Friday, October 29, 2010

CCM WANATISHIA AMANI

Friday, October 29, 2010

MIJADALA MBALIMBALI

GONGA LINKI KWA HABARI ZAIDI

MBINU ZA VITUO HEWA VYA KUPIGA KURA WAGUNDULIKA KWENYE BAADHI YA MAJIMBO
WANANCHI WENZANGU, SAFARI HII TUSIDANGANYIKE!
Kura zimeshaibwa, Kikwete 80% ameshinda!
Mbinu chafu za CCM jimbo la Ubungo

FFU WAKIMBIZA WAFUASI WA CHADEMA IRINGA ,DK SLAA AKWAMA KUHUTUBIA

"
Hapa tupo gado akitua tu Dk Slaa tunaye"
"
Ila hawa wananchi mbona ni wengi sana itakuwaje hawawezi kufanya fujo"
"
Jamaa hakuna kulala hadi kieleweke twendeni uwanja mwingine kama huu hapa wamezuia"
"
Mzee salama hapa ama ?kwani kuna nini ni vita ?"
"
Hapa tupo kamili kwa lolote "kama wanazungumza

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoa wa Iringa wakiwa wamejipanga kwa lolote katika viwanja vya uwanja wa shule ya msingi Mlandege mjini Iringa ambako ulipangwa mkutano wa mwisho wa mgombea urais wa Chadema Dk Willibrod Slaa ambaye hata hivyo hakuweza kutua katika uwanja huo kama njia ya kukepa mbinu za CCM kutaka kuvuruga mkutano wake huo iwapo angetua katika uwanja huo leo asubuhi
Wanafunzi wa shule ya msingi Mlandege mjini Iringa wakiwa wamejifungia ndani ya vyumba vyao vya madarasa kuhofu usalama wao baada ya polisi wa FFU kutanda kuzunguka majengo ya shule hiyo ambayo yapo jirani na uwanja wa mkutano uliokuwa ukifanywa na mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa baada ya mgombea urais Dk Willibrod Slaa kushindwa kutua kuhofu fujo kati yake ya polisi hao ambao walikuwa wakipinga mkutano huo kuhutubiwa na mgombea urais
Polisi wa FFU wakilinda eneo la mkutano ambao lilipaswa kuhutubiwa na mgombea urais wa Chadema Dk Slaa ambaye hata hivyo ameshindwa kuhutubia katika viwanja hivyo vya Mlandege
Wanafunzi wa shule ya msingi Mlandege wakichungulia madirishani baada ya walimu wao kukimbia madarasani kuhofu mabomu muda mfupi baada ya FFU kutua eneo hilo na kuwataka wananchi kutawanyika kabla ya viongozi wa Chadema kujitoa mhanga na kuangua kilio cha kuomba msahama mbele ya askari hao
Hapa uwanja wa Mwembetogwa Iringa ambako ilipaswa Dk Slaa kufanya mkutano wake wa kampeni leo asubuhi japo imeshindikana
Askari wa FFU mjini Iringa wakiwa wamepiga kambi katika uwanja wa Mwembetogwa kuzuia mgombea urais wa Chadema Dk Slaa kufanya mkutano eneo hilo ,kulia ni mwananchi akijikaza kupita kiume eneo hilo ambalo wananchi walitawanywa .




Na Francis Godwin,Iringa

NGOMA nzito Iringa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa amegonga mwamba kutaka kufanya mkutano wa kampeni bila kibali katika viwanja viwili tofauti mjini Iringa, baada ya Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) kutanda katika viwanja vyote kuzuia mikutano hiyo kwa madai kwamba haina baraka za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.



Polisi waliokuwa na silaha kali na mabomu ya kutoa machozi, walifanikiwa kuwatawanya maelfu ya wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakiendelea kukusanyika kwa wingi katika uwanja wa Mwembtogwa mjini hapa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi.

Baada ya kutawanywa, wananchi hao walielekea katika uwanja wa Shule ya Msingi Mlandege walikotangaziwa kwamba Dk Slaa angetumia jukwaa la mgombea udiwani wa kata ya Kwakilosa, kuwasalimia wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kabla hajaendelea na ziara yake ya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Njombe Kaskazini, Njombe Magharibi na Songea Mjini.

Thursday, October 28, 2010

Namuunga Mkono DR Slaa Asema Prof Lipumba wa CUF

Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF amesema anamuunga mkono
yule wa CHADEMA DR W P SLAA , Kwahiyo amewasihi wananchi wampigie kura dr
slaa kama wasipompa yeye ila kasema yeye ni kama Mlima wakati DR SLAA ni
Kichuguu ameyasema hayo katika Mdahalo maalumu unaorushwa na ITV Moja kwa
moja sasa hivi

Gonga hapa kufuatilia Mjadala Huu
Namuunga Mkono DR Slaa Asema Prof Lipumba wa CUF

Kituo Bandia cha Kupiga Kura Chagundulika Shinyanga

Kuna jamaa yangu ameniambia kwamba kuna taarifa za kugundulika kituo Bandia
( Feki ) Cha kupiga kura , Anasema wananchi wa maeneo hayo walikuta majina
yao yameandikwa mara 2 moja kwenye eneo lao na kopy ya pili kwenye eneo
lingine na kubandikwa ambako hakuna kutuo lakini majina yao yalibandikwa
hapo .

Hizi ni tetesi tu sijadhibitisha lakini watu wawe makini kwa kuangalia
vizuri vituo na majina yao

Thursday, October 28, 2010

AHADI ZA WAGOMBEA


 Kuelekea Uchaguzi Jumapili:.List ya Ahadi za Dkt. JK vs Dr. Slaa

Ahadi za Dkt. JK:
  1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  2. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) na NYANZA- Shinyanga na Mwanza
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu- Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  44. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  45. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  46. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  47. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  48. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  49. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  50. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  51. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  52. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  53. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  54. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  55. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  56. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  57. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
  58. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  59. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  60. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  61. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  62. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada TanzaniaRuvuma
  63. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  64. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  65. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  66. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  67. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
  68. Kuwapokonya eneo TanzaniteOne baada ya 2012
  69. Kujenga Maabara kubwa na ya kisasa kuliko zote dunia -Tanga


Ahadi za Dk Slaa:
1. Kujenga nchi isiyo na ufisadi
2. Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
3. Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
4. Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
5. Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
6. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
7. Kutoa huduma bora za afya na elimu bure
8. kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
9. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
10. Kubana matuzi Ikulu (Yuko tayari kula mihogo)
11. Kupunguza idadi ya baraza la mawaziri hadi 15
12. Mawaziri kuteuliwa nje ya Bunge

Tumia AKILI yako kupima mgombea anayekufaa na TUMIA haki yako kumchagua


CHADEMA YAWASHIKA ARUSHA

Thursday, October 28, 2010

Tusikubali miaka mitano mingine ipotee

Evarist Chahali

MWAKA 2005 nilikuwa miongoni mwa waliokuwa na shaka juu ya uteuzi wa Jakaya Kikwete kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lakini baada ya ushindi wake wa kishindo, nilianza kuwa na imani naye, hasa kutokana na kauli zake za kuleta matumaini mapya.

Baada ya miaka 20 ya tawala za Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, nchi yetu ilihitaji mtu mwingine mwenye kuelewa kwa nini inazidi kuwa masikini wa kutupwa licha ya utajiri lukuki, mtu mwenye dhamira ya dhati ya kupambana na rushwa kwa vitendo, si maneno matupu (kwa mfano kutangaza kuwa anawafahamu wala rushwa ila anawapa muda wa kijirekebisha).

Awali, sikuamini kuwa Kikwete angeweza kuipatia Tanzania kiongozi wanayemuhitaji kwa vile hukuwa na rekodi hiyo. Licha ya kwamba urais si taaluma inayosomewa, lakini uongozi bora unaweza kubashiriwa kutokana na rekodi ya nyuma ya kiongozi mtarajiwa hasa kwa vile kabla ya kuwa rais wetu, Kikwete alikwisha kushika nyadhifa kadhaa lakini pasipo rekodi ya kujivunia.

