katika uwamuzi huo, msimamizi huyo alisema Dewji hajatenda vitendo vya rushwa kama Sheria ya Gharama ya Uchaguzi inavyoelekeza.
0 #16 tiky 2010-08-23 12:53

Mimi sishangai hao watu wa chama ca kijani kushinda mapingamizi yao, tangu lini kesi ya mbuzi ikaamuliwa na Chui?? Wenye akili tunajua kuwa ni uonevu tu. Masauni kule Zanzibar kadanganya umri bado amepeta wakati udanganyifu huo ulimvua uenyekiti wa UVCCM. Pia huyo Masauni kwa kuwa alidanganya kuna hatua gani vyombo vya dora vimechukua mpaka sasa??? Hapo ndipo uone uonevu wa CCM.Siku zenu CCM zinahesabika wala msiwe na wasiwasi kudondoka kwa Mgombea wenu hadharani kuna maana kubwa, mtaanguka anguko kubwa na wala hamtasimama tena. Msisingizie kufunga kwani wangapi tunafunga na hatuanguki??? Je mwaka jana kule Mwanza alivyoanguka nako alifunga????? Nyie viiiiipi???

Quote

0 #15 tiky 2010-08-23 12:45

Ukiwa na watu kama akina Mtebene unaweza kabisa kuwapa chupa au hata pipi halafu wewe ukachukua Almasi toka kwao halafu akabaki anachekelea kama ZUZU. Mwl Nyerere aliwaona akina Mtebene na akawaonywa tatizo hawaambiliki. Hawa akina Mtebene kesho tu utasikia wanalalamika huduma hospitali hakuna, maji mwezi mzima hayajatoka, nauli zinapanda.....nk ni hawa hawa. Yaani kwao ni bora liende tu. Mtebene hujachelewa hata sisi tulikuwa kama wewe lakini tumeamka.Hiyo serikalin ya JK unayoifagilia ndio ambayo imemfunga mtu aliyeiba bilion 254 Benki Kuu kifungo cha miaka miwili wakati wezi wa kuku mtaani wanachomwa moto au kufunga kifunga as if wameua. Uchumi wa nchi kila siku unashuka, maisha ni magumu hayaelezeki, hivi unaona haya wewe???? Hujachelewa na tunakuomba usiharibu kua yako mpe Dr. Wilbroad Slaa. Tunataka Rais makini si mwimba Taarabu!!!!!

Quote

-1 #14 Ridhiwan Kikwete 2010-08-23 11:19

Baba halafu maswala yako kuanguka hovyo kwenye kampeni hata sio viuzurimanake unatuogopesha wanao na usione kuwa mama amekaa kimya ni kwa sababu anaogopa tu kukwambia.Jikaze baba tushinde kwa kishindo.

Quote

0 #13 Daniel 2010-08-23 10:27

Sasa Ndugu yangu SALLY? CCM walipoleta "maendeleo" hayo ilikuwa ni Fadhila au Jukumu lao walilopewa baada y a kukabioidhiwa dola? Je ilikuwa ni hiari?

Na je ndugu SALLY, Hayo "maendeleo" unayomaanisha unalinganisha na nchi ipi? Kenya? Uganda? Nigeria?..... na je Umefanya pia utafiti na ulinnganifu wa uwepo wa mali asili (Natural resouces endowment)baina ya Tanzania na nchi ambazo pengine umetulinganisha nazo na ukagundua CCM wameleta maendeleo Tanzania na kwahivyo tuendelee kuwapa ridhaa ya kutawala? au ndo upo kwenye Chain ile ile ya Kagoda na wengineo? Ipo siku wenye nchi wataamka ninyi endeleeni kushangilia msichokijua........

Quote

0 #12 Daniel 2010-08-23 10:13

Ni jambo la ki[NENO BAYA] kusheherekea ushindi wa mezani kama huyu ndg yetu Matebene anavyofanya. Ukiona mtu anafanya hivyo haswa katika nchi ya kidemokrasia ya vyama vingi ana mapungufu makubwa ya ufahamu. Nitawapongeza sana wale watakaohimili vishindo vya kampeni na kupata ridhaa ya wananchi na sio kuipata ridhaa hiyo "kiubakaji". Wewe kwa akili na ufahamu wako na kwa dalili zilizokuwa wazi hapa Mwanza unadhani Masha alikuwa na njia nyingine ya kurudi bungeni? Kwa lipi alilofanya tulipompa ridhaa ya miaka 5 iliyopita? Sasa unasheherekea u[NENO BAYA]? Ilikuwa ni busara Watunga sheria wetu wakaona umuhimu wa kuvipa vyama nafasi ya mwisho katika kurekebisha kasoro zinazojitokeza katika fomu zao na ikibidi pale mgombea anapokosa sifa chama kikateua mtu mwingine. Hii ndio demokrasia na siio kulazimisha eti huyu ni mbumbe kapit bila mkupingwa. nani kakuambia? apigiwe basi hata kura ya NDIYO au HAPANA halafu tuone kama watu wenye ufahamu wa ki-mtebene wataendelea kusheherekea kudumazwa na kudhalilishwa kwa Demokrasia.

Quote

0 #11 TAFAKARI 2010-08-23 10:09

WATANZANIA WENGI WATAISHIA KUWA KAMA HUYU BIBI. AMECHOKA KUTOKANA NA HALI NGUMU YA MAISHA LAKINI BADO HAJIELEWI. HIVI WATANZANIA NANI ALIYEWALOGA?

Quote

-3 #10 Siegfried David 2010-08-23 10:06

Hata ukipinga ccm wataendelea kushika hatamu,sio kwamba sihitaji mapinduzi hapana,wapinzan i wa hii nchi ni wanafiki hawajapatatokea kwenye hii dunia,ndomana cmm itaendelea kutamba na nyie upinzani kuendelea kungojea hiyo ruzuku ,sihamna mnalo fikiri zaidi ya hilo nyie waroho wa madaraka!!! JK IS THE BEST!!?

Quote

+3 #9 GILLIARD 2010-08-23 10:02

Watu wanaoshabikia CCM ni wale wako karibu sana na ufisadi au ndio wanaufuja mali za umma hivyo wanachekelea watoto wa masikini wanavyoliwa na mainzi mpaka machoni.Mimi nadhani kuna watu hawajatembelea majimbo kama yale ya kina Olesendeka kule Simanjiro wanakodai amepita bila kupingwa.Mtoto anashikwa na mainzi kuanzia midomoni,puani hadi machoni mapaka analala chini kujisalimisha kwa ajili ya kukosa maji ya kunawia uso lakini Watanzania bado wanashabikia CCM. Kuna umuhimu wa wawekezaji kuja na vipimo vya kutupima akili.Siamini kuwa mpaka dakika hii kuna watu wanashabikia CCM wakati hatuna viwanda wala sehemu muhimu za ajira.

-Viwanda vyote vimekufa.

-Mashamba ya kuzalisha mazao(NAFCO)kal asi.

-Shirika la Ndege kalasi.

-Shirika la reli kalasi.

-Kiwanda cha Matairi kule Arusha kalasi.

-Tanzanite kule Arusha kalasi.

-Viwanda vya nguo kalasi.

Jambo la kushangaza tunaagiza pamba ya kufungia vidonda China wakati Mwanza tunalima pamba.Tunaagiza matairi Kenya wakati tuna kiwanda Arusha.Tunaagiza nguo Thailand na China wakati tuna viwanda na Pamba nchini.Mtu anayeshabikia CCM ana lake jambo.Huyu atakuwa sio Mtanzania hivyo anafurahia mateso tunayopata.Leo dola ni 1,600/= T.shs je baada ya uchaguzi dola moja itakuwa imefikia shs ngapi?

Quote

0 #8 Muungwana 2010-08-23 10:00

Watu kama monto na mtebene ni [NENO BAYA] ngu watu tunataka changes na demokrasia ya kweli. kama mmesoma basi hamjaeleimika otherwise tunaquestion kama mna akili kweli

Quote

+1 #7 kalungu 2010-08-23 09:51

ccm mnaikandamiza demokrasia ya vyama vingi,ni vema mngetutangazia kurudi RASMI kwa mfumo wa chama kimoja!

Quote

-1 #6 sally 2010-08-23 09:48

unajua nawashangaa sana wasioona maendeleo yaliyoletwa na yanayoendelea kulatwa na CCM,hawajui kwamba CCM ndio yenyewe wengine wanagiza ,nawauliza kama sio CCM wangeongea hayo wanayoyaongea leo hii,hii ni kutokana na kuimarishwa kwa demokrasia katika nyanja zote za kijamii acheni longolongo hazito kusaidieni tuungane sote kuiletea USHINDI WA KISHINDO CCM(IDUMU CCM DAIMA)

Quote

+2 #5 Nyau 2010-08-23 09:31

Quoting Mtebene A.J:

CCM wera wera!!!!!!!!!! na bado wakimbizeni hao mpaka wawaheshimu......nashangaa wanataka kuvaa suruali kabla ya nepi na bado endeleeni kuwapa dozi..........wamesahau usemi usemao mtaka nyingi nasaba hifikwa na mwingi msiba!!!!???????....waacheni wayaokote makapi maana ndio kawaida yao....Nimejua ni kwanini Kikwete alisema hajui kwanini Tanzania ni masikini. Kama una watu wenye akili kama ya Mtebene ambaye haoni kabisa uhuni wote ambao CCM imefanya wa kubaka uchumi wa nchi yetu, basi ni bora tu kuongoza makondoo kuliko kuongoza binadamu. Binafsi namshangaa sana Mtanzania mwenye akili timamu ambaye bado anashabikia CCM hadi hivi sasa, asione ukweli kwamba thamani ya pesa yetu imezidi kushuka, mfumko wa bei unazidi kutisha, hali ya maisha ya mtanzania inazidi kudidimia huku hali ya mafisadi ikizidi kustawi. Kama kuna mtanzania haoni hilo na kwa dhati kabisa anasimama kuisifia CCM kama Mtebene anavyofanya basi yumkini ni taahira au kichwani kwake hakupo sawasawa. Nchi yetu sasa hivi inahitaji mageuzi na si longolongo za CCM.

Quote

+1 #4 LENGAI 2010-08-23 09:30

Kicheko unachokicheka leo ndugu Mtebene kitakuwa kilio chako baada ya uchaguzi.

Labda kama unakaa ikulu ndio utapata salama baada ya uchaguzi.Lita moja ya petroli itakuwa 3,000/=, Lita ya Diesel 2,800/=, Kilo ya Sukari 2,500/= wakati unalipwa mshahara 200,000/=. Hapo ndio nitajua unajua kucheka.Endekezeni tu kukaa na viongozi wa kubeba mabakuli ya kwenda kuomba kila mwaka ulaya na marekani cha moto tutakipata.Nchi naina hata Ndege moja ya kwenda hata hapo Dodoma wewe unachekelea,Vyu ma ya reli vimekatwa vinauzwa madukani wewe unachekelea,Mat ibabu ya foleni tena kwa kulipia wewe unachekelea.Subiri uchaguzi upite utapata jibu la msiba uliouomba.

Quote

+1 #3 CAROLINE 2010-08-23 09:17

Mimi nadhani Watanzania tuna mapungufu fulani.Bibi kama huyu anayecheza kwenye picha muulizeni mara ya mwisho alikunywa lini chai ya maziwa na mkate hata hakumbuki.Kilo moja ya sukari ni shs.2000/= sidhani anaweza kununua.Sukari anaipata siku za kampeni na kupiga kura tu.Rais akisha ingia ikulu wala hana habari naye.Mtalala barabarani mkidai haki zenu hadi mauti iwakute.

