Monday, August 23, 2010

Hongereni Wana-Upinzani Tz, mtakumbukwa kama Mashujaa wa Taifa hili.....


Ni nani asiyejua kuwa wapinzani wanatumia muda, rasilimali na jasho lao kwa kipindi kikubwa sana ili kuikomboa nchi yetu kutoka katika madudu ya wasioipendea mema nchi na wananchi wake bali waliotayari kujineemesha wao na familia zao?



Tuchukue mfano mrahisi, wakati mimi na wewe tukienda kazini kwa ajili ya familia zetu na maisha yetu binafsi, kuna wakina Freeman Mbowe, Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe, na wengine weeeengi ambao wanatumia muda wao mwingi kuzunguka huku na huko kuwaamsha watanzania wengi waliolala waone jinsi gani wanadhulumiwa haki zao.



Cha kushangaza, hatuwaungi mkono watu hawa, inafika kipindi watu hawa wanaingia mifukoni kutoa chochote kwa ajili ya mpambano huu. Badala yake wengi wetu tunawakejeli na kuona ni haki yao na ni wajibu wao kufanya hivi!



Hii ni aibu kabisa! Itakuwaje wao nao wakaamua kutundika daluga na kuamua vision zao ziwe kwenye familia na maslahi yao binafsi? What if wakiamua upinzani sasa basi, kama ndo imekuwa hivi basi acha iwe kila mmoja afe na lake? Unafikiri katika miaka kumi kutakuwa na Tanzania tena?Mmeliona hili?

What if na wenyewe wangeamua: Sasa basi, acha na wao wakubali fulana za kijani na njano na wapokee hizo takrima za chini chini washabiki wa ccm wanazopewa kwa sasa?



Cha ajabu sana, watanzania wanasahau mapema kweli kweli. Juzi tu hapa, wapinzani hawa tunaowakejeli leo wamefanya kazi nzuri sana bungeni hatimaye tukaona kilichokuwapo EPA na RichMond, leo hii watanzania wanajidai wamesahau. TUCTA nao watu wa ajabu sana, juzi walikuwa na mwelekeo huu, leo out of blue wanamwelekeo wa kiaina fulani. Media na yenyewe, juzi juzi ilikuwa na uzalendo, leo hii naona wameanza kuwa na mwelekeo wa U-CCM.



Ninajiuliza, unafikiri tunawakomoa wapinzani? Unafikiri ni wajibu wa wapinzani kumwagika jasho ili nchii hii iwe ya neema hapo baadaye?



Wangapi leo hii mnashabikia tu sera ya kilimo kwanza na ongezeko la bajeti ya kilimo wakati ki-uhalisia ukichambua hicho kitu hakipo? (Dr Slaa aliwachambulia vizuri - mchango mwingine wa upinzani makini kwa hatima ya nchi hii)



Kama watanzania wanafikiri ni muda wa kuwakomoa wapinzani, basi wajiaandae na maumivu zaidi.

CCM ni wataalamu wa kuuma na kupuliza, leo wanapuliza, ngoja uchaguzi upite tuwaone!

Leo hii fedha ya Tanzania inashuka thamani kila kukicha, kwenye mzunguko wa fedha leo hii, Tsh. elfu kumi na Elfu tano (noti kubwa) zimekuwa za kawaida kuwepo kwenye mzunguko wa kawaida kabisa wa maisha hata yale ya kawaida sana. Ndio maana hadi kesho, watanzania mishahara haitatosha na gharama za maisha zitazidi kwenda juu kila kukicha.



Wizi wizi wa mali za umma, na ubadhirifu utazidi kuongezeka, tusitegemee mapya kutoka kwa CCM.

na sitashangaa sana, ifikapo mwaka kesho katikati, watu wataanza kulalamika tena kuwa serikali ni mbovu ilhali katika uchaguzi walikubali kurubuniwa.



Angalia wasanii majuukwaani wanavyoimba kinafiki? Mimi sina jingine zaidi ya kusikitika. Ni lini watu hawa wooote watafunguka macho na kuona magumu na mazito yanayoikabili nchi yetu chini ya CCM?Akili ipo kichwani mwako, fanya maamuzi sahihi mwananchi

No comments:

Post a Comment