Hofu yangu kuhusu Kikwete ilianza kuyeyuka baada ya kusikia kauli yake wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania ingekuwa kipaumbele chake kikuu pindi akichaguliwa, sambamba na kibwagizo cha Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya.

Hotuba yake wakati anazindua Bunge, Dodoma, ilileta msisimko mpya, matumaini na imani kwamba hatimaye sasa tumepata kiongozi wa kuifikisha Tanzania inakopaswa kuelekea. Na hata alipotangaza baraza kubwa la mawaziri (lililojumuisha sura zenye utata), nado niliendelea kuwa na matumaini naye na kukubaliana na utetezi wake kwamba ili afanikiwe kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania angehitaji timu kubwa.

Matumaini yangu yalianza kufifia pale ulipotoa hotuba na kutamka kwamba “nawafahamu wala rushwa kwa majina lakini nawapa muda wa kujirekebisha”. Nilivunjwa moyo na kauli hiyo kwa sababu sijawahi kusikia mahala ambako rushwa ilikoma baada ya kiongozi kutoa muda kwa wala rushwa kujirekebisha. Na labda hapa niulize, hivi ile deadline aliyotoa mwaka 2006 kwa wala rushwa (aliodai kuwafahamu kwa majina) kujirekebisha bado haijaisha? Au ilikuwa indefinite deadline (isiyo na ukomo)?

Baadaye alirejea kauli kama hiyo alipofanya ziara ya ghafla Bandari ya Dar es Salaam alikotamka bayana kwamba anawafahamu wala rushwa katika sehemu hiyo na kilichobaki ni kuwaumbua tu (nadhani alimaanisha kilichobaki ni kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria). Inasikitisha kuona hadi leo hakuna aliyewajibishwa huku mamlaka husika zikirejesha mpira huo kwake kwa maelezo ya “waulizeni Ikulu maana wao ndio walidai wana orodha ya wala rushwa hapa”.

Tuwe wakweli, hivi kama aliahidi kuwasilisha majina ya mafisadi wa bandarini lakini hajatimiza ahadi hiyo maana yake ni nini? Je, tunastahili kuendelea naye kama ahadi alizotoa ni zisizotekelezwa? Kama anashindwa kutekeleza ahadi anazotoa mwenyewe pasipo kulazamishwa ataweza vipi kutekeleza mambo muhimu ambayo japo hajaahidi ni lazima ayatekeleze?

Ni kweli kwamba kiongozi wa nchi lazima afanye safari za kujitambulisha nje, lakini hicho hakiwezi kuwa ndiyo kipaumbele kwa kiongozi mwenye dhamira ya dhati ya kurekebisha hali ya nchi masikini kama yetu. Hata Barack Obama na David Cameron, viongozi wa mataifa tajiri kabisa duniani, wametuthibitishia kwamba kwenda nje ya nchi kujitambulisha si kipaumbele kwa kiongozi mpya.

Lakini pengine eneo tata zaidi ni la mafisadi. Kusita kupambana na kundi hili kumezua tafsiri nyingi katika vichwa vya watu, nyingi za hizo, hazimsemi vizuri Rais Kikwete kwa vile imejikita imani kwamba kuwaacha mafisadi waendelee ndiko kulikokwamisha “Maisha Bora kwa Kila Mtanzania”.

Ni siri ya wazi kuwa aliingia madarakani kwa nguvu na jitihada za wanamtandao, wengi wao wakiwa watu wenye rekodi zisizopendeza. Kosa kubwa alilofanya ni kutotumia nafasi yake kama Rais kuwadhibiti, matokeo yake wameishia kuutumia urais wake kujinufaisha wao wenyewe.

Matukio mawili ambayo hayatafutika katika historia ya Urais wa Kikwete ni ujambazi wa fedha za EPA na utapeli wa kampuni ya Richmond na ‘binamu’ yake Dowans.