Quote

0 #2 Montto 2010-08-23 09:16

Hahaha nilijua wengi wao ni matapeli wa siasa sasa kama mtu hujui hata mtaa unaoishi unataka umtawale nani?upinzani wa kweli utatokana na ccm yenyewe pale ambapo nusu itakapomeguka na kwenda upande wa pili huku nusu ikibaki upande mmoja,mimi huwa nashangaa sana ukishindwa kura za maoni ccm inakuwa mbaya lakini ukishinda unakisifia Pole sana baba SHIBUDA

Quote
Waandishi Wetu


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezidi kujitwalia majimbo ya ubunge kabla ya upigajikura hapo Oktoba 31 mwaka huu, baada ya idadi ya wagombea wake wakiwemo mawaziri kupita kwa ushindi wa 'mezani' wa mapingamizi dhidi ya washindani wao na kuwezesha chama hicho, kuweka kibindoni majimbo 16 hadi sasa hivi.Hadi jana, CCM iliweza kujitwalia majimbo zaidi likiwemo Mlele kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, baada ya mgombea wa CUF Abasi Rashid, kujitoa kwenye mbio hizo huku katikia Jimbo la Mtama, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akipita kwa mlango huo wa pingamizi dhidi ya Isaya Ndaka wa TLP, baada ya kukosa idadi ya wadhamini wanaohitajika.Kasi hiyo ya CCM ilizidi kuongezeka jana baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha kupita kwa mlango huo wa pingamizi dhidi ya mshindani wake kutoka Chadema Wenje Ezekie huku Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja, naye akipeta.Hadi sasa wana CCM waliotangazwa kuteuliwa wabunge na majimbo yao kwenye mabano ni Pinda (Mlele ), Mohamed Dewiji (Singida mjini), January Makamba (Bumbuli), Job Ndugai (Kongwa), Deo Filikunjombe (Ludewa), Gregory Teu (Mpwapwa), Anne Makinda (Njombe Kusini), William Lukuvi (Isimani, na Celina Kombani ( Ulanga Mashariki).Wengine ni Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), Profesa Anna Tibaijuka (Muleba kusini), Profesa David Mwakyusa (Rungwe Magharibi), Philip Mulungu (Songwe) na (Mtama, kwa Membe).Jimboni Nyamagana, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo alikubaliana na pingamizi la Waziri Masha dhidi ya mshindani wake ambaye baadhi ya taarifa ikiwemo uraia wake, zilikuwa tata.Akitoa uamuzi wa tume ya uchaguzi jimbo la Mwanza chini ya msimamizi Willison Kabwe alisema, Wenje ameenguliwa katika mbio hizo kutokana na kukosa sifa ya uraia ikiwa ni pamoja na kudanganya makazi.“Pingamizi alilowekewa Wenje, alidaiwa kuwa siyo raia, katika utetezi wake hakuweza kuwasilisha ushahidi wowote kuonyesha uraia wake kama vile vyeti vya kuzaliwa, kuhitimu shule na alizosomea hapa nchini," alifafanua na kuongeza:,"Hakuweza kuwasilisha paspoti wala kiapo chochote na shahada ya kupigia kura, basi nakubaliana na pingamizi la kuwa siyo raia.”Ingawa Masha aliweka pingamizi hilo kama mgombea ubunge, lakini kisheria wizara anayoongoza ndiyo yenye dhamana ya uraia wa wageni na wazawa, kwani akiwa waziri anaweza kumtangaza nani ni raia na nani si raia.Katika pingamizi la pili dhidi ya Wenje, Masha alidai alidanganya nafasi yake ya kazi kuwa yeye ni mtumishi wa cheo cha ‘Country Manager’ wa kampuni ya Nation Media Group, wakati yeye ni mtumishi wa cheo cha Sales Manager (Meneja Mauzo).Mtoa pingamizi (Masha) aliweka pingamizi hilo na kuonyesha ushahidi wa barua, kutoka kampuni hiyo ikipinga maelezo ya mgombea huyo.“Katika utetezi wake Wenje aliwasilisha Job description na alikana kumtambua mmoja wa viongozi wa juu, akisema hahusiki na kampuni hiyo ya Nation Media group," aliweka bayana Kabwe na kuongeza:,"Nilitegemea Wenje angewasilisha barua ya ajira kutoka kwa mwajiri wake ikithibitisha cheo chake alichodai ana kitambulisho chake. Hivyo nakubaliana na pingamizi kuwa alidanganya nafasi yake ya kazi.”Hoja nyingine katika pingamizi hilo iliyomtupa mgombea huyo nje ya mbio za kuwania jimbo hilo, inahusu tamko la wadhamini katika fomu na 8 C, ambayo alichanganya tarehe ya uteuzi akidai utafanyika Oktoba 31 mwaka huu badala ya Agosti 19 mwaka huu, jambo ambalo alipaswa kuwa makini nalo kutokana na kugombea nafasi hiyo nyeti.Pingamizi la mwisho ambalo aliwekewa lilikuwa ni eneo lake la makazi, Wenje alieleza anakaa mtaa wa Bulola ‘A’ jijini Mwanza, jambo ambalo siyo kweli.“Katika maelezo yake alieleza anamiliki nyumba namba BSL/BLL/01/219 mtaa huo. Alipaswa kuwasilisha nyaraka za uthibitisho wa umiliki wa nyumba aliyotaja kumiliki kutokana na kukosekana kwa uthibitisho huo mimi msimamizi wa uchaguzi nakuwa na shaka na ukazi wake,” alizidi kupigilia msumari Kabwe.Alisisitiza kwamba, kwa kuzingatia sababu zilizobainishwa hapo juu, "nakubaliana na sababu za pingamizi hivyo kwa mamlaka niliyopewa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985 pamoja na marekebisho yake natamka rasmi kutengua uteuzi wa bwana Wenje."Kutokana na maamuzi hayo ya msimamizi wa uchaguzi, Masha anabaki kuwa mgombea pekee wa ubunge katika jimbo hilo la Nyamagana.Hata hivyo, akizumgumza uamuzi huo Wanje alisema aliupokea na kuongeza kwamba, kwa sasa anawasiliana na viongozi wa chama cheke mkoa na kisha atasafiri kuelekea Dar es Salaam makao makuu ya chama ambako atakutana na wanasheria wa Chadema kuona namna ambayo watakata rufaa kupinga uamuzi huo wa msimamizi wa uchaguzi.“Sikubaliani na umuzi huo na lazima tutakata rufaa, ikishindikana rufaa hiyo basi nitakwenda wilayani Rorya mkoani Mara kufanya mkutano mkubwa kuwaeleza wananchi wanaonitambua kuwa mimi ni mzaliwa wa Rorya wajue Waziri wa Mambo ya ndani ameninyang’anya uraia,” alitangaza azma hiyo.Aliweka bayana kwamba, katika mkutano wake kwa wananchi wa Rorya atawaeleza wagome kulipa kodi kwa serikali ya Tanzania kwa vile Rorya siyo eneo la Tanzania na wao licha ya kuzaliwa hapo siyo raia.SENGEREMA, wagombea wawili kutoka vyama vya upinzani waliokuwa wanashiriki mbio za kuwania nafasi ya ubunge wilayani Sengerema, wametupwa nje kutokana na kukosa sifa za kugombea.Wagombea hao kutoka CUF, Mbaraka Sadi Chilu pamoja na mgombea wa Chadema, wameenguliwa katika dakika za mwisho baada ya kushindwa kujitetea kutokana na makosa ambayo yamejitokeza.Akizungumza kwa njia ya simu Msimamizi wa Uchaguzi Wilayani hapo Erica Msika, alifafanua kwamba mgombea wa CUF alishindwa kusaini fomu namba 10 pamoja na kutokuheshimu maadili ya uchaguzi.Kwa mujibu wa msimamizi huyo, kutokana na makosa hayo ni dhahiri mgombea huyo amekosa sifa ya kuwa mgombea halali kupitia tiketi ya chama chake .Kuhusu mgombea wa Chadema, Magafu Salvatori, msimamizi wa uchaguzi alisema uteuzi wake ulitenguliwa baada ya wadhamini wake kukosa sifa ya kumdhamini.Aliweka bayana kwamba, kuna baadhi ya wadhamini wake vitambulisho vyao vya kupigia kura vilikuwa havijasajiliwa katika daftari la mpigakura, kosa ambalo linawapotezea sifa ya kuwa wadhamini wa mgombea.Msimamizi huyo aliongeza kwamba, pamoja na wadhamini hao kukosa sifa mgombe huyo hakusaini fomu ya tamko na kushindwa kujitetea sababu zilizomfanya ashindwe kuzisaini.Msika alisisitiza kwamba, baada ya kupitia pingamizi hilo kutoka kwa muweka pingamizi (Ngeleja), alibaki kuwa mgombe pekee kwa tiketi ya CCM katika Jimbo hilo.Wakati huo huo, pingamizi zote ambazo zilifikishwa kwa msimamizi wa uchaguzi kutoka katika Jimbo la Ukerewe, zimetupiliwa mbali.Katika mapingamizi hayo mwanasiasa wa mkongwe, Getrude Mongella, alimwekea pingamizi mgombea wa Chadema, Salvatory Machemli, kwa madai alikiuka kanuni za uchaguzi huku naye akiwekewa pingamizi na mgombea huyo wa upinzani kwa madai ya (Mongella), alikosea kujaza kazi yake.Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Dk Leonard Masale, alisema baada ya kupitia mapingamizi yote na kupitia vielelezo vyote aliamua kuyatupilia mbali hivyo wagombea wote watabaki katika mbio hizo kwa ajili ya uchaguzi wa Oktoba 31.

SINGIDA, mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Singida Mjini, Mohammed Dewji, naye amepata ushindi huo wa mezani baada ya wapinzani wake watatu kuenguliwa kutokana na fomu zao kuwa na mapungufu mengi.Waliokuwa wapinzani wa Dewji ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) Omari Sombi, mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Siuyu, Josephat Isango kupitia Chadema na Rashid Mindika wa CUF.Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Yona Maki, alifafanua kwamba, wagombea wote watatu walioenguliwa, walielezwa siku wanachukua fomu hizo kwamba watapaswa kuzijaza na kuzirudisha siku tatu kabla ya siku ya mwisho kisheria ili zikaguliwe na endapo zitakuwa na mapungufu, wazirekebishe kabla ya muda kumalizika."Ndugu zangu hawa hawakufanya hivyo na walipozirejesha na kukaguliwa, zilikutwa na mapungufu mengi na muda wa wao kuzirekebisha, ulikuwa hautoshi na ndio maana ulipofika muda wa kufunga pazia kwa zoezi hilo, wenyewe wakawa hawajakamilisha shughuli hiyo ya kuondoa mapungufu," aliweka bayana.Akimzungumzia Dewji ambaye ametangazwa rasmi kuwa mbunge mteule wa jimbo la Singida mjini, msimamizi huyo alisema alirejesha fomu zake siku tatu kabla ya muda kwisha na fomu zake zilikaguliwa na kukutwa hazina tatizo.Maki aliongeza kwamba, kwa sasa zoezi la kumtafuta mbunge wa Jimbo la Singida mjini limekamilika na wamebakia na zoezi la madiwani.Naye Dewji kwa upande wake alisema hana la kuzungumza zaidi ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uweza wake, na kwamba alimsaidia kuwaumbua wale ambao walikuwa hawamtakii mema kwa kumzushia mapingamizi yasiyokuwa na msingi, fitina, majungu na kueneza taarifa zenye lengo la kumpaka matope.Habari hii imeandikwa na Frederick Katunlanda, Mwanza, Sheilla Sezzy, Sengerema, Gasper Andrew, Singida

Friday, August 20, 2010

Rais Kikwete na Wafanyakazi


Madai ya wafanyakazi kutaka nyongeza ya mshahara yalianza muda mrefu, kiwango hicho ambazo Rais Kikwete amekitaja leo kwa dhihaka kilianza kuzungumziwa toka mwaka 2007; ni hatua gani serikali yake ilichukua toka wakati huo mpaka wakati huu?

Hotuba ya Rais imenifanya nikumbuke makala hii ambayo niliindika mwaka 2007: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=51Katika makala hiyo nilinukuu kipande cha hotuba ya Nyerere ambacho ni muhimu nikakirejea hivi sasa katika muktadha wa Hotuba ya Kikwete.

Mwalimu Nyerere yeye alikabiliana moja kwa moja na wahuhusika na kuwaeleza: “Mna haki mnapozungumzia mishahara…..mishahara yetu ipo juu sana. Mnataka niipunguze? (makofi)…..mnataka nianzie na mshahara wangu? Ndio, naanza kuukata wa kwangu (vilio vya ‘hapana’). Nitapunguuza hii mishahara katika nchi hii. Wangu naukata kwa asilimia ishirini kuanzia sasa…..hii mishahara hii. Hii mishahara ndio inajenga huu mtazamo kwa wasomi, wote kabisa. Mimi na wewe. Tuko katika tabaka la wanyonyaji. Niko katika tabaka lenu. Ambapo nafikiri paundi mia tatu na themanini kwa mwaka (kiwango cha chini cha mshahara uliokuwa ukilipwa katika Jeshi la Kujenga Taifa) ni kambi ya gereza, ni kufanyishwa kazi kwa shuruti. Tuko katika tabaka la juu la wanyonyaji. Je hiki ndicho ambacho taifa letu kilipigania? Je hiki ndicho tulichokihangaikia? Ili tuendeleze tabaka la juu la wanyonyaji?....mko sawa, mishahara ipo juu sana. Kila mtu katika nchi hii anahitaji paundi ya ziada. Kila mtu isipokuwa mkulima masikini. Anawezaje kutaka? Haijui lugha…je ni nchi ya namna gani tunajenga?” (tafsiri yangu toka nukuu ya hotuba ya kingereza ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliitoa papo kwa papo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Dar es Salaam baada ya maandamano ya wanafunzi Oktoba mwaka 1966)

Nyerere wakati huo alikwenda kuihutubia hadhira muafaka kwa suala alilolizungumzia, lakini kwa Kikwete yeye alikwenda kuwahutubia wazee na kuhusu ‘wafanyakazi’; je, alikuwa anapeleka mashtaka au alikuwa anatafuta kupigiwa makofi na hadhira isiyohusika ama ni ishara ya hofu ya kuogopa kukabiliana na wafanyakazi ana kwa ana?

