Nani kama Dr. Slaa???


Na tuweni wakweli? Katika wagombea URAIS bila kuangalia chama..ukiambiwa pigia kura "UADILIFU, HAKI na UZALENDO nani anastahili??? Jibu lako nani apewe uongozi wa nchi???



Mtanzania yeyote Mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu, asiye na
mtindio wa ubongo, wala mtumwa wa hila chafu, wala udumavu wa kiakili,
tena asiye na utando wa buibui wala tongotongo za ufisadi machoni,
wala asiye mzembe wa kufikiri, anaalikwa asome kwa uangalifu na
azingatie makala hii na awashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zake
popote pale walipo..



Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere
kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini
wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya
wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani.

Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.



Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge
kupungzwa
kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila
woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa
amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga
kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?

Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili
ajibu bila unafiki!



Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr
Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana
na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao
Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa
mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa
ni nini?



Ni Dr. Slaa anayeongelea treni ya umeme kwenda Kigoma, Dodoma , Tabora,
na Mwanza. Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta
mabehewa ambayo mababu
zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi
wanabaki kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa
vinatumika kujenga vyoo. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na
akina Carl Peters.



Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni
sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo
lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata
moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini,
wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado!

Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na
vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni
sehemu ya maisha yao . Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..



Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu
ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na
Tanzanite. CCM
wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na
wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya
shilingi 350.000 achana na CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili
ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji
yao .



Ni Dr.Slaa anayeweza kusimamia mashirika ya umma kuleta tija achana na
CCM wanaofyonza michango yetu kule, kwani haya mashirika yameshindwa
nini kuwajengea nyumba wanachama wake? Mbona kwingine yameweza? Ni
Dr.Slaa anayeweza kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa
sheria bila kuwaonea watu wala bila kulipiza visasi.



Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya
walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba
anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa
sheria uko wapi? Naomba niwape heko ITV kwa kuturejeshe kwenye hotuba
za mwalimu. Katika hotuba yake moja
alisema waziri mmoja kule
uingereza aliandikwa kidogo tu gazetini juu ya kashfa, yule waziri
alijiuzulu na waziri mkuu hata hakumjibu bali aliteua mtu mwingine.



CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule
wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake.

Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili
imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara
kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!



Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Si tumeona mnazi mmoja alivyowataja
mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia
nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto
utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata
madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekaa
chini? we must be serious! Hivi kweli dunia ya leo watu wanavuliwa
nguo njiani kwenda Mwanza,
Shinyanaga, Tabora, Kigoma, Mbeya, Lindi na
Mtwara kwa sababu ya usafiri wa malori?



Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya
maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa
kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya
umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima
wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao ? Nani asiejua asilimia 85 ya
watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua
tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu??



Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi?

Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni
akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini
wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?



Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa,
anaweza
kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa
kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito , maziwa, national
parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini tuko
maskini wa kutupwa! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania.



Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi
kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa
nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika
kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu
haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi
wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache
woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona
zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi,
inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.



Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi
wote na atuwekee katiba sawa. Huo
ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi.

CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio
waendelee kututawala na kutunyonya.



Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni
kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu
nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote
zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi. Peleke ujumbe
huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako
wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Peleka ujumbe huu
haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa
waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..