Kuhusu suala la EPA, wengi wetu tunaamini kwamba bado kuna maswali mengi kuliko majibu. Japo inapendeza kuwaona baadhi ya watuhumiwa wakifikishwa mahakamani, bado haieleweki kwa nini hadi muda huu wamiliki wa kampuni iliyokwiba fedha nyingi zaidi, Kagoda, wameendelea kuhifadhiwa.

Ni kweli safari hii pana ushindani wa kutosha kwenye kiti cha urais. Ni kweli pia kwamba kama akipita, Kikwete atakuwa, kwa mujibu wa Katiba, akitumikia kwa muhula wake wa mwisho. Ninachojiuliza ni kama amemudu kufumbia uoza wote huu katika kipindi muhula wake wa kwanza huku akijua fika kuwa baada ya miaka mitano angepaswa kuomba tena ridhaa ya kupigiwa kura, hali itakuwaje katika muhula wake wa mwisho ambao hatahitaji tena kura zetu?



Barua-pepe:
epgc2@yahoo.co.uk

CHADEMA YAFUNIKA MJI WA ARUSHA

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15816&d=1288241646

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15817&d=1288241863

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15818&d=1288242109

MKUTANO WA CHADEMA UNGA LIMITED ARUSHA

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15819&d=1288242331

Wednesday, October 27, 2010

SLAA ALIVYOTIKISA DAR

Wednesday, October 27, 2010

DR SLAA ALIVYOTIKISA MWEMBEYANGA

Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wakazi wa Manzese jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake wa kampeni leo mchana.
Wapenzi na wananchama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwa na bango lenye ujumbe mbalimbali, katika mkutano wa mgombea urais kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam leo jioni.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, katika mkutano wa kampeni, kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke leo jioni.Picha kwa hisani ya Joseph Senga wa Tanzania Daima.

Monday, October 25, 2010

HUDUMA ZA MAJI VIJIJINI

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA

KAWE

Mdahalo ITV Bila Profesa Lipumba Na Wengine, Kwanini?


Ndugu Zangu,
Jana tumesikiliza mdahalo, au labda mazungumzo au mahojiano kati ya Dr Slaa ( CHADEMA) na Rosemary Mwakitwange. Mahojiano yaliyoruhusu wengine kuchangia kwa njia ya simu pia.
Tunawapongeza walioshiriki kufanya jitihada zile. Ilitoa fursa kwa sisi wapiga kura kumsikiliza Dr Slaa. Hata hivyo, pungufu kubwa kabisa lililoonekana ni namna waandaaji walivyoandaa mdahalo wa upande mmoja bila kuwashirikisha wagombea wengine wa Urais waliopitishwa na NEC. Maana, ni vema pia tukatofautisha maana ya mdahalo na mahojiano. Kama yale ya jana yalikuwa ni mahojiano tu, hakuna tatizo kwa mgombea mmoja tu kuhojiwa. Lakini kama unaitwa mdahalo, basi, tujadili maana ya mdahalo.

Kama ni mdahalo, basi, ingekuwa ni vema na busara kwa wagombea wengine wa Urais kushiriki. Bila shaka, wagombea wengine nao wana haki za msingi za kupewa nafasi ya kuelezea sera zao na kujibu maswali ya wapiga kura. Hata kama chama tawala, CCM kimeweka wazi kuwa mgombea wao hatashiriki mdahalo, lakini hatujasikia vyama vingine vitoa misimamo kama hiyo.

Wengi wetu tungependa kuona wagombea wengine wa Urais nao wakialikwa, hivyo basi, kupewa fursa ya kuelezea sera za vyama vyao na kuulizwa maswali. Kungetoa fursa ya wagombea hao kushindana kwa hoja pia. Labda kama kuna maelezo ya kuwa wagombea hao walialikwa lakini hawakuitikia mwaliko wa kwenda studioni. Au kuwa gharama za muda wa kurusha hewani mdahalo ziligharamiwa na chama cha mgombea aliyefika kwenye mdahalo/mahojiano. Kama sivyo, basi, waandaaji watakuwa hawakuwatendea haki wagombea na wapiga kura kwa ujumla wao.