Kuhusu Hotuba la Rais kusema kwamba mgomo ni batili anapewa taarifa nusu nusu au anapotoshwa ama ameamua kuupotosha umma. Ni vizuri serikali ikarejea na kukumbuka kuwa kusudio la mgomo lilitolewa siku nyingi nyuma kama sheria inavyohitaji; na wafanyakazi walieleza wazi kwamba walirejea kwenye majadiliano kwa maombi ya umma huku kusudio lao likiwepo pale pale. Hivyo, ni muhimu serikali ikaepusha mgomo kwa kushughulikia madai ya msingi ya wafanyakazi ambayo ni nyongeza ya mshahara hususani kima cha chini, punguzo la makato ya kodi na uboreshaji wa pensheni wakati wa kustaafu. Nilisoma tangazo la baraza husika ambalo limeshapwa na serikali katika magazeti mbalimbali hivi karibuni lilieleza bayana kwamba katika suala la kiwango cha kima cha chini 'wamekubaliana kutokukubaliana'; hivyo nimeshangazwa na kauli ya Rais Kikwete ya kwamba majadiliano yalifikia makubaliano kuhusu kiwango.Tafsiri ya matukio haya ni ama kuna ufa mkali ndani ya serikali ama serikali imekerwa na kutoalikwa Mei Mosi huku ikijaribu kutumia kila mbinu kuficha aibu ya mgomo wa wafanyakazi wakati nchi ikiwa mwenyeji wa World Economic Forum-Africa(mbinu waliyoitumia kupanda miti mikubwa ya haraka haraka along Sam Nujoma Road).Lakini naamini Rais anatambua kwamba watu wachache wanaweza kudanganywa kwa muda mchache, lakini sio watu watu wakati wote. Jaribio la hotuba ya Rais kuwatweza viongozi wafanyakazi linaweza likaishia kuwakweza zaidi, jaribio la kuwachangonanisha wafanyakazi kuwa wanataka mishahara mikubwa wakati serikali inahitaji fedha za kutoa huduma kwa jamii ili wananchi wawajie juu wafanyakazi kuwa wanajipendelea nalo limeelekea kushindwa. Jaribu la kuwachonganisha wafanyakazi kwa wafanyakazi, wafanyabiashara kwa wafanyakazi( kwa kutumia mifano ya mwenye baa na mifano ya house girl) nalo limeelekea kupuuzwa. Taasisi ya Urais sio idara ya propaganda za kutumia kejeli ama uchonganishi; Rais alipaswa kujenga hoja, kutoa matumaini na kutoa uongozi mbadala.Hasira alizozionyesha kwa TUCTA ndio amekuwa amezionyesha kwa kiwango hicho hicho kwa mafisadi, na nguvu hizo hizo za kuzima hoja angekuwa amezitumia kwenye kutoa uongozi bora na kusimamia vizuri rasilimali za taifa mapato ya serikali yangewezesha kuwa na nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi na ukuaji wa uchumi ungewezesha hata kukuka kwa kipato katika sekta binafsi huku mfumuko wa bei ungedhibitiwa kwa kiwango cha kuridhisha. Wakati wafanyakazi wanaendelea kutozwa kodi kubwa(dai ambalo Rais hakulizungumzia), ni serikali yake hii ambayo iko mstari wa mbele kutoa katika mazingira ya utata misamaha mikubwa ya kodi.Kama divide and rule hii ikiindelea kwa kiwango cha wafanyakazi kushindwa kushikamana, bado kila mmoja anayo fursa ya kugoma kumpa kura (kwanza ameshatangaza mwenyewe kuwa kura hazitaki). Upo msemo kwamba madaraka hulevya, na madaraka zaidi hulevya zaidi; unapokuwa na taifa lenye hodhi (monopoly) ya chama kimoja katika vyombo vya maamuzi; si ajabu kupata kauli za namna hii. Hii ndio athari ya kura zilizoitwa za mafiga matatu; lakini ipo fursa bado ya kubadili mfumo wa utawala ili tuwe na uwajibikaji wa kutosha si kwenye sererikali tu, hata kwenye taasisi zingine ikiwemo vyama vya wafanyakazi vyenyewe.Kwa walio nje ya ajira zenye malipo duni suala hili wanaweza wakaona haliwahusu, lakini ukweli ni kuwa kuna uhusiano mkubwa katika ya ubovu wa huduma tunazozipata kwenye sekta mbalimbali na hali duni katika sekta hizo; hili ni bomu la wakati. Wafanyakazi wa Tanzania wamekuwa wawafanyi migomo rasmi kama nchi nyingine duniani, lakini aina ya mgomo unaoendelea chini kwa chini nchini ni mbaya zaidi kwa mustakabali wa nchi yetu. Tanzania kuna mgomo wa kutokuwajibika, katika hususani katika utumishi wa umma; wapo wanaokwenda kazini mwaka mzima lakini wanafanya kazi masaa machache au siku chache; muda mwingine kwenye warsha/semina kufidia kipato duni wanachopata ama muda mwingi zaidi kwenye shughuli zao binafsi. Mfano; walimu wenye wanaofundisha masomo ya ziada (tuition) ama kufanya biashara za visheti kwa wanafunzi shuleni; ama daktari anayetumia muda mwingi zaidi kwenye shughuli binafsi kuliko ndani ya hospitali ya umma, sasa 'consultancy' ndani ya serikali kwa serikali ndio zimekuwa utamaduni wa kawaida.Rais atangaze mshahara wake hadharani na atueleze baraza lake la mawaziri limeshughulikiaje madai makuu matatu ya wafanyakazi toka aingine madarakani mwaka 2005 badala ya kukimbilia kuwapa jina baya viongozi wa wafanyakazi kuwa 'wanatumiwa'. Kama kweli wanatumiwa atueleze wanatumiwa na nani kwa kwanini? Na yeye na serikali yake waulizwe 'wanatumiwa na nani' au wanamtumikia nani?

Posted by John Mnyika at 5:43 AM 0 comments Links to this post

Thursday, April 15, 2010

Mnyika: Uhamisho wa watumishi Mwananyamala ni wa kisiasa

Mnyika: Uhamisho wa watumishi Mwananyamala ni wa kisiasana Lucy NgowiMWENYEKITI wa Mkoa wa Kinondoni, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amesema suala la kuwahamisha watumishi 96 katika Hospitali ya Mwananyamala limefanywa kisiasa zaidi katika kipindi hiki kinachoelekea Uchaguzi Mkuu.Mnyika alisema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuongeza kuwa analiona suala hilo lipo kisiasa zaidi kwa kuwa hatua hiyo iliyochukuliwa imechelewa, kwani wananchi na vyama vya siasa wamekuwa wakililalamikia tangu mwaka 2005.Mnyika ambaye ni Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA, alisema upunguzaji huo si suluhisho la kudumu, ila kiutawala ni hatua inayopunguza tatizo kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa Mnyika, hatua ambazo zilipaswa kuchukuliwa ni pamoja na kubadili mfumo mzima wa utoaji huduma katika hospitali za umma kwa kubadili uongozi na kuongeza masilahi ya watumishi wa sekta hiyo.Mkurugenzi huyo wa vijana alisema kuwa hatua nyingine ni pamoja na kuboresha huduma kwa wananchi, hususan upatikanaji wa dawa.“Kuhamisha bila kushughulikia kero za msingi ni sawa na kiini macho. Serikali iweke wazi ripoti za tume na kamati zote zilizoundwa kuchunguza matukio yaliyokuwa yanajitokeza toka wakati huo, pamoja na kueleza gharama zilizotumiwa na tume ama kamati hizo bila mapendekezo kutekelezwa kwa ukamilifu,” alisema.Mwanzoni mwa wiki hii, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alisema kuwa, serikali imewahamisha watumishi 96 katika Hospitali ya Mwananyamala ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikilalamikiwa kwa uzembe.Chanzo: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=14932

Posted by John Mnyika at 11:51 AM 0 comments Links to this post

Thursday, March 25, 2010

Tamko letu kuhusu ajali ya leo Kata ya Kibamba Wilaya ya Kinondoni

Taarifa kwa Umma: Kwa niaba ya Uongozi wa CHADEMA Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum ya Dar es salaam; natuma salamu za rambi rambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wafiwa wote kufuatia ajali mbaya iliyotokea leo asubuhi Kibamba jijini Dar es salaam ikihusisha Lori la Mafuta na Hiece iliyokuwa na abiria.Aidha tunatoa mwito kwa serikali na vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina kuhusu vyanzo vya ajali za mara kwa mara katika eneo la Kibamba ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.Ikumbukwe kuwa mwezi Disemba mwaka 2007 ajali nyingine ilitokea eneo la Kibamba Hospital ikihusisha malori na kusababisha vifo vya watu saba akiwemo mjamzito na wengine 11 kujeruhiwa.Aidha mwezi Aprili 2008 Bunge jumla ya watu 181 wamepoteza maisha kwa kugongwa na magari kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2007 katika eneo la kuanzia Kibamba mpaka Ubungo kwenye mataa.Ikumbukwe kuwa Mei 2009 madereva wawili walikufa baada ya magari yao kugongana uso kwa uso huko maeneo hayo hayo ya Kibamba.

Itakumbukwa pia kwamba mwezi Januari 2010 watu 18 walijeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya Morogoro eneo la Kibamba Darajani (barabara ina mteremko kuelekea darajani) ambapo magari matano yaligongana kwa pamoja.Imetolewa tarehe 25 Machi 2010:John Mnyika-0754694553; mnyika@chadema.or.tz

Mwenyekiti wa Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum (CHADEMA)

Posted by John Mnyika at 3:31 AM 0 comments Links to this post

Saturday, March 20, 2010

Natangaza rasmi dhamira ya kugombea ubunge 2010

Ni wakati wa mabadiliko ya kweli; tuwajibikeUtanguliziWapendwa wananchi wezangu na marafiki zangu ndani na nje ya jimbo la Ubungo. Ninayofuraha kuwatangazia rasmi dhamira yangu ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Nimefikia uamuzi huu baada ya kusikia maoni ya wengi wenu na kuisikiliza pia nafsi yangu katika kipindi cha kuanzia mwishoni mwa mwaka 2009 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2010. Wakati wa kampeni bado, hivyo sitazungumzia kwa sasa ahadi zangu kwenu wala ilani ya chama; lakini inatosha kuwaambia tu kwamba: ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike. Naamini katika kuwa na uongozi bora wenye dira na uadilifu wa kuwezesha uwajibikaji katika kusimamia rasilimali za umma ikiwemo kodi zetu na mali asili za nchi yetu kwa ajili ya kujenga taifa lenye kutoa fursa kwa wote.

