Thursday, September 23, 2010

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo  CHADEMA kimeendelea kukitia kiwewe chama tawala cha Mapinduzi  CCM katika jimbo la Musoma mjini kutokana na mgombea wa chama hicho katika nafsi ya ubunge kuonekana anakubalika kwa wananchi

Katika mikutano ambayo tayari imefanyika tangu kuzinduliwa kwa kampeni za chama hicho hapo siku ya jumamosi zimepelekea chama cha Mapinduzi CCM kuahirisha uzinduzi wake kila mara kwa kile wanachodai kuwa kuna vitu muhimu ambavyo vitatumiwa na chama hicho havijafika.

Mgombea ubunge katika jimbo la Musoma kupitia chama hicho Vicenti Nyerere ambaye ni mtoto wa kaka yake na Baba wa Taifa hayati Mwl Julius Nyerere,Joseph Kiboko ameonekana kuweka changamoto kubwa kwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha Mapinduzi CCM Vedastus Mathayo ambaye anatetea kiti hicho.



CCM ambayo ilipanga kuzindua rasmi kampeni zake leo Ijumaa katika jimbo la Musoma mjini lakini habari za uhakika zilizopatikana mjini jana zinasema kuwa baadhi ya viongozi wa Chama hicho wamehairisha kufanya uzinduzi huo kwa kumsubiri ziara ya mgombea mwenza wa Urais Dk Ghalib Bilal ambaye anayetarajia kuanza ziara ya za kampeni mkoani Mara mwishoni mwa wiki ijayo.



Akizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano aliyoifanya mjini hapa Nyerere alisema kuwa kujitokeza kwake kugombea ubunge kupitia chama cha upinza ni kutokana na kuchukizwa na umaskini uliokithiri ambao alisema umesababishwa na sera mbovyo za chama cha mapinduzi CCM

Alisema jimbo la Musoma mjini pamoja na kuwa rasirimali nyingi ambazo zingeweza kuwaondoa wananchi wake katika lindi la umasikini lakini zimekuwa zikiwanufaisha watu wachache jambo ambalo alisema endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo atatumia uwezo wake kupambana na hali hiyo.


Katika mkutano wa kampeni wa chama hicho katika mtaa wa Baruti,mgombea huyo wa Chadema,aliwaambia mamia ya wananchi  waliofurika kumsikiliza kuwa endapo atapata ridhaa katika kuliongoza jimbo la Musoma mjini atahakikisha anatafuta wafadhili na kuishauri serikali ili ikamilishe ujenzi wa hospital kubwa ya Kwangwa ambayo ujenzi wake ulianza miaka ya themanini lakini licha ya kuchangiwa na wakulima ujenzi wake ulisimama baada ya michango hiyo kutafunwa na viongozi wa CCM.

Hospitali hiyo ya Kwangwa ambayo inategemewa kuwa hospital ya rufaa ilianza kujengwa wakati wa uongozi wa Mwl Nyerere na kuishia njiani kutokana na ujanja wa watu wachache ambao alidai walishindwa kuthamini maisha ya wananchi wa jimbo la Musoma na mkoa wa Mara kwa ujimla.

Katika hatua hiyo Nyerere alisema kuwa kuendeleza ujenga wa hospital hiyo itakuwa moja uttekelezaji mambo matatu ambayo anaimani hata mwalimu Nyerere huko kaburi roho yake itafurahi kwani dhamira yake ilikuwa ni kuwasaidia wana Mara.

Mgombea huyo alidai kuwa mbunge aliyemaliza muda wake ameshindwa kuleta mageuzi ya kimaendeleo katika jimbo hilo kutokana na kuwa na ubinafsi na tamaa ya kupata  kuliko wenzake kitu ambacho bado kimewafanya wakazi wa jimbo la Musoma kuwa katika dimbwi kubwa la umaskini.

Katika jimbo la Musoma mjini mpaka sasa kumeonekana kuwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea watatu ambao wanagombea nafasi hiyo,wagombea hao ni pamoja na  Mstapher Wandwi(CUF) Vicent Nyerere (CHADEMA) na Vedastus Mathayo(CCM).

No comments:

Post a Comment