Maana, tukianza sasa kujenga tabia ya kubagua wagombea itakuwa ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, tangu Uchaguzi Mkuu wa 1995, tulianza kujenga misingi mizuri ya wagombea kupewa fursa sawa. Kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 wagombea wote wa Urais walialikwa kwenye mdahalo uliofanyika kwenye iliyokuwa Kilimanjaro Hotel. Kama inavyoonekana pichani, kulikuwa na Profesa Lipumba, Augustino Mrema, Benjamin Mkapa na Bwana Cheyo. Historia ni mwalimu mzuri. Tujifunze.


NITAGOMBEA KIPINDI KIMOJA – Slaa
Mwandishi Wetu
(Pichani Dk. Slaa akihutubia maelefu ya wananchi wa mji wa Mwanza siku ya Jumatano)

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa amesema kuwa endapo wapiga kura watamchagua kuwa Rais wao basi atawatumikia kwa kipindi kimoja na hatogombea tena mwaka 2015. Dr. Slaa ametoa ahadi hiyo alipozungumza na kijarida hiki mapema wiki hii katika mazungumzo ya kina yaliyohusu kampeni yake, mipango yake na mwelekeo wa chama chake kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA amesema kuwa tangu mwanzo alipoombwa kuwa mgombea wa Urais katika uchaguzi huu alishaamua kuwa akipata nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa kisiasa nchini basi hatotaka kugombea tena kipindi cha pili akimaliza muda wake wa Urais. Dk. Slaa alirejea maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere Ikulu “siyo mahali pa kukimbilia” na kuwa yeye hakuwahi katika maisha yake kuwazia wala kutamani cheo hicho, hivyo anataka kuingia kufanya aliyoahidi kufanya na kutoka kuwaachia wengine.   

“Tangu mwanzo waliponiomba nilikubali nikiwa na nia ya kuwa Rais kwa awamu moja tu na kinyume na wengine sitoingia ili nitumie miaka miwili au mitatu kujifunza halafu nirudi kuomba niongezewe muda, mimi ninaingia tayari kufanya kazi kwani Urais hauna chuo” amesema Dk Slaa mara baada ya kumaliza mkutano wake mkubwa wa kampeni huko Shinyanga na akiwa anajiandaa na mikutano ya Mwanza na maeneo mengine nchini huku siku zikiwa zinakimbia kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 31 mwaka huu.

Akizungumzia kwa kina uamuzi wake huo Dr. Slaa amesema kuwa pamoja na kuzingatia usia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere yeye mwenyewe alikuwa na sababu zake nyingine za kutotaka kugombea tena kipindi cha pili. “Kwanza, kiumri nitakuwa nakaribia miaka sabini ifikapo mwaka 2015 (Dr. Slaa anatimiza miaka 62 Oktoba 29)  sasa heka heka za kampeni tena na mambo ya kisiasa nataka niwaachie wengine ili na mimi nifurahie maisha ya kustaafu” ameelezea.

Pamoja na sababu hiyo Dr. Slaa ameelezea vile vile nia yake ya kuhakikisha kuwa utakapofika mwaka 2015 serikali ya Chadema na chama vitakuwa vimeandaa watu wa kutosha na wenye uzoefu wa kutosha kiuongozi ili waweze kuchukua nafasi baada  yake. “Unajua CCM wamewaandaa watu wao mbalimbali kiasi kwamba wana wigo mkubwa sana wa kupata viongozi wa serikali kwani wengi wamepata uzoefu wa aina mbalimbali kwa muda mrefu. Kwa upande wetu ninataka tutumie miaka hiyo mitano kuandaa viongozi wapya kabisa wa kisiasa nchini nje ya wale walioko CCM ambao wanaweza kuiongoza serikali.”