Nautambua wajibu; tushirikianeNaamini kwamba mbunge (ambaye pia kwa nafasi yake ni diwani katika halmashauri) ana wajibu katika maeneo makuu manne (kwa kadiri ya umuhimu).Mosi; kusikiliza na kuwakilisha wananchi, Pili; kuisimamia na kuiwajibisha serikali na viongozi wake, Tatu; kushiriki katika kutunga sheria, Nne; kuhamasisha upatikanaji wa huduma.Hata hivyo, sehemu kubwa ya wabunge wetu hawaweki kipaumbele katika majukumu ya kwanza matatu ambayo ndio msingi wa ubunge wenyewe. Matokeo yake ni matakwa ya wananchi kutokuwakilishwa kikamilifu, ufisadi, rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na mikataba mibovu; uwepo wa sheria dhaifu na kutetereka kwa utawala wa sheria na mifumo ya haki masuala ambayo yanakwaza jitihada za maendeleo za wananchi binafsi za taifa kwa ujumla.Wabunge wengi wanawaza kwamba jukumu kubwa la mbunge ni kutoa bidhaa na huduma kwa wananchi; wakiacha taifa katika lindi la umasikini na kufanya sehemu ya wananchi kujenga mazoea ya kutegemea hisani toka kwa viongozi wa umma na wafadhili wao.Mwaka 2005 pamoja na majukumu hayo makuu matatu, nilizungumzia suala la mfuko wa maendeleo ya jimbo. Lakini si katika mwelekeo wa mfuko wa sasa uliopitishwa kuwa sheria unaosubiriwa kutungiwa kanuni. Kwa hiyo, wakati nikiunga mkono jukumu la mbunge kuhamasisha maendeleo na kushiriki kwenye shughuli za kijamii, siamini katika mazoea na mfumo wowote unaomfanya mbunge kuwa “mtoa bidhaa na huduma” (mithili ya ATM) kwani unarutubisha ufisadi wa kisiasa na kuhatarisha mwelekeo mzima wa utawala bora. Kama ambavyo siamini pia katika siasa chafu za rushwa, uongo na aina nyingine ya upofu wa kimaadili katika kampeni na uongozi kwa ujumla.Haiwezekani wakati ambapo makisio yanaonyesha kwamba zaidi ya trilioni mbili (sawa na milioni milioni mbili) zinapotea kila mwaka kupitia misamaha ya kodi, upangaji bei hovyo kwa bidhaa za Tanzania, biashara haramu kati ya Tanzania na nchi za nje au makampuni ya kimataifa halafu wananchi wakubali kupumbazwa na bidhaa za milioni chache zinatolewa na viongozi wa umma walioshindwa kurekebisha hali hii.Nilisema wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005, na narudia leo. Kipaumbele cha wananchi wa Jimbo la Ubungo ni kupata mbunge mkweli, mwadilifu, mwajibikaji, mwenye dira, atayewasilikiliza na kuwawakilisha ipasavyo. Iwe ni wananchi wa Kwembe, Mloganzila na maeneo mengine yenye migogoro ya ardhi. Ama wale wa Saranga, Baruti na kwingineko kwenye matatizo ya maji huku mabomba makubwa ya maji yakipita jimboni na uwepo wa Chuo cha Maji, na Wizara ya Maji ndani ya jimbo letu. Iwe ni wale Bonyokwa, Mpiji Magoe na kote kwenye udhaifu wa mipango miji na matatizo ya usafiri huku Chuo cha Usafishaji cha Taifa kikiwa ndani ya jimbo hili hili.Iwe ni wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki hapa Ubungo ama wa sekta umma na wa binafsi waoishi ndani ya jimbo hili wenye kubebeshwa mzigo mkubwa wa kodi na kuzongwa na maslahi duni. Iwe ni wafanyabiashara ndogo ndogo wanawake kwa vijana pale Manzese, Makurumla na kwingineko; iwe ni wanafunzi wa sekondari na vyuo Mbezi na Ubungo ambao kwa ujumla wake wanaishi katika mazingira yenye mifumo dhaifu yenye kudorora kwa ubora na upatikanaji nafuu wa huduma za kijamii.Iwe ni mwananchi wa Jimbo la Ubungo anayeathirika kwa bei na mgawo wa umeme huku akipita na kuona mitambo ya kampuni feki ya Dowans inayotakiwa kurejesha mabilioni iliyolipwa mara mbili (double payment) na serikali; mitambo ambayo imeendelea kukaa pembeni na makao makuu ya TANESCO yaliyopo jimbo la Ubungo bila kutaifishwa. Iwe ni mtanzania wa kawaida anayeelemewa na mzigo wa kodi na kupanda kwa gharama za maisha. Wote wanahitaji mbunge wa kuwasikiliza, kuwawakilisha, kushiriki kutunga sheria bora na kuziwajibisha mamlaka zinazohusika. Tanzania bila mafisadi inawezekana. Huu si wakati wa kuahidi nitafanya nini kwa kuwa si kipindi cha kampeni. Ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike.

Tunahitaji mabadiliko ya kweli kuliko ahadi kedekede utekelezaji legelegeNatambua kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (pamoja na ubovu wake) imetaja katika ibara ya 9 Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha: kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa; kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa; kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumyonya mtu mwingine; kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja; kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini; kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi. Misingi hii na mingine, haitekelezwi wala kuzingatiwa kikamilifu kutokana na ombwe la uongozi, udhaifu wa kitaasisi na upungufu wa uwajibikaji. Ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike.Aidha naelewa kuwa katiba hiyo hiyo (pamoja na mapungufu yake) inatamka katika Ibara ya 63 kifungu cha pili na cha tatu kuwa Bunge ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kupitia maswali, mijadala, kuidhinisha mipango (zikiwemo bajeti), kutunga sheria na kuridhia mikataba.Madaraka hayo ya bunge na majukumu ya wabunge hata baada ya uongozi wa awamu ya nne kuahidi kuyatekeleza kwa ari, nguvu na kasi mpya na Spika wa Bunge kuahidi kuyasimamia kwa kasi na viwango; hali kwa sehemu kubwa iko vile vile; ahadi kedekede, utekelezaji lege lege.Hasara kwa taifa iliyotajwa kwenye orodha ya mafisadi (list of shame) na ile inayotokana na ufisadi kwenye serikali za mitaa pekee kwa ujumla wake inafikia takribani trilioni mbili. Hivyo Tanzania ni nchi tajiri wa rasilimali huku wananchi walio wengi wakiishi katika lindi la umasikini na ugumu wa maisha.Naamini hali hii inachangiwa na kufilisika kiitikadi na kidira kwa chama tawala, hodhi (monopoly) ya chama kimoja bungeni, bunge kukosa uhuru wa kikatiba na udhaifu wa taasisi za kusimamia uwajibikaji. Hali hii inachochewa pia na udhaifu wa kiuongozi ikiwemo uzembe wa sehemu kubwa ya wabunge wengi wao wakiwa wameingia kwa nguvu ya ufisadi katika uchaguzi wa mwaka 2005 na hivyo kukosa nguvu ya kimaadili na dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli. Hata wale wachache wenye dhamira ya kufanya mabadiliko wanadhibitiwa na kamati za chama chao (party caucus) chenye mmomonyoko wa kimaadili. Hivyo, harakati za ukombozi zinapaswa kuungwa mkono na watanzania wote wakiwemo wanachama wa chama hicho wanaokerwa na hali ya mambo. Ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike.

Tuchukue hatua; kwa pamoja tunawezaJukumu lililo mbele yetu la kuwezesha mabadiliko ya kweli ni kubwa linalohitaji hatua za haraka kujitoa sadaka na kutumia talanta kuanzia sasa mpaka wakati wa uchaguzi Oktoba 2010; kabla ya majukumu makubwa zaidi kuanzia wakati huo na kuendelea. Kwa pamoja tunaweza, pamoja tutashinda.Hatua ya kwanza ni kuhakikisha kila mmoja mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea ama atayefikisha umri huo wakati wa uchaguzi kama bado hajajiandikisha anajitokeza kujiandikisha katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura unaonza katika Mkoa wa Dar es salaam kuanzia kesho tarehe 22 mpaka 27 Machi, 2010 ikiwa ni awamu ya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu. Aidha kwa waliohama makazi, huu ndio wasaa mwafaka pia wa kwenda kubadilisha taarifa zenu ili muweze kupiga kura katika maeneo mliyopo.Hatua ya pili ni kushiriki kwa hali na mali katika kujenga oganizesheni ya chama mbadala. Kuhamasisha wagombea mbadala kujitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali, kuwaunga mkono na kueneza ujumbe wa matumaini wa mabadiliko kwa watanzania wengine katika maeneo yenu. Izingatiwe kuwa kipindi cha kuanzia mwezi Aprili mpaka Julai ni cha wagombea kuonyesha nia, kuchukua fomu ndani ya vyama, kampeni za ndani ya vyama, kuingia katika kura za maoni na uteuzi kufanywa na vyama vyao kwa kuwa serikali mpaka hivi sasa imekataa matakwa ya umma ya kutaka wagombea binafsi waruhusiwe.Kampeni kwa umma zinatarajiwa kuanza baada ya wagombea kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwezi Agosti na zinatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka 2010. Hatua muhimu wakati huo ni pamoja na kushiriki katika kampeni kwa hali na mali, kupiga kura na kuunganisha nguvu ya umma katika kulinda kura. Ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike.Haturudi nyuma kamwe; matumaini yapo mbeleMwaka 2005 Mwezi Machi kama huu nilipochukua fomu kwa mara ya kwanza kugombea ubunge, CHADEMA haikuwa na mtandao imara katika jimbo la Ubungo tofauti na sasa ambapo ina mtandao madhubuti na ipo fursa bado ya kuufanya kuwa mzuri zaidi. Ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike.Hivyo Disemba 2005 (pamoja na kukubalika kwa wananchi) baada ya mvutano wa siku kadhaa matokeo ya uchaguzi yalitangazwa kwa shuruti bila kupitia utaratibu wa kupitia na kujumlisha kituo hadi kituo na kufanya jumla ya wapiga kura waliotangazwa kupiga kura katika ubunge kuzidi wale waliopiga kura za urais kwa zaidi ya kura elfu thelathini (30,000) katika uchaguzi uliofanyika katika siku moja.Kutokana na hujuma hizo na nyinginezo zilizohusisha pia ufisadi katika uchaguzi niliamua kufungua kesi namba moja ya mwaka 2006 katika Mahakama Kuu kupinga matokeo hayo. Kesi ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikipigwa danadana za kiufundi bila kuingia katika kusikiliza msingi wenyewe wa kesi.Wakati najiandaa kutangaza rasmi dhamira ya kugombea nikitazama mbele kwa matumaini, nimepokea simu toka kwa Wakili wangu katika kesi hiyo Ndugu Tundu Lissu akinieleza kwamba hatimaye Mahakama Kuu imepanga kuwa kesho tarehe 22 Machi 2010 ndio siku ambayo mahakama itatoa hukumu juu ya kesi hiyo.Bila kuingilia uhuru wa mahakama, nieleze wazi tu kwamba kwa mtiririko wa mambo mpaka sasa hukumu hiyo itahusu zaidi ombi langu la kuondolewa kuweka dhamana ya milioni tano kama sharti la kufungua kesi na kupita kwa muda toka kesi ifunguliwe badala ya utata wa matokeo na kasoro za uchaguzi husika.Hata hivyo kwa miaka takribani mitano ambayo nimekuwepo katika siasa na kushiriki katika chaguzi mbalimbali za kiserikali, mmoja nikiwa kama mgombea na zingine nikiwa kwenye timu za kampeni nimejifunza kuwa pamoja na uwepo wa katiba na sheria mbovu zenye kusababisha tume ya uchaguzi kutokuwa huru na kukosekana kwa uwanja sawa wa kisiasa kwa ujumla; bado vyama mbadala vinaweza kuunganisha nguvu ya umma kupata kura nyingi na kushinikiza mshindi kutangazwa pale ambapo kunakuwa na mikakati thabiti, oganizesheni makini na uongozi mahiri. Ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike.Naweza nikalazimika kutangaza upande wa kugombeaTunahitaji mabadiliko ya uongozi na mfumo wa utawala ili kutumia vizuri kodi za wananchi na rasilimali za taifa kuwa na miundo mbinu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kuwezesha ustawi wa wananchi.Badala ya kuelekeza nguvu zaidi katika azma hii, serikali ya sasa inaongeza nguvu katika matumizi ya anasa na mzigo mkubwa wa gharama za utawala na sasa inajadili kuongeza zaidi idadi ya wabunge.Mathalani mwaka wa fedha 2009/2010 kiasi cha bajeti kilichotengwa kwa ajili ya Bunge ni shilingi bilioni 62 ambayo ni sawa na wastani wa zaidi ya milioni 190 kwa kila mbunge kwa mwaka. (Pato la mtumishi wa umma wa kima cha chini halifiki hata asilimia 1% ya fedha hizo).Ndio maana binafsi siungi mkono ongezeko la majimbo lisiloangalia tija na ufanisi wa wabunge katika kutimiza majukumu ya msingi ya kibunge. Kwa mtizamo wangu, tunapaswa kupunguza idadi ya majimbo ya uchaguzi badala ya kuyaongeza kwa kufanya wilaya za sasa za kiutawala ndio ziwe kitovu cha mgawanyo wa majimbo.Mathalani, wilaya ya Kinondoni badala ya kuwa na majimbo matatu ya Kawe, Kinondoni na Ubungo iwe na jimbo ni jimbo moja tu la Kinondoni. Badala yake Halmashauri ya Kinondoni bila kushirikisha vyama vya siasa ilipeleka mapendekezo kwa Baraza la Mashauriano la Mkoa (RCC) wa Dar es saaalam ambalo nalo limepeleka mapendekezo ya kugawa majimbo kadhaa ya mkoa huu likiwemo jimbo la Ubungo.Kwa mujibu wa mapendekezo yao Kata za Kimara, Makuburi, Mbezi na Kibamba zimependekezwa kuwa kwenye jimbo la Kibamba toka Jimbo la sasa la Ubungo. Kwa msingi huo wanapendekeza sasa jimbo la Ubungo libaki na kata za Mabibo, Manzese, Makurumla, Ubungo, Sinza na Mburahati na kuongezewa pia kata ya Kigogo (ambayo kwa sasa iko ndani ya Jimbo la Kinondoni).Kwa hiyo, pamoja na kutangaza dhamira yangu ya kugombea ubunge katika eneo ambalo ni Jimbo la Ubungo; haiwezekani kwa sasa kutangaza kwa hakika nitagombea katika jimbo gani mpaka pale Tume ya Uchaguzi itakapotangaza maamuzi yake kuhusu mgawanyo wa majimbo baada ya kupokea mapendekezo hayo toka kwa serikali. Iwapo Tume ya uchaguzi italigawa jimbo la Ubungo nitalazika kutangaza upande ambao nitagombea. Ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike.

