ELIMU, AFYA, MAJI, UMEME (BURE AMA KWA GHARAMA NAFUU VIPO NDANI YA UWEZO WETU)

Wana JF na watz kwa ujumla, napenda kuchukua fursa hii kuwaletea mada hii tuijadili. Kwa mtazamo wangu upatikanaji wa elimu na afya bila gharama yoyote ni suala ambalo lipo ndani kabisa ya uwezo wa nchi yetu. Kinachokosekana ni utashi pekee.

Serikali yetu imeshindwa kukusanya kodi na hivyo kushindwa kutoa huduma hizo kwa jamii. Kukusanya kodi ni jambo la kitaalam na linalohitaji ubunifu wa hali ya juu, kwani wlipa kodi kila kukicha huamka na mbinu mpya za kukwepa kodi. Sasa ukizingatia uhalisia wa serikali yetu, na kukithiri kwa rushwa nchini, utaona jinsi kodi inavyokusanywa kiasi kidogo sana, huku mzigo mzito wakiangushiwa wafanyakazi wa sekta rasmi.

Nitoe mfano mdogo tu jinsi tunavyokosa mapato. Natumai kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine anatumia mawasiliano ya simu za mkononi. Na kila unaponunua muda wa hewani unalipa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) 18%. Katika kila sh. 100 unayotumia shs. 15.25 (Sh. 100 inajumuisha VAT) inakuwa ni VAT (pesa ya serikali).

Kuna watumiaji waliosajiliwa wapatao milioni 9. Iwapo kwa siku hao watumiaji milioni 9 wanatumia shilingi 100, serikali inapaswa kupata sh. 137,250,000/- kwa mwezi 4,117,500,000/-. Hapo tunaweza kukusanya zaidi na zaidi iwapo tu serikali itakusanya kodi toka kwenye chanzo (tax at source), na si mfumo uliopo (tax on invoice). Yaani wakati makampuni ya simu yanapomkata mteja anapopiga simu na serikali ipate kodi yake palepale (kuweka mtandao unaofanya kazi sambamba na mitambo ya makampuni ya simu).

Hiyo ni changamoto moja tu, lakini tunamaeneo mengi sana yanayoweza kuifanya nchi hii kuwa na surplus budget. Bila kusahau Tanzania ni Dubai ya ukanda huu, naishia hapo, naomba michango yenu.