Pamoja na sababu hiyo Dk. Slaa amesema kuwa lengo lake ni kuanzisha mabadiliko makubwa nchini ya kusahihisha makosa ya utawala wa CCM yaliyodumu kwa miaka 49. “Ni lazima tusahihishe makosa haya, hatuwezi kuendelea na njia ambayo tunajua tayari tumepotea. Tutakuwa ni watu wa ajabu kama pamoja na kujua tumepotea tutaendelea kwa hiari yetu kuchagua kupotea miaka na miaka, hivyo nataka niweke msingi wa mageuzi makubwa ya utendaji kazi na utawala nchini ili tuweze kuwarithisha watoto wetu na watoto wa watoto wetu taifa bora zaidi lenye mafanikio na maendeleo zaidi”

Akizungumzia mwelekeo wa kampeni yake ambayo kwa maoni ya watu wengi inaonekana kuwa na uhai wa aina yake Dk Slaa amesema kuwa kama kuna watu walifikiri ameingia katika kinyang’anyiro hicho ili kubahatisha basi wamefanya makosa. “Tumeingia kwa lengo la kushinda na siyo kusindikiza na kinachosimama kati yetu na ushindi ni wapiga kura!” Alisema kwa kujiamini. Akijibu swali la ni kitu gani kimemgusa hasa katika kampeni zake zilizomchukua katika kona mbalimbali za nchi yetu Dk. Slaa amesema kuwa kati ya mambo ambayo yamemgusa zaidi na kumfanya awe shime zaidi ya kuwatumikia Watanzania kama Rais wao ni hali ya makazi ya wananchi wengi kijijini.

“Wananchi wetu wengi wanaishi katika nyumba ambazo kwa kweli kabisa hazistahili kuishi wanadamu. Yaani miaka 49 ya uhuru bado watu wanaishi kama walivyoishi kabla ya uhuru na kabla ya kuja wakoloni!, hii ni dhambi ya taifa na ni aibu” alisema Dr. Slaa.

Katika mazungumzo hayo Dr. Slaa amewataka Watanzania kumchagua kwa kura nyingi na wasitishwe na kauli zenye kuwafanya wahofie kupiga kura au kutoona umuhimu wa kura bali wajitokeze kwa maelfu, wakishikana mikono katika familia kwenda kumchagua yeye pamoja na wagombea wote wa Ubunge na Udiwani ili aweze kweli kupata watu wa kushirikiana nao na wenye mtazamo mmoja.

Dr. Slaa amezungumzia mambo mengine mengi kuhusu kampeni yake, ajenda yake na malengo yake kuelekea Uchaguzi Mkuu. Mazungumzo hayo
na Dr.
Slaa yatarushwa siku ya Jumamosi asubuhi (saa za Marekani) kupitia mtandao wa http://www.bongoradio.com na baadaye yatapatikana kwa njia ya mtandao na Cds yakijumuisha mahojiano na wagombea wengine wa Uchaguzi huu.

Friday, October 22, 2010

DR W P Slaa Kujibu Maswali Live ITV

Jumamosi ijayo, yaani Oktoba 23 ni siku muhimu kwa sababu Mgombea Urais wa
Chadema, Dk. Willibrod Slaa atajibu maswali ya wananchi moja kwa moja (live)
kupitia ITV Televisheni, kuanzia saa moja jioni hadi tatu usiku. Mwambie
rafiki yako na wadau wote wa uchaguzi wasiokuwa kwenye mtandao huu, kwa njia
ya simu au ujumbe mfupi wa maandishi, ni wakati murua wa kumuuliza maswali
na kumbana kujua anataka kuifanyia nini hasa nchi hii, maana midahalo ndio
kama hiyo ya urais hatuoni kama itakuwapo tena.
Kila la heri wote, na nawatakia kazi njema.

CHANZO
[wanabidii] Re: DR W P Slaa Kujibu Maswali Live ITV

CHAGUA SAMBWEE SHITAMBALA CHAGUA CHADEMA MBEYA VIJIJINI

Mgombea ubunge wa jimbo la Mbeya vijijini Bw.Sambwee Shitambala (katikati)

CHAGUA MTELA MWAMPAMBA CHAGUA CHADEMA MBOZI MASHARIKI


Wananchi wa jimbo la Mbozi Mashariki mkoani Mbeya wakiwa wamefanya maandamano ya furaha kwa kumbeba juu juu mgombea wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Bw Mtela Mwampamba ambaye alionyesha kuitikia wito wa wananchi hao kwa kufika katika mdahalo uliokuwa umeandaliwa na asasi za kiraia mkoa wa Mbeya (Mbengonet) katika ukumbi wa RC Mbozi huku mgombea wa CCM Bw Godfrey Zambi akishindwa kutokea