Hitimisho:Maneno na matendo yangu katika harakati za umma katika kipindi cha mwaka 2000 mpaka 2005 wakati nikiwa kwenye uongozi wa kijamii katika asasi za kiraia na katika kipindi cha mwaka 2005 mpaka 2010 nikiwa kiongozi wa kisiasa yanaweza kurejewa kama msingi wa kuashiria ni watu gani nitawawakilisha na masuala gani nitayasimamia katika uongozi wa umma kabla hata sijateuliwa rasmi na kutoa hotuba katika kampeni. Naomba uwasiliane nami kwa kunitumia ujumbe kupitia johnmnyika@gmail.com au 0784222222 tuwe pamoja hatua kwa hatua katika safari ya ushindi. Ni wakati wa Mabadiliko; tuwajibike mpaka kieleweke.Wenu katika demokrasia na maendeleo;
Mnyika apitishwa kwa 100% Ubungo


MGOMBEA wa Ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. John Mnyika amepitishwa na na chama chake kugombea jimbo hilo kwa asilima 100.Bw. Mnyika alipitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa jimbo hilo baada ya wajumbe wote 62 kumpa kura ya ndiyo.Wajumnbe waliohudhuria katika mkutano huo ni Wenyeviti na makatibu wote wa jimbo hilo, wageni waalikwa 60 na wawakilishi wa vyuo vikuu walioko Ubungo na wawakilishi wa matawi ya CHADEMA katika jimbo hilo.Wakati huo huo, Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limemtaja, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa kuwa shujaa baada ya kukubalia maombi ya Kamati Kuu ya kugombea urais wakati baado alikuwa anahitajika katika jimbo lake.Akizungumza katika mkutano wa wakilishi wa vyuo vikuu Mweyekiti wa Kamati ya baraza hilo, Bw. John Mnyika alisema kitendo alichofanya Dkt. Slaa cha kuachia jimbo ambalo alikuwa na uhakika wa kushinda katika Uchaguzi Mkuu ni la kishujaa."Tunakutana leo kwa kuwa tendo alilofanya Mtanzania mwenzetu, Dkt. Slaa kukubali kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni la kishujaa," alisema Bw. MnyikaAlisema Dkt. Slaa ni sawa mashujaa waliokubali kupoteza maisha yao na kulilinda na kuliteta taifa na hivyo ni shujaa wa demokarsia na maendeleo.Alisema mashujaa wa namna ya Dkt. Slaa hawafii kwa kuwa fikra zao zitakumbukwa milele uamuzi wa huo utandika historia mpya kwa taifa ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo misingi ya CHADEMAAlisema Bendera ya chama hicho ni rangi ya nyekundu, nyeupe bluu, bahari na nyeusi uwepo kwa rangi nyekundu unatoka na kuthamini mashujaa wa nchi walipigana vita ili kulikomboa taifa hili.Alisema maadhimisho yanayofanywa na serikali Julai 25 kila mwaka kuwakumbuka mashujaa ni unafiki kwa kuwa hufanywa kwa maneno na si wa kivitendoAlisema tunu ya taifa hili ziko kwenye ngao ya taifa ambayo ni Uhuru na Umoja lakini uhuru umetoweka na nchi imekuwa tegemezi kwa kuwa sehemu kubwa ya rasilimli zake zimeuzwa kwa bei ya kutupwa kwa wageni na sehenu kubwa ya Watanzania hawafaidi nayoAlisema umoja umetelemshwa kutokana na kupuuzwa utawala wa sheria kumea kwa ubaguzi na kupanuka kwa matabaka katika jimii kwenye sekta mbalimbali za afya, elimu na hata mifumo ya haki hali ambayo ni tishio la ustawi na usalama wa nchi.Alisema Dkt. Slaa ametimiza wajibu huo kwa kusimamia ukweli, uwazi, uadilifu na amani kama rangi nyeupe katika bendera ya CHADEMA inayowakilishwa hususani kupitia ngazi ya ubungeni katika jamii na jimboni kwake karatuBw Mnyika alisema umefika wakati wa Dkt. Slaa kuinuliwa na kupewa wajibu mkuu zaidi katika nchi wa ili kuunda serikali na kusimamia utekelezaji ilikurudisha nchi kwa wananchi.Chanzo: Gazeti la Majira 26/07/2010

Posted by John Mnyika at 4:43 AM 0 comments Links to this post

Mnyika apita kwa kishindo ubungo

HATIMAYE Mkurugenzi wa Mambo ya Nchi za Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amepitishwa kuwania ubunge wa Jimbo la Ubungo kwa kupata ushindi wa asilimia mia moja kwenye kura za maoni.Kwa mujibu wa matokeo ya kura za maoni za CHADEMA katika Jimbo la Ubungo yaliyotolewa na Nassor Balozi, Mnyika aliyekuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo alipata kura za ndiyo 62 zilizopigwa na wajumbe wote 62 waliohudhuria mkutano mkuu wa jimbo hilo.“Mkutano mkuu umepiga kura za ndiyo na hapana na kati ya wajumbe 62 wote wamepiga ndiyo, hakuna hapana, hakuna iliyoharibika. Hivyo John Mnyika amepitishwa na kura hizo za uteuzi kwa asilimia 100,” alisema Balozi.Wajumbe wa mkutano huo walikuwa ni wenyeviti na makatibu wote wa CHADEMA Jimbo la Ubungo.Aidha, mkutano huo pia ulishirikisha wageni waalikwa 60 ambao ni wawakilishi wa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu vilivyomo ndani ya Jimbo la Ubungo pamoja na wawakilishi wa matawi ya chama hicho Jimbo la Ubungo.Akizungumza baada ya matokeo hayo, Mnyika alisema alitarajiwa kupitishwa kugombea ubunge na mkutano huo lakini hakutegemea kupitishwa kwa asilimia 100 kama ilivyotokea na kuielezea hali hiyo kuwa ni kielelezo cha CHADEMA kuwa moja zaidi ndani ya jimbo hilo.“Kwa matokeo hayo wamenipa changamoto kubwa, lakini pia ni changamoto kwao katika kuhakikisha wanaitekeleza imani yao kwangu kwa vitendo kwa kushiriki kikamilifu katika harakati zote za kutupatia ushindi,” alisema Mnyika.Mnyika anayewania ubunge wa jimbo hilo kwa mara ya pili baada ya kudaiwa kushindwa kwa mizengwe katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alisema vipaumbele vyake ni kupigania ajira na maslahi ya wafanyakazi, miundombinu bora ya maji, barabara na makazi, kuchochea uwajibikaji wa watendaji wa serikali, idara na mamlaka zake pamoja na kufanikisha upatikanaji wa huduma bora za afya ndani ya jimbo hilo.Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima-26/07/2010

Posted by John Mnyika at 4:32 AM 0 comments Links to this post

Saturday, July 24, 2010

HOTUBA: Ufunguzi wa Mkutano wa BAVICHA na Wanavyuo

HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA (BAVICHA) JOHN MNYIKA AKIFUNGUA MKUTANO WA WAWAKILISHI WA WANAVYUO VIKUU VYA MKOA WA DAR ES SALAAM KATIKA VIWANJA VYA MAKAO MAKUU YA CHAMA KINONDONI JUMAPILI TAREHE 25 JULAI 2010Vijana wenzangu wanavyuo;Wageni waalikwa na wanahabari;Ni mara yangu ya kwanza leo kuhutubia vijana wenzangu toka Kamati Kuu ya chama katika kikao chake cha tarehe 25 mpaka 26 Aprili 2010 iliponiteua kuongoza Kamati ya taifa ya BAVICHA katika kipindi hiki mpaka uchaguzi wa vijana utapofanyika baada ya uchaguzi mkuu.Nimeupokea wajibu huu kwa moyo mkunjufu kwa kuwa umenikumbusha kipindi nilichokuwa Mkurugenzi wa Vijana na hakika ni jukumu muhimu kwa chama hiki cha kizazi kipya wakati huu ambapo ubunifu, uwingi na uthubutu wa vijana unahitajika kuwezesha mabadiliko katika taifa letu.Awali ya yote naomba tusimame kwa dakika moja ya ukimya kuwakumbuka mashujaa waliomwaga damu yao na kutangulia mbele ya haki wakiwa katika wajibu wa kulinda na kutetea ardhi ya nchi yetu na watu wake.Nashukuru tumekutana leo tarehe 25 Julai ambayo ni siku ya mashujaa nchini kujadili matendo ya kishujaa yaliyofanywa na yanayokusudiwa kufanywa katika taifa letu.

Tunakutana leo kwa sababu ya tendo la kishujaa la mtanzania mwenzetu Dr Wilbroad Slaa kukubali ombi la kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tendo hili la kishujaa la kuachia jimbo la uchaguzi ambalo alikuwa ana uhakika wa kuletetea na badala yake kugombea nafasi ya urais ambayo baadhi ya watu wametafsiri kama ni ‘kuuawa ama kujiua’ kisiasa.Kama vile mashujaa walivyokubali kupoteza maisha yao kulilinda na kulitetea taifa, ndivyo ambayo Dr Slaa ni shujaa wa demokrasia na maendeleo kwa kufanya tendo ambalo linaweza kutafsiriwa kuwa ni kutishia maisha yake ya kisiasa hususani katika bunge kwa kuamua kugombea nafasi ya Urais kutokana na kuweka mbele maslahi ya taifa kwanza.

