Kwenye Kampeni za Urais mwaka jana JK alipokea simu katikati ya hotuba yake ya kampeni pale Manispaa ya Iringa. Baada ya kuongea na Simu aliwaambia wananchi kuwa Balozi wa marekani amemhakikishia kuwa serikali ya Marekani itaendelea kutoa misaada kwa Tanzania. Pia alikumbushia jinsi Serikali ya Marekani ilivyo na dhamira nzuri ya kutusaidia akitoa mfano wa Mwaka 2007 pale USA kupitia kwa BUSH alivyotembelea bongo na kusaini mkataba wa shilingi billion 700. Msaada huo ulikuwa wa miaka mitano. Msaada huo ni sawa na shilingi bilioni 140 kwa mwaka. Wakati huo huo Serikali ya Tanzania kwa mwaka 2009/2010 [mwaka mmoja baada ya kuanza utekelezaji wa msaada huo] ilitoa misamaha ya kodi ya shilingi bilion 700. Nusu ya hiyo misamaha ina-originate kwenye madini. Na 70% ya migodi inamilikiwa na wawekezaji wanao-originate Marekani hivyo kufanya misahamaha ya shilingi zipatazo bilioni 300 ktk huo mwaka kutolewa kwa makampuni ya kimarekani huku serikali ya marekani ikirudisha shilingi bilioni 140 [Je huo ni msaada?]. Huo ni mfano mmoja kati ya mingi iliyotawanyika kuanzia ulaya, Marekani, China Japan na kwingineko tunakoenda kulamba miguu ya hao wezi tukifikiri wanatusaidia. Kwa kuangalia mfano huo, FIKIRIA KAMA TANZANIA INGETOA MISAMAHA YA ANGALAU TSH 350 BILION KWA MWAKA KATIKA HIYO MIAKA MITANO, JE TUNGEHITAJI MSAADA WA NANI DUNIANI HAPA? Siku moja simama pale makutano ya barabara ya Bibi titi Muhamed na Ali hassan Mwinyi, hesabu Magari mangapi ya Kijapan ambayo yameuzwa yakiwa used/reconditioned linganisha na misaada ya kifedha inayotolewa na Japan uone kama kuna uwiano.Baada ya Hapo nenda Kariakoo kanunue bidhaa yeyote kuanzia nguo hadi eletronics equipments [buy at random] halafu chunguza quality yake, kisha oanisha na misaada inayotolewa na serikali ya China. Tathmini kama kuna uuwiano! ASK YOURSELF THIS QUESTION "DO WE REAL HAVE PROGRESSIVE PLANS?" ,"DO WE REAL KNOWS WHAT WE ARE DOING?" "DO WE REAL HAVE ECONOMISTS IN TANZANIA?" "DO WE REAL HAVE RESEARCHERS IN THIS NATION?"
Monday, January 17, 2011
ANGALIA HAPA JINSI Tz INAVYOVUNWA NA HAO WANAOJIITA WAFADHILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment