Monday, August 16, 2010

Kwanini Dar siyo ngome kuu ya upinzani?


Karibu nchi zote duniani ambazo zimekuwa na mwamko wa kisiasa na upinzani uliokomaa zimefanya hivyo baada ya kuteka mji wake wake mkuu au mji mashuhuri. Ni katika miji mikubwa ya nchi ndipo upinzani umeonekana kukomaa



Zambia - Lusaka

Kenya - Nairobi

Irani - Tehran

Thailand - Bangkok

Ukraine - Kiev

Uingereza - London





n.k



Lakini kwa Tanzania, Dar-es-Salaam jiji kubwa zaidi, lenye watu wengi zaidi na lenye kufikiwa na vyombo vya habari vingi zaidi siyo ngome ya upinzani Tanzania. Zaidi ya watu kujitokeza kushangilia na kuonesha kukerwa na serikali ya chama tawala mara kwa mara ni hao hao watu wa Dar ndio wanaipa nguvu CCM na sitoshangaa (natumaini isiwe) upinzani unaweza usinyakue mbunge tena Dar.



Ni kitu gani kinafanya Da isiwe ngome ya upinzani? Kwa mfano kushindwa kuchukua halmashauri hata moja, kushindwa kutoa mameya, madiwani wengi wakiwa bado ni CCM na wabunge bado ni CCM licha ya madudu yote. Na hasa ukizingatia kuwa Dar ndiyo yaweza kudaiwa kuwa ina wasomi wengi zaidi!!!!



Yawezekana lawama ziiangukie CCM au pongezi kwa kuweza kuchakachua nguvu za upinzani Dar? Kwa sababu hata kwenye kura za maoni utaona wana CCM Dar wanaonekana kuchangamka zaidi kuliko wale wa upinzani. Au mimi siangalii vitu kwa usahihi maana hata CUF haina nguvu Dar mahali ambapo tungetarajia kuwa na nguvu ya aina fulani.

No comments:

Post a Comment