Mashujaa wa aina hii huwa hawafi kwa kuwa fikra zao hukumbukwa milele, uamuzi wa Dr Slaa kujitokeza kugombea wakati huu utaandika historia mpya kwa taifa la Tanzania. Uamuzi huu wa kishujaa ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo misingi ya CHADEMA ambayo inaweza kueleweka vizuri zaidi kupitia bendera anayoipeperusha.Bendera ya CHADEMA ina rangi nne; nyekundu, nyeupe, bluu bahari na nyeusi. CHADEMA ikiwa ni chama kinachothamini mashujaa wa nchi hii imeweka rangi nyekundu katika bendera yake ambaye imefafanuliwa vizuri katika katiba na kanuni za chama kwamba ni ishara uzalendo na upendo kwa taifa.Leo tarehe 25 Julai wakati sisi tukiwa hapa kwenye mkutano huu viongozi wa kiserikali wako kwenye viwanja vya mnazi mmoja wakifanya maadhimisho ya kinafiki ya kuwakumbuka mashujaa kwa maneno huku kwa vitendo wakiwa wamewasahau na kusahau misingi waliyoisimamia.Tunu za taifa hili zilizoko kwenye ngao ya taifa ni “Uhuru na Umoja”, hata hivyo tunavyozungumza hivi sasa uhuru huu umetoweka kwa nchi kuwa tegemezi na rasilimali kwa sehemu kubwa kuuzwa kwa bei ya kutupwa kwa wageni huku sehemu kubwa ya watanzania ikiwa hainufaiki na matunda ya uhuru kutokana na kufungwa na kongwa za umasikini, ujinga, maradhi na ufisadi. Tanzania imegeuzwa chanzo cha malighafi ghafi, soko la bidhaa duni toka nje chini ya soko holela na watawala kukiunga misingi ya uongozi.Kwa upande mwingine misingi ya umoja inazidi kutetereshwa kutokana na kupuuzwa kwa utawala wa sheria, kumea kwa ubaguzi na kupanuka kwa matabaka katika jamii kwenye sekta mbalimbali iwe ni afya, elimu na hata mifumo ya haki hali ambayo ni tishio kwa ustawi na usalama wa nchi yetu. Hali hii inahitaji mashujaa kujitokeza kutanguliza mbele uzalendo na upendo kwa taifa ili kulikomboa taifa kwa kuleta mabadiliko ya kweli ya uongozi na mfumo mzima wa utawala.Dr Slaa ametimiza wajibu huo kwa kusimamia ukweli, uwazi, uadilifu na amani kama rangi nyeupe katika bendera ya CHADEMA inavyowakilisha hususani kupitia kazi yake bungeni, katika jamii na jimboni Karatu katika kipindi cha utumishi wake. Hata hivyo baadhi ya mambo hayajaweza kutekelezwa na serikali iliyopo madarakani kutokana na dola chini ya CCM kutekwa na mafisadi na kuwa na mfumo legelege wa uongozi uliofilisika kidira na kimaadili.Umefika wakati sasa wa Shujaa huyu kuinuliwa kupewa wajibu mkuu zaidi katika nchi yetu wa kuwa Rais wa Tanzania aweze kuunda serikali na kusimamia utekelezaji ili kurudisha nchi kwa wananchi. Ndio maana tunaunga mkono uamuzi wa Kamati kuu ya chama iliyoketi tarehe 20 Julai kumwomba kugombea urais ili ajaze fomu na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa chama tarehe 20 Agosti 2010.Na kabla ya kuanza kuutekeleza wajibu huo akiwa ikulu, uchaguzi ambao kampeni zake zinaanza rasmi tarehe 20 Agosti mpaka 30 Oktoba kabla ya kupiga kura tarehe 31 Oktoba ulipaswa kuwa na mgombea wa uwezo wa Dr Slaa ili uwe sehemu ya mchakato wa kuiwajibisha serikali wakati wote wa kampeni. Dr Slaa akiwa mgombea urais uchaguzi utakuwa ni mchakato wa pekee wa kusambaa kwa elimu ya uraia kwa umma, kuunganisha watanzania bila kujali itikadi katika kuleta mabadiliko, kuibua uozo uliopo na kutoa sera mbadala zenye kuleta tumaini jipya la watanzania kupitia chama na uongozi mbadala. Mchango huu wa kishujaa kwa taifa utapanda mbegu ya mabadiliko ya kisiasa na kuliondoa taifa kutoka kwenye lindi la mazoea ya ufisadi kwa kuhamasisha utamaduni wa uwajibikaji.Katika kampeni hizo kama sehemu ya dhamira ya pamoja ya kuondoa ukiritimba na hodhi ya chama kimoja kwenye vyombo vya maamuzi Dr Slaa kuwa mgombea urais kwa uzoefu na makini atazunguka nchi nzima kuwanadi wagombea udiwani na ubunge na kuwaongeza nguvu ili tuweze kuwa na wakina Dr Slaa wengi zaidi wazee kwa vijana katika halmashauri na bungeni.Viongozi hawa mbadala wataweza kujenga taifa lenye kutoa fursa na kutumia vizuri rasilimali za taifa iwe ni mali asili, kodi, utaalamu na vipaji vya watanzania katika kuwezesha maendeleo ya mwanachi kwa ujumla na taifa kwa ujumla kupitia chama mbadala. CHADEMA ikiwa ni chama mbadala kinatambua umuhimu wa kutumia vyema rasilimali katika sera zake na misingi yake, hivyo Dr Slaa atapeperusha bendera ya chama rangi ya bluu bahari ikiwa inawakilisha haki na rasilimali za taifa hususani maji.Maneno yoyote ya kupingana mwelekeo huu wenye kutanguliza taifa kwanza iwe ni kwa nia njema inayosukumwa na hofu ya ombwe la Dr Slaa bungeni au mashaka ya pengo lake Karatu ama dhamira mbaya ya wapambe wa Kikwete za kuhadaa nafsi za watanzania yanapaswa yapingwe kwa matendo ya wote wenye kuitakia mema nchi yetu kwa kumuunga mkono Dr Slaa kwa hali na mali.Ndio maana napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza vijana wenzangu wasomi wa vyuo vikuu mlioona mbali kabla hata ya kamati kuu kukaa tarehe 20 Julai kwa kutumia ubunifu na uthubutu wa kuweka saini (petition) ya kumwomba kugombea. Naamini kamati kuu ilizingatia kuwa demokrasia ni utawala wa watu kwa ajili ya watu na kukubaliana na wito wenu na wa makundi mengine katika jamii wakiwemo wanachama wa CHADEMA wa kumuomba kugombea.Tanzania bila CCM inawezakana kila mtu akitimiza wajibu; hivyo nashukuru kwamba baada ya kufanikisha hatua ya kwanza leo mmeomba kukutana nasi kwa hatua ya pili ya kujadiliana namna ya kufanikisha ushindi.Hivyo ukiondoa hotuba hii ya ufunguzi leo hakutakuwa na mada za viongozi badala yake tutasikiliza kutoka kwenu mawazo yenu na namna ambavyo mmejipanga kumuunga mkono Dr Slaa katika azma ya kuleta mabadiliko tunayoyataka.Karibuni katika viwanja vya ofisi ya chama chenye fikra za kuamini katika falsafa ya “Nguvu ya Umma” ambayo inakilishwa na rangi nyeusi katika bendera yetu ambayo ni ishara ya utu wetu: kwamba umma ndio wenye mamlaka juu ya viongozi; umma ndio wenye wajibu wa kuamua hatma ya maisha yao na ya taifa; na umma ndio unaopaswa kunufaika na rasilimali za nchi yetu.Ni falsafa hii hii ndio tutakayotumia kuwezesha ushindi wa Dr Slaa na ushindi wa wabunge na madiwani mbadala kwa vijana kuwa mstari wa mbele kugombea ama kuunga mkono wagombea ikiwemo kutafuta na kulinda kura kwa kupitia pia falsafa ya Baraza la Vijana wa CHADEMA(BAVICHA) kwamba: Vijana; Nguvu ya Mabadiliko.Serikali yenye woga wa mabadiliko inayotawala kwa hujuma imetoa waraka na kuziingilia ratiba za vyuo husasani vya umma na kufanya vifunguliwe baada ya uchaguzi kwa hoja kanyaboya na hivyo kukwamisha baadhi yenu kupata haki ya msingi ya kikatiba ya raia ya kupiga kura pamoja na kuwa mlishajiandikisha tayari. Aidha ratiba hii ina dalili zote za kukwepa mshikamano wa wasomi wakati wa uchaguzi kwa kila mtu kuwa likizo katika hali inayoweza kutafsiriwa kuwa ni mpango wa ‘wagawe uwatawale’.Hata hivyo, ni wakati wa vijana kuwaambia watawala kuwa ‘hatudanganyiki wala hatugawanyiki’, uamuzi wenu wa kukukutana wawakilishi wa wanavyuo mbalimbali kabla ya kutawanyika ili kuunganisha nguvu ya pamoja umefanyika katika wakati muafaka.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba dhima ya wasomi na kama wajibu wa mtu aliyepewa chakula aweze kupata nguvu ya kwenda kuleta chakula kwa ajili ya wengine katika kijiji chenye njaa; mtu kama huyo asiporudi ni msaliti.Ni wajibu huu ndio unaopaswa kuwasukuma maeneo yoyote ambayo mtakuwa muifuatilie fursa yenu ya kupiga kura na kufanya hivyo, lakini mnawajibu mkubwa zaidi wa kutafuta kura nyingine nyingi zaidi kwa kuwaelimisha watanzania wengine na kuongoza harakati za mabadiliko ya kweli.Katika kushinda uchaguzi vipo vipaumbele vinne ambavyo naomba nivitaje kwa kadiri ya umuhimu wake kama sehemu ya kuibua majadiliano yetu siku ya leo; mosi, mgombea; pili, ajenda; tatu, oganizesheni na nne; rasilimali.Kwa upande wa Urais mgombea tayari tunaye ambaye anasubiri tu kuthibishwa na mkutano mkuu baada ya michakato kukamilika; wa upande wa ubunge na udiwani pia katika maeneo mbalimbali ya nchi wapo wagombea wamejitokeza ingawa milango bado iko wazi kwa kuwa tarehe ya mwisho ya uchukuaji na urudishaji fomu ndani ya chama ni tarehe 9 Agosti kabla ya uteuzi wa kiserikali Agosti 19. Kwa bahati njema pia sehemu kubwa ya wagombea ni vijana wenzetu na wazee wenye kutaka mabadiliko. Hivyo mnawajibu wa kwenda kuwaunga mkono wagombea katika maeneo ambayo mnakwenda.Kipaumbele cha pili ni ajenda za kisiasa ambazo katika uchaguzi huwekwa katika ilani. Tayari kamati kuu ya chama imepokea rasimu ya ilani na mchakato wa kuiboresha unaendelea kwa kuzingatia mawazo na maoni mbalimbali unaendelea mpaka itakapopitishwa na Mkutano Mkuu wa chama Agosti 12 mwaka huu. Hivyo, nyinyi kama vijana wasomi wa kada za mbalimbali mna wajibu wa kushauri hoja za kuwekwa kwenye ilani katika sekta mbalimbali ambazo mmezisomea na mnaendelea kuzisomea kwa kuzingatia pia hali halisi ya taifa na watanzania kwa sasa. Majadiliano ya leo yatawezesha kuanza kupokea maoni yenu si tu ya kuchambua hali ilivyo chini ya uongozi wa CCM bali pia kupendekeza CHADEMA ifanyeje pindi ikiingia katika uongozi ama ni Tanzania ya namna gani mngependa ijengwe na chama mbadala. Pamoja na kuwa CHADEMA inazo sera zake na mwaka 2005 ilikuwa na ilani ambayo mnaweza kuirejea kupitia www.chadema.or.tz bado tunaamini kwamba chama cha siasa kina wajibu wa kuwasikiliza wananchi badala ya kujifungia na kuandaa ilani zisizosingatia hali halisi ya taifa.Kipaumbele cha tatu ni oganizesheni ya kampeni ikiwemo mikakati mbalimbali ya kujipenyeza katika jamii kwa kutumia mbinu na timu mbalimbali. Hivyo, natarajia kikosi hiki kitasambaa katika maeneo mbalimbali na kutumia ubunifu, nguvu, uwingi na uthubutu wa vijana kufanya kampeni za kipekee kama ambavyo mtabadilishana mawazo katika mkutano wa leo. Tanzania bila CCM inawezekana kila mmoja akitimiza wajibu.

Kipaumbele cha nne ni rasilimali, izingatiwe kwamba tayari CCM imeshaanza na imejipanga kutumia nyenzo ikiwemo za dola/serikali na fedha nyingi zikiwemo za ufisadi na ubadhirifu katika kulazimisha ushindi kwa ushahidi wa nyaraka ambazo binafsi ninazo mpaka sasa ambazo zitatolewa katika wakati muafaka. Ni wajibu wetu kushirikiana kuwaumbua kila mahali mipango yao ya kiharamia lakini ni wajibu wetu pia kutumia mbinu mbadala na rasilimali mbadala za kukabiliana na hali hiyo. Rasilimali mbadala kwa kutumia nguvu ya umma ni pamoja na vijana wasomi kama nyinyi kujitolea utaalamu wenu, muda wenu, vipaji vyenu na nguvu yenu kuwezesha maandalizi, kampeni na ulinzi wa kura. Haya ni kati ya mambo ambayo ni muhimu mkayatafakari katika mkutano wa leo.Historia ya duniani inaonyesha kwamba mchango wa vijana na wanafunzi ni wa muhimu sana katika kuanguka kwa tawala za kidikteta, za kibaguzi na za kifisadi. Historia kama hii inapaswa kuandikwa nchini mwetu kwa njia za kidemokrasia kupitia uchaguzi ili kuleta mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli.Tuyafanye hayo tukitambua kwa pamoja kwamba mabadiliko ya kweli katika taifa letu hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale, wa chama kile kile, chenye uoza ule ule, wakiendeleza yale yale kwa Ari, Nguvu na Kasi (ANGUKA) zaidi. Kwa falsafa ya chukua chako mapema(ccm), ya chama cha mafisadi(ccm); Tanzania yenye neema haiwezekani. Tuunganishe nguvu kurudisha nchi kwa wananchi; Tanzania bila CCM inawezekana kupitia chama mbadala na uongozi bora.Natangaza kwamba mkutano huu umefunguliwa rasmi na tuko tayari kuwasikiliza; Vijana, Nguvu ya Mabadiliko.