CHAGUA KAZAMOYO JIDAWAYA CHAGUA CHADEMA MBARALI

mgombea ubunge Bw. Kazamoyo H. Jidawaya (Chadema)

CHAGUA SUGU CHAGUA CHADEMA MBEYA

Mgombea ubunge wa Chadema Bw Joseph Mbilinyi (MR II SUGU) akijinadi kwa wananchi katika kata ya Nonde pamoja na katika eneo hilo CCM kuendelea na kampeni zao za udiwani kinyume ya kanuni za uchaguzi

SUGU FOR MBEYA


Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini Bw. Mwambigija akimwaga upako kabla ya Sugu kupanda

Msanii mahiri G Solo pamoja na mmoja wa wasimamizi wa kampeni Kwame Anangisye wakiwa na full gwanda

Watu mbalimbali wakimpongeza baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni

Umati wa wana Mbeya ukimsindikiza Sugu baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni

ZITTO KABWE AUZA NGUO ZAKE MKUTANONI KUMCHANGIA MGOMBEA WA UBUNGE SUMBAWANGA MJINI

Zitto kabwe akionyesha fedha zilizochangwa katika mkutano wake wa kampeni leo ,kushoto ni mgombea ubunge jimbo la Sumbawanga mjini aliyechangiwa na kulia na makamu mwenyekiti wa Chadema Taifa Baadhi ya fedha zilizochangishwa na Zitto kwa ajili ya kusaidia mgombea ubunge wa Sumbawanga mjini kuwalipa mawakala wake siku ya Octoba 31


Hapa Kabwe akipata picha ya pamoja na wapenzi wa Chadema waliojitokeza kuchangia
Askari polisi ,magereza na mgambo wakilinda mkutano wa kampeni za Chadema ambao alikuwa akihutubia naibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe viwanja vya Sumbawanga mjiniNaibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe (kulia) akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga mjini mkoani Rukwa Mwalimu Norbart Yamsebo wakati wa kampeni za Chadema mjini Sumbawanga

Naibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe akiendesha harambee ya kumchangia fedha za kuweka mawakala wa mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga mjini Mwalimu Norbart Yamsebo (chadema) ,katiba harambee hiyo zaidi ya shilingi 800,000 zilipatikana huku yeye Kabwe akiuza kwa manadi kombati yake iliyonunuliwa kwa shilingi 200,000

Naibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe( kulia) akihesema fedha zilizochangwa katika viwanja vya mkutano wa kapeni vya Sumbawanga mjini wakati wa kampeni zake

Fedha zilizochangwa na wananchi wa jimbo la Sumbawanga mjini kila mmoja alitoa kulingana na uwezo wake ili kusaidia mgombea wa Chadema ashinde na apata fedha za kuweka mawakala