Posted by John Mnyika at 1:48 PM 5 comments Links to this post

Tunu kwa kumbukumbu ya mashujaa

MAKALA IFUATAYO NILIIANDIKA MWAKA 2006, NIMEIREJEA WAKATI HUU KWA AJILI YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA TAREHE 25 JULAI 2010: Kamaradi Kinjeketile na mashujaa wenzako popote mlipo! Hii ni tunu kwenu. Hidaya kwenu mliomwaga damu wakati mapambano kadhaa na Mreno na Mwarabu. Tuzo kwenu nyinyi mliopigana na Ujerumani wakati wa utawala na mliomwaga damu katika vita vya dunia. Heko ninyi ambao damu ilisafisha safari ya kumng’oa Nduli Amin. Heri wewe Sethi Benjamini na wote waliopotesha maisha katika hekaheka za kueneza Azimio la Arusha. Kumbukumbu kwenu mliotoa damu katika mikikimikiki ya mfumo wa vyama vingi kutoka Zanzibar mpaka bara. Damu yenu iliyomwagika haizoleki, ukiwa mlioucha hauzoeleki lakini fikra mlizosimamia hazizeeki. Mapambano bado yanaendelea!Kwako Bushiri bin Salim wa Tanga, suriama wa kiarabu na kiafrika, pamoja na nia yako tenge ya kulinda maslahi katika biashara ya utumwa ulimwaga damu kwa kunyogwa Pangani baada ya kuongoza maasi makali dhidi ya kuingia kwa ukoloni wa Kijeruamani-damu yako ilimwagika pamoja na damu za wapiganaji wa Pwani, Morogoro mpaka uhehe. Ewe Mtemi Meli, uliowashinda wadachi mpaka mwenzio Sina alipokusaliti hatimaye wewe na mashujaa wenzako mkamwaga damu kaskazini mkilinda uhuru.Wewe Chifu Mkwawa, tunakukumbuka uliovyowaunganisha wahehe-toka Kalenga, Tosamaganga mpaka ulipoamua kuimwaga damu yako mwenyewe kuliko uhuru upotee mikononi mwako. Mtemi Isiki wa Tabora uliendesha mashambulizi ya kishujaa, hatimaye ukaamua kumwaga damu yako na ya familia yako kwa kujilipua na baruti ili tu usipate aibu ya uhuru kuchukuliwa mbele ya macho yako. Ewe Mtemi Makongoro wa Musoma, ulipambana kwa ushujaa mpaka ilibidi kikosi cha wanamaji kiletwe kupitia miji ya Mombasa na Kisumu kukumaliza.Nakutunuku Kinjeketile kwa kuongoza vita vya kutisha vya Maji Maji kwa miaka kadhaa vilivyoanzia vilima vya Matumbi karibu na Kilwa. Nyinyi mlitaka kumwondoa mkoloni kwa nguvu na mlikuwa tayari kumwaga damu kuliko kuendelea kuishi bila ya uhuru. Mapambano yenu yalisambaa maeneo mengi ya ardhi yetu. Ninyi mlikuwa mashujaa kweli kweli mliojua umuhimu wa imani na falsafa katika mapambano-mkawapa watu ujasiri kwa dawa ya “Kugeuza risasi, Kuwa maji”. Pamoja na kushindwa vita na wazalendo zaidi ya laki moja kupoteza maisha katika wakati ambao ardhi ilikuwa na watu wachache yapo mapigano ambayo mlishinda. Pamoja na machifu 47 wa Kingoni kunyongwa damu yenu ilileta mabadiliko katika utawala. Kwa vyovyote vile damu nyingi kiasi hiki iliyomwagika kwa sababu ya kudai uhuru haiwezi kupuuzwa. Hivyo waraka huu ni tunu kwenu. Mapambano bado yanaendelea!Nawaandikia waraka huu ninyi wahenga mashujaa muweze kurejea na kurekebisha historia. Najua mnaweza msirudi kimwili, lakini ni vyema kiroho mkandelea kuwa nasi. Fikra zenu za kimapambano hazipaswi kupotea. Kumbukumbu zenu za kishujaa hazistahili kufutika. Taifa lisilo na historia haliishi, linakufa. Kupotosha historia ya mashujaa ni kinyaa. Karibu kila eneo katika nchi yetu yupo shujaa ambaye anaweza kukumbukwa laiti kama historia zenu zingejulikana kizazi hata kizazi na kuwa chimbuko la kujiamini, kujithamini na uzalendo miongoni mwa Watanzania.Julai 25 ilikuwa siku nyingine ambapo tulifanya maadhimisho ya kinafiki ya siku ya mashujaa. Mtanishangaa kwa kutumia dhana kali- “UNAFIKI”. Namaanisha!. Ni dhana ambayo mnaifahamu na hamkuipenda. Ndio maana hamkutaka kuishi katika unafiki wa kukubaliana ama kutumiwa na watawala. Mkaamua kupambana! Mkamwaga damu mkiukimbia unafiki. Sasa tunawakumbuka! Lakini nasema tena, tunawakumbuka kwa kufanya maadhimisho ya kinafiki ya siku ya mashujaa. Ndani ya dhana ya unafiki kuna tabia nyingi, mojawapo ni kunena tofauti na matendo na kutenda tofauti na kauli. Na ndiyo tabia tunayoifanya wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa. Ndio maana nasema, tunafanya maadhimisho ya kinafiki.Labda ni waambie wakina Kinjeketile, nini tulifanya huku kama ishara ya kuuadhimisha ushujaa wenu. Siku chache zilizopita 25 Julai, tulijumuika chini ya Amiri Jeshi Mkuu, kwa sasa ni Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Yeye mwenyewe hakuwepo, alituma mwakilishi wake. Tulielezwa kwamba Rais yupo kwenye ziara ya kikazi Ujerumani!Usiku mmoja kabla tuliwasha mwenge wa uhuru pale Mnazi mmoja. Halafu asubuhi yake gwaride lilijipanga kuwapokea wageni wa Kitaifa. Zikatolewa salam za Rais na wimbo wa Taifa ukapigwa kwa heshima yenu. Kikundi cha Buruji kikapiga “last post” na gwaride likaweka silaha begani. Askari sita waliojipanga vyema wakapindua silaha zao chini na baadae mizinga ikapigwa kwa ajili yenu huku watu wote wakiwa kimya. Gwaride likafanya “present arms” na kikundi cha buruji kikapiga “reveilles”. Gwaride likateremsha silaha na kufungua miguu.Halafu silaha za asili ambazo nyingine nyinyi mashujaa mlizitumia zikawekwa kwenye mnara pamoja na maua. Baadhi ya silaha zilizowekwa ni pamoja na mkuki, ngao, sime, shoka, pinde na mishale. Hizi ni kumbukumbu sanifu za mapambano mliyoyafanya.Hatimaye zikafuata sala na swala kutoka kwa viongozi wa dini wakiwakilishwa na sheikh, mchungaji, padri na maraji wa wahindu. Ingawaje sikumwona kiongozi wa dini ya jadi-ambao najua baadhi yenu nyinyi mashujaa na wahenga mliwaamini. Pengine dini za jadi zilitoweka na damu zenu. Gwaride likatoa tena heshima na wimbo wa taifa kupigwa ukafuatiwa na itifaki za viongozi wa kitaifa kuondoka. Wakabaki polisi kuzilinda silaha za kumbukumbu ya mashujaa mpaka jioni na hatimaye mwenge wa uhuru ukazimwa kama ishara ya mwisho wa maadhimisho ya kumbukumbu yenu ninyi mashujaa. Niwaulize wakina Kinjeketile, haya siyo maadhimisho ya kinafiki ya mashujaa? Pengine mtanijibu hapana!.Ngoja niwaeleze masuala kadhaa halafu niwaulize tena. Siku hizi kuna kitu kinaitwa Bunge, hiki ni chombo cha juu chenye uwakilishi wa wananchi ambacho kunafanya maamuzi mbalimbali ambayo mengine huwa sheria. Chombo hiki ni kama yale mabaraza ya jadi yaliyokuwepo wakati wenu. Wiki iliyopita bunge lilijadili kuhusu maadhimisho ya vita vya Maji Maji ambavyo nyinyi wakina Kinjeketile mliviongoza. Miaka mia moja imepita toka damu yenu azizi ilipomwagika katika mapambano hayo ya kumwondoa mkoloni.Ungekuwepo najua ungekuwa Mbunge wa Kilwa, ungeshangaa sana-Eti maadhimisho ya vita mlivyovianza Kilwa na mapambano ya mwisho yakawa Songea, yanafanyika kinyume chake! Maadhimisho yameanzia Songea na waziri ameahidi pengine yataishia Kilwa. Chacha Wangwe, mbunge wa CHADEMA (wakati wenu hakukuwa na vyama vya siasa vyenye majina haya) jimbo la Tarime, yeye akahoji-kwanini bendera ya taifa isiwekwe rangi nyekundu kama ishara ya kuwakumbuka nyinyi mashujaa wetu? Naibu waziri wa habari na michezo, Mheshimiwa Emanuel Nchimbi-yeye akajibu, hakukuwa na sababu ya rangi nyekundu kuwekwa kwenye bendera ya Taifa kama ishara ya kuwakumbuka mashujaa. Eti, historia ya uhuru wa nchi yetu inaamuliwa kuanzia mkoloni wa mwisho aliyetutawala ambaye ni Muingereza. Sasa kwa kuwa tulipata uhuru wetu kwa amani bila kumwaga damu chini ya uongozi wa mwalimu Nyerere basi hakukuwa na sababu ya kuweka rangi nyekundu. Enyi mashujaa Kinjeketile na wenzako tunaowakumbuka leo mnakubaliana na jibu hili?Ndio maana nikasema ni maadhimisho ya kinafiki. Tunanena tofauti na matendo. Nimesema awali, tunaanza maadhimisho ya leo kwa kuwasha mwenge wa uhuru halafu baadae tunaweka silaha za jadi. Kinjeketile na wenzako, iulizeni serikali- kama uhuru wetu tuliupata kwa amani, iulizeni serikali kwanini tunawasha mwenge wa uhuru na baadaye kuweka silaha za jadi? Tunanena tofauti na tunavyotenda? Iulizeni serikali, je harakati za mwisho za uhuru ni kipimo pekee cha historia ya nchi na hivyo kuwa kigezo pekee cha kuamua alama za nchi ikiwemo bendera?Enyi mashujaa mlioambana kuulinda uhuru wetu dhidi ya wakoloni kuingia kuanzia wakati wa Mreno, Mwarabu na Mjerumani na kumwaga damu, mnakubaliana na majibu haya? Kushindwa kwenu na hatimaye ukoloni kuingia hakuondoi historia kuwa mlimwaga damu kwa ajili ya kulinda uhuru wa ardhi hii tukiyoirithi!Enyi mashujaa mliopambana kuondoa ukoloni hususani ule wa Ujerumani mkamwaga damu, mnakubaliana na kumbukumbu hii? Kwamba mliyoyafanya si historia kuu kama historia ya uhuru toka kwa Mwingereza?Enyi mashujaa, waulizeni wataalamu wa historia-baada ya Ujerumani kushindwa na makoloni yake yote kuwekwa chini ya halmashauri ya mataifa na baadaye baraza la udhamini, Tanganyika ikiwekwa chini ya uangalizi wa Uingereza-si kwamba tulikuwa katika hatua za mwisho kabisa za kupewa uhuru ambao tayari tulishaupata kwa damu? Waulizeni pia, hakuna damu yoyote iliyomwagika wakati wa Mwingereza? Je, historia ya nchi yetu iliyojikita katika kipenzi chetu Nyerere imewajumuisha mashujaa wote wa ardhi hii?Nasema kwa damu-kuanzia ushindi pamoja na kushindwa dhidi Mjerumani ambao ulileta mabadiliko katika mfumo wa utawala sanjari na mashujaa ambao walikuwa mstari wa mbele katika jeshi la Mwingereza na washirika wake katika vita dhidi ya Mjerumani, vile vita vya dunia ambavyo vilipiganwa pia katika ardhi yetu? Wakina nani walimwaga damu zaidi katika kile kinachoitwa ukombozi ulioletwa na majeshi ya mfalme Afrika (KAR) kama si nyinyi babu zetu?Hojini serikali, hivi bendera hii ni ya Tanganyika au Tanzania? Jibu la Nchimbi limetolewa katika muktadha wa historia ya Tanganyika, Ingekuwa vipi jibu lingetolewa mintaarafu bendera ya Tanzania ambayo ilipatikana kutokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilihali visiwani kuna historia ya damu kumwagika ama kumwagwa wakati wa mapinduzi? Kama kweli tuna serikali ya mapinduzi Zanzibar na utawala wa Chama cha Mapinduzi(CCM), je ni mapinduzi yasiyo na ‘rangi nyekundu’?Tunatenda tofauti na kauli! Tunafanya maadhimisho ya kinafiki. Wakina Kinjeketile tunawakumbuka kwa kuwa mlimwaga damu kupinga ukoloni na unyanyasaji. Mtuulize wajukuu zenu, je tunawaadhisha kwa kuendelea kupiga vita yale mliyoyakataa? Kwa hali ilivyo, wapo wanaotenda yale mliyoyakataa pamoja na kuwa wote kwa kauli tunawaenzi ninyi mashujaa. Tunapaswa sasa kuweka fikra zenu katika vitendo kwa ajili ya ukombozi wa taifa letu. Mwalimu Nyerere alikumbuka fikra zenu akatamka na kutenda kwamba uhuru, si uhuru wa maneno. Ni uhuru dhidi ya ujinga, uhuru dhidi ya maradhi, uhuru dhidi ya umaskini na baadaye akaongezea uhuru dhidi ya rushwa ama ufisadi. Enyi wahenga mashujaa, shukeni katika nyoyo za watoto na wajuu zenu, mtufanye kutokana na maadhimisho ya mwaka huu tuweke dhamira ya kupigana vita kwa zana kisasa kuleta mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli, kuleta haki na maisha bora. Hii ndiyo hidaya kwa damu yenu azizi. Sio siri, kwa sera bila silaha, mapambano bado yanaendelea!Chanzo: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=40