mapokezi ya naibu katibu mkuu wa Chadema Taifa Bw Zitto Kabwe katika jimbo la Sumbawanga mjini leo palikuwa hapatoshi,
KAMPENI za naibu katika mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Zitto kabwe katika jimbo la Sumbawanga mjini zaendelea kukiweka pabaya chama cha mapinduzi zaidi ya 2000 leo kufanya maandamano ya furaha kwa kumsindikiza mgombea ubunge wa jimbo hilo Mwalimu Norbert Yasembo .(CCM) baada ya wananachi
Pia wananchi hao jana walitumia mkutano wa kampeni za Chadema kumchangia mgombea huyo fedha za kuwalipa mawakala wake kiasi cha shilingi zaidi ya 800,000 katika harambee iliyoendeshwa na Kabwe ambaye pia alijitolea kuchangia kampeni hizo kwa kuuza kombati yake kiasi cha shilingi 200,000 .
Akihutubia katika mwendelezo wa mikutano ya kampeni ya Chadema mkoani Rukwa katika viwanja vya Rukwa High School jana mbali ya kukataa kata kata dua za wananchi hao kumwombea kuwa spika wa bunge lijalo la muungano wa Tanzania ,Kabwe alisema kuwa lazima CCM itambue kuwa hatua ya wannachi hao kuchangia kiasi hicho cha fedha ni misho mbaya kwake na kuwa isitegemee kushinda kwa miujizi jimbo hilo.
“Nasema napongeza sana kwa mapokezi haya makubwa ambayo mmeonyesha kwangu na huu ni ushadidi kuwa mgombea wa CCM katika jimbo hilo Aesha Hillary si chaguo halisi la wana jimbo la Sumbawanga mjini hivyo si vizuri kwa wachache waliobaki kupoteza kura zao kwa kumpa mgombea ambaye hatakiwi “
Alisema kuwa mkoa wa Rukwa , Kigoma na Tabora ni mikoa ambayo makao makuu yake bado hadi sasa hajaunganisha na lami hali ambayo inahitaji kuwapata wabunge makini watakaoweza kutetea wananchi wa mikoa hiyo kuwa ni sehemu ya wananchi wa mikoa ya Tanzania ambayo kwa sasa imeunganishwa kwa lami .
“Ndugu zangu Tanzania ni moja na mikoa yote ya Tanzania wananchi wake ni walipaji wakubwa wa kodi hivyo kitendo cha serikali ya CCM kuendelea kuwabagua wananchi wa mikoa hiyo ni sawa na kuwaona kuwa hawafai kupewa huduma hiyo na dawa pekee ni wananchi wa mikoa hiyo kuungana kuwanyima kura wagombea ubunge wa CCM na kuwapa wale wa Chadema ambao kupitia Rais mpya wa awamu ya tano kwa Tanzania Dk Willibrod Slaa wananchi wa mikoa hiyo wanapewa haki yao ya lami”
Kabwe alisema kuwa wananchi wa Tabora ,Kigoma na Rukwa wasipo kubali kuunganisha nguvu zao katika kuchagua wabunge wa Chadema bado CCM itaendelea kuwanfaya kuonekana kuwa wanyonge na kuwa katika mkoa wa Kigoma kwa bunge lililopita mbunge wa upinzani alikuwa ni mmoja pekee huku katika mkoa wa Rukwa pia kulikuwa na mbunge moja hivyo ni vizuri Octoba 31 kuongeza idadi zaidi ili wabunge wa mikoa ya kaskazin kuwe na idadi kubwa ya wabunge.
Hata hivyo alisema kuwa kwa upande wake hana tatizo la jimboni kwake kwani tayari ameshinda na anasubiri kuapishwa na Rais wake Dk Slaa.
Katika hatua nyingine Kabwe ameshangawa na hatua ya ulinzi mkali aliowekewa katika jimbo hilo la Sumbawanga mjini ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha askari polisi ,askari magereza pamoja na mgambo kufika kulinda mkutano jambo ambalo hajapata kuona askari magereza wakifika katika mikutano ya kampeni kama jimbo hilo la Sumbawanga mjini na kuwa yawezekana katika mkutano wake huo wafungwa pia wamefunguliwa ili kuja kusikiliza sera za Chadema.
Katika mkutano huo wa Zitto uliomalizaka kabla ya muda wa kampeni kuisha wananchi walifanya maandamano makubwa huku biashara zao zikisimama kwa muda kwa ajili ya kusukuma gari la Zitto Kabwe pamoja na ile ya mgombea ubunge wa Chadema huku wakiimba kuwa wanataka mbunge Msomi wa Chadema sio CCM .
Hatua hiyo ilionyesha kuwapa wakati mgumu askari polisi magereza na wale wa jeshi la polisi nchini kuwatuliza wananchi hao na kuwaomba viongozi wa Chadema kuwatuliza na kuwatawanya wananchi hao zaidi ya 2000 kabla ya mgombea ubunge wa Chadema kuamua kuwatoroka viongozi wenzake ofisini ili waandamanaji hao kutawanyika