Posted by John Mnyika at 8:02 AM 0 comments Links to this post

Saturday, July 17, 2010

RIP: Profesa Mwaikusa, Gwamaka na Mtui

Unahitajika mkakati wa pekee kukabiliana na ujambazi maeneo ya pembezoni mwa DSM kama Salasala, Mpiji Magoe, Goba, Temboni, Kwembe, Saranga nk. Wananchi wanalipa kodi wakitarajia kwamba moja ya jukumu kuu la serikali na vyombo vyake ni kulinda usalama wa maisha yao na mali zao. RIP: Profesa Mwaikusa, Gwamaka na Mtui.

Posted by John Mnyika at 9:21 AM 0 comments Links to this post

Tuesday, July 13, 2010

Hongera Kinondoni kwa kushinda Copa Coca Cola U 17

Nawapongeza timu ya vijana(U 17) wa Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni kwa kuwa mabingwa wa Copa Coca Cola tarehe 10 Julai 2010.Mashindano kama haya ya vijana na watoto na yale ya mashuleni kama umishumta na umiseta ni ya muhimu sana katika kujenga oganizesheni ya soka na kuunda timu bora za baadae(dream team).Ni muhimu sana tukayapa mkazo na kuwekeza pia katika mafunzo na viwanja kuanzia ngazi ya chini kabisa mitaani na kwenye wilaya.

John Mnyika-Mwenyekiti Mkoa wa Kichama wa Kinondoni (CHADEMA)

Posted by John Mnyika at 8:56 AM 0 comments Links to this post

Tuesday, June 29, 2010

Mnyika ataka Londa, Kandoro na Makamba wahojiwe ufisadi wa ardhi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, wanastahili kuhojiwa katika kashfa ya uuzwaji viwanja vya wazi katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Viongozi hao katika chama tawala na serikali, wanadaiwa kuhusika katika kashfa hiyo walipokuwa Wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa nyakati tofauti.Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, Makamba anatajwa kama Katibu Mkuu wa CCM na pia anatajwa kwa nafasi yake alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.Chadema inataka viongozi hao wahojiwe kwa vile wanatajwa kwenye taarifa ya kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya CCM wilayani Kinondoni.Alisema taarifa hiyo ya siri ya Machi 15, mwaka juzi, ilihusu mgogoro wa madiwani wa manispaa ya Kinondoni dhidi ya Meya wake, Salum Londa, mpasuko miongoni mwa madiwani, ubadhirifu wa fedha, mali ya manispaa na uongozi mbovu katika manispaa hiyo.Mnyika alisema Kandoro, ambaye ndiye aliyemrithi Makamba kwa nafasi hiyo mkoani humo, anatakiwa ahojiwe kwa vile naye anatajwa katika taarifa hiyo.Mbali na Makamba na Kandoro, Chadema pia inataka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, awaeleze Watanzania alikuwa anafahamu nini kuhusu kashfa hiyo, ambayo inawataja kwa majina Londa na madiwani wengine wa manispaa ya Kinondoni kwenye tuhuma za rushwa na uuzaji wa viwanja.Katika taarifa hiyo, Londa anatuhumiwa kupokea rushwa ya Sh. milioni 20, na kwa sababu hiyo Chadema, inataka asiishie kuhojiwa tu, bali akamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.Kwa mujibu wa Mnyika, Chadema inataka viongozi hao wahojiwe na Polisi pamoja na kamati iliyoundwa na Lukuvi hivi karibuni.Kamati hiyo iliundwa kwa lengo la kupitia maeneo yote ya wazi ya jiji la Dar es Salaam, kuyabaini na kuainisha kama yalivyo katika ramani kuu (master plan).Hatua hiyo ingefanikisha kufahamu orodha kamili ya maeneo hayo, yalipo, yamepangiwa shughuli gani na wamiliki ni akina nani na utaratibu gani ulitumika kuyagawa.Mnyika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chadema, alisema wanataka viongozi hao wahojiwe na wengine kukamatwa ili kujiridhisha kwamba, dhamira ya kuundwa kwa kamati hiyo si mchakato wa kisiasa wa kuelekea Uchaguzi Mkuu.Alisema siasa hizo zinaweza kutumiwa kupitia kero zinazowakabili wananchi kwa muda mrefu na mbazo serikali ya awamu ya nne haijazishughulikia tangu iingie madarakani.“Sasa kama kweli wana dhamira ya dhati ya kuchukua hatua, tunataka polisi na kamati husika wamhoji Makamba kwa sababu anatajwa humu (kwenye taarifa ya CCM) siku zote, anatajwa kama Katibu Mkuu wa CCM, anatajwa kama kwa nafasi yake alipokuwa Mkuu wa Mkoa,” Mnyika alisema.Aliongeza: “Wamhoji Kandoro, kwa sababu anatajwa humu. Na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa sasa hivi, Lukuvi, ambaye ndiye ameunda kamati, na yeye awaeleze Watanzania alikuwa anafahamu nini kuhusu hii taarifa ya mwaka 2008.”Taarifa hiyo ya CCM ni ile inayowataja kwa majina Londa na madiwani wengine kwenye tuhuma za rushwa za uuzaji wa viwanja.Wakati Chadema ikishinikiza hivyo, sakata hilo linaonekana `kumchanganya akili’ Meya Londa, ambaye hivi sasa anahaha kumsaka mchawi.Meya Londa aliitisha kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni jana, katika kile kilichoelezwa kuwa ni kuwatafuta madiwani wanaohusika katika uvujishwaji wa taarifa zinazohusu kadhia hiyo.Kwa mujibu wa habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa baraza hilo, Meya Londa anadaiwa kukanusha tuhuma zinazomkabili.Londa na madiwani wengine watano wa manispaa hiyo, walikwisha kuhojiwa na polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam juu ya tuhuma za uuzaji wa viwanja.Mmoja wa madiwani waliohudhuria kikao cha jana, alieleza kuwa ajenda iliyotawala kikao hicho ilihusu masuala ya uuzaji wa viwanja vya wazi.Hata hivyo, madiwani wengine walipoulizwa kikao hicho kilikuwa kinahusu nini, walisema kilikuwa kililenga masuala ya kisiasa yanayokihusu CCM.Kwa upande mwingine jana maofisa mbalimbali wa serikali walikutana katika manispaa hiyo kwa ajili ya kikao maalumu cha kuendelea kufanya uchunguzi wa kashfa ya uuza viwanja kinyume cha sheria na taratibu.Kikao hicho kilifanyika ukumbi wa jirani na walipokuwa wamekaa madiwani hao, ambapo pande zote hazikuruhusu waandishi wa habari kuhudhuria.Alipoulizwa na waandishi wa habari, Londa alithibitisha kufanyika kikao hicho cha madiwani, lakini akasema ajenda kuu ilikuwa ni kuzungumzia masuala ya Chama cha Kuweka na Kukopa (Saccos) ilichoanzishwa na madiwani hao.“Unajua sisi tuna Saccos yetu hapa kama madiwani na kwa kuwa tunamalizia muda wetu, lazima tuchukue fedha kwa ajili ya kwenda kufanyia kampeni,” alisema.Meya huyo alionekana kutotaka kujibu maswali zaidi kutoka kwa waandishi wa habari waliofika ofisini kwake, ili kupata ufafanuzi kuhusu kikao alichoitisha.Awali, Mnyika alisema wanatilia shaka utendaji wa kamati hiyo inayoanza kazi yake leo kwa sababu mbalimbali, ikiwamo muundo wake na uadilifu wa mwenyekiti anayeiongoza, Albina Burra.Alisema Burra, ambaye ni Mkurugenzi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kurugenzi anayoiongoza wizarani hapo mwaka 2007, 2008 na 2009, imekuwa ikituhumiwa kwa ufisadi katika mgogoro wa ardhi eneo la Luguruni-Kibamba, katika manispaa hiyo. Burra ni Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji katika Wizara hiyo.Kutokana na hali hiyo, alisema ili shaka iondoke, wanataka kamati hiyo ifanye kazi kwa uwazi, ikiwa ni pamoja na kuviruhusu vyombo vya habari na wadau wengine kufuatilia majadiliano ya kamati, Lukuvi aeleze mamlaka na mipaka ya kazi ya kamati, itakamilisha lini kazi yake na ripoti yake iwekwe hadharani.Aliwataka wananchi popote walipo kujitokeza kutoa ushahidi kwa kamati na kusema watakaohofia usalama wao, wawasiliane na Chadema kwa namba ya simu 0784222222 na barua pepe: kinondoni@chadema.or.tz This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it ili wakawawakilishe.Pia, alimtaka Lukuvi kuielekeza kamati ili katika kufanya kazi yake leo, izingatie kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa hadharani mwaka huu, alipotembelea Manispaa Kinondoni kwamba anawajua kwa majina madiwani waliouza viwanja vya umma na kuwataka waache jambo hilo, la sivyo atawataja.Alipoulizwa na Nipashe jana, Makamba alisema hapaswi kuhojiwa, bali anastahili kuulizwa ili aeleze ukweli wa mambo kuhusu mambo yote ya Jiji la Dar es Salaam.Alisema ameongoza Dar es Salaam kwa takriban miaka 10, hivyo anajua mambo mengi yanayohusu sekta mbalimbali, ikiwamo ardhi.“Anayehojiwa ni mhalifu, mimi sihojiwi. Londa ndiye anayepaswa kuhojiwa kwa sababu ndiye mwenye matatizo. Mimi niulizwe, nieleze ukweli wa mambo.Mwingine anayestahili kuulizwa ni Kapteni (John) Chiligati (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) yeye anahusika na ardhi,” alisema Makamba.Kwa upande wake, Kandoro alisema uamuzi wa kuhojiwa au la, uko mikononi mwa Kamati ya Lukuvi, hivyo ushauri uliotolewa na Chadema juu yake, haoni kuwa ni tatizo.“Kwani tatizo liko wapi? Chadema wametoa maoni yao. Sasa wenye kamati wataamua wanihoji ama vipi,” alisema Kandoro.Jumatano wiki iliyopita, Lukuvi alimfukuza kazi Ofisa Ardhi wa Manispaa hiyo, Magesa Magesa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi, akidaiwa kuidhinisha ujenzi katika kitalu namba 1274 na 1275 eneo la Msasani, Peninsula kwa Kampuni ya Tanzania Building Works. Tayari Magesa amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.