Wednesday, October 6, 2010

KAMPENI ZA JK MUHEZA LEO MCHANA…!!!


Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na wananchi wa Muheza baada ya kuhutubia Mkutano wa Kampeni leo mchana.

Mgombea Urais kupitia CCM,Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na wananchi wa Muheza baada ya kuhutubia Mkutano wa Kampeni leo mchana.

Dr. Kikwete akiwapungia wananchi wa wilaya ya Muheza wakati akiondoka mara baada ya kuwahutubia katika mkutano wa kampeni mchana huu.

DONDOO ZA KISIASA….!!!

MSAJILI WA VYAMA:

John Tendwa, amekataa  kuzungumzia uamuzi alioutoa juu ya pingamizi lililofikishwa mezani kwake  na Chadema dhidi ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete.Aalikiri kumaliza kulishughulikia pingamizi hilo na kulitolea uamuzi, lakini akasema hawezi kuwaeleza waandishi wa habari alichoamua.,”Sheria inaniagiza nikishafanya uamuzi niwape wahusika. Mimi sina madaraka ya kusema hayo.” Alisema .
Nakuongeza “Mimi nadhani kwa sasa (CCM na Chadema) wanatafakari nilichoamua. Mimi nitaweza kusema chochote baada ya wao kuzungumza, labda wakilalamika ndipo nitatoa ufafanuzi.”

MOHAMMED DEWJI:

Ambae ni mgombea ubunge katika  Jimbo la Singida Mjini  amepata mpinzani kutoka Chadema baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kutengua pingamizi aliloliweka. Ambapo hivi sasa atakutana uso kwa uso na Bw Isango Hadu, na kwa mujibu wa barua ya Nec iliyotumwa kwa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema  tume hiyo imemrudisha mgombea huyo katika orodha ya wagombea wa ubunge wa jimbo hilo.

SIASA NA MAPENZI:

MGOMBEA urais wa Chadema, Dk.Willibrod Slaa na mkewe mpya, Josephine Mushumbusi, watafunguliwa kesi wakidaiwa fidia ya Sh bilioni moja na mume wa ndoa wa Josephine, Aminiel Mahimbo.
Kesi hiyo itakayofunguliwa  katika Mahakama Kuu inawataka Slaa na Josephine kulipa fidia hiyo kutokana na mgombea huyo kudaiwa kumnyang’anya mke Mahimbo na Josephine kuvunja mkataba wa ndoa ya mke na mume mmoja.
Mwanasheria wa Mahimbo, Abduel Kitururu alisema, mteja wake anadai fidia ya Sh milioni 200 za usumbufu aliopata baada ya Slaa kumtangaza mkewe wa ndoa kuwa mchumba wake, huku akijua ni kinyume cha sheria.
Alisema Sh milioni 800 ni hasara za jumla ambazo wanaamini madhara aliyopata yanalingana na gharama hizo na anastahili kulipwa kabla hajafungua kesi nyingine kwa mujibu wa sheria ya ndoa, itakayoshughulika na masuala ya talaka na malezi ya watoto.

VURUGU ZA KISIASA:

Kutoka na vurugu zilizo wahusisha wafuasi wa vyama viwili maarufu vya siasa nchini, CCN na Chadema huko mkoani Kilimanjaro siku ya jumapili. Chama tawala mkoani humo kimelaani vikali vurugu hizo ambazo zinasemekana kuanzishwa na wafuasi wa chama pinzani (Chadema) katika eneo la mji mpya jimbo la Moshi. Bw Stephan Kazidi ambaye ni katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro alisema sikuzote siasa zautulivu ziapendeza na ndizo zinazo ifanya CCM iweze kushinda.

DK. SLAA NA MADAKTARI:

Mgombea uraisi huyo kupitia chama cha  chadema aliwaahidi wananchi kama atapewa nafasi ya kuingia ikulu basi atawalipa madaktari wote mishara yao ambao wapo katika vituo vya afya vinavyo milikiwa na madhehebu ya dini nchini akiwa na lengo la kuhakikisha wanapata malipo sawa na wale waliopo katika ajira za serikali..
Aliyasema hayo wakati alipokuwa katika mchakamchaka wake wa kupiga kampeni katika kijiji cha Makiungu wilayani Singida.
Filed under: Politics | 2 Comments

NAPE: HAKUNA UPINZANI WA KUING’OA CCM…!!!


Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM, Nape Nauye (kulia) akimnadi mgombea wa kiti cha Udiwani wa Kata ya Mwananyamala Bw.Songoro Mnyonge wakati wa kampeni za Chama cha CCM zikiendelea katika mikoa mbalimbali.
Mjumbe wa Halamashauri kuu ya Taifa Nape Nauye ambaye pia ni mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo akihutubia wakazi waKata ya Mwananyamala  katika kampeni za kumnadia mgombea kiti cha  Udiwani wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa chipukizi na mwanaharakati wa kutetea haki za watoto Nimka Lameck (11) akizungumza na wakazi wa kata ya Mwananyamala na kuwasihi kuchagua viongozi wanaojali maslahi ya watoto katika kampeni hizo.
Mgombea kiti cha  Udiwani kata ya Mwananyamala Bw.Songoro Mnyonge akimpongeza mtoto Nimka Lameck kwa hotuba nzuri aliyoitoa katika mkutano huo.
Wanachama wa CCM waliokusanyika katika kampeni hizo jana kata ya Mwananyamala.
Vijana wa CCM wakitoa burudani kwenye kampeni hizo.
Vijana wakazi wa Mwananyamala waliojitokeza kusikiliza sera za Mgombea kiti cha Udiwani kata ya Mwananyamala.
******************
Na MO Blog Team
MJUMBE Halimashauri Kuu ya CCM, Nape Nauye ametamba kuwa hakuna wapinzani wa kukitoa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kuanzia ngazi zote za Udiwani,Ubunge na Rais.
Nape alisema hayo jana wakati alikuwa akimnadi mgombea wa kiti cha Udiwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge. Akiwa katika uwanja Msufini katika Kata hiyo, Nape aliwahutubia wanachama hao na kuwataka kuchukua maamuzi sahihi kwa kuhakikisha wapinzani hawafurukuti kila nafasi za uongozi.
“Jamani, Mwenyekiti wetu, Rais Jakaya Kikwete amenituma kwenu, ameniambia niwaombe msimuangushe..mtekeleze yale anayosisitizia ushindi lazima hivyo Diwani,Mbunge na Rais ni kwa CCM, hakuna upinzani wakutung’oa’ alisema Nape huku akishangiliwa na umati wa watu.
Kwa upande wake mgombea wa nafasi hiyo ya Udiwani, Songoro aliwataka wananchi kumchagua na kuwatumikia kwani CCM, ni chama makini na kinachodajali wananchi wake.
“Nichagueni niendeleze yale yote ya CCM, kutoka katika ilani na uwezo wangu nilionao katika Siasa na uongozi’ alisema Songoro.
Katika kampeni hizo, Mwenyekiti wa Chipukizi (CCM) wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto nchini, Nimka Lameck (11) aliwahutubia wananchi na kuwataka watumie fursa hiyo kuwachagua viongozi ambao watajali matatizo ya watoto.
“Wazazi wangu, na kemea na kulaani vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto wenzetu vikiwemo vya kuuwawa bila hatia,nawaombeni msichague viongozi wasiojali na matatizo yetu’ alisema Nimka na kuwaacha wananchi wakishikwa na butwaa alipokua akisimulia jinsi watoto wanavyouwawa ikiwemo na watoto wa mitaani wanavyo pata shida.

CUF WALIA UKATA SINGIDA…!!!

Na Hillary Shoo,
Singida.
Mgombea Ubunge wa chama cha wananchi (CUF) katika Jimbo la Singida Kaskazini amelia kuwa chama chake kinakabiliwa na ukata mkali wa kifedha hali inayozorotesha kampeni zake katika jimbo hilo.
Mgombea huyo Kanyota Sizimwe Kibabi alisema hali hiyo kwa kiasi kikubwa inachochangia kuzorotesha kampeni za wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Aidha mgombe Ubunge huyo wa CUF aliyasema hayo katika mahojiano maalumu na mwandishi wetu  juu ya mikakati ya kampeni ya chama chake kabla ua kufanyika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Alisema kwamba yeye binafsi uwezo alionao kifedha, hautaweza kumwezesha kuzunguka jimbo hilo lote kuomba kura kwa wananchi kutokana na ukubwa wa jimbo hilo.
“Kwa uzinduzi tu, ilibidi tufanye harambee ambayo nayo haijatupatia fedha kiasi cha kutosha kukidhi mahitaji yote ya uzinduzi, hivyo, namshukuru sana Mungu tumefanikiwa kuzindua kampeni ingawa kwa shida shida tu .” alilalama Kanyota.
Alisema pamoja na ukata huo, hautamkatisha tamaa,na kwambva yuko ngangari kuendelea na kampeni kwa imani kwamba huenda siku moja makao makuu ya CUF,yatamwezesha ili apate nguvu ya kuweza kulinyakua jimbo hilo.
Katika hatua nyingine, Kanyota alitaja baadhi ya vipaumbele vyake endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo, ataishinikiza serikali kujenga viwanja vya ndege vikubwa kila mkoa ili wakulima waweze kusafirisha mazao yao kwa usafiri wa ndege.
Alitaja vingine kuwa ni kuhakikisha kunakuwepo mashamba darasa ya kutosha na maafisa ugani wanakuwa wa kukidhi mahitaji na kuwa karibu zaidi na wakulima.
Aidha,mgombea huyo alisema atasimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambayo inazungumzia elimu kuwa ya bure kutoka shule ya msingi hadi chuo kikuu, huduma ya afya bure na kuboresha miundombinu ya barabara.
Pamoja na Kanyota,jimbo hilo la Singida kaskazini,linawaniwa na Lazaro Samweli Nyalandu (CCM) na Msaghaa Omari Kimia (CHADEMA).

JK AUTEKA MJI KASORO BAHARI…!!!


JK akimnadi mgombea ubunge wa CCM Morogoro mjini Abdulaziz Abood leo katika uwanja wa Jamhuri katika ziara yake ya kampeni ya siku mbili mkoani humo.

JK akihutubia wananchi wa Morogoro uwanja wa Jamhuri jana.

Umati mkubwa ukiwa umefurika kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Marogoro jana.

Maelfu ya wakazi wa mji kasoro bahari walifurika kwenye Uwanja wa Jamuhuri kusikiliza sera za JK jana.
Mkazi wa Matombo, Morogoro Vijijini Mashariki, akipuliza vuvuzela la asili kwenye mkutano wa kampeni wa Jakaya Kikwete jana.

JK NA AHADI ZA ZINDUKA…..!!!!

Kikwete alitoa ahadi hiyo juzi kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine,mjini Mbeya.
Katika mpango wake wakupambana na malaria, serikali inatoa vyandarua kwa watoto na wanawake wajawazito ambayo ni msaada wa serikali ya Marekani, uliotolewa na Rais George Bush alipotembelea nchini 2008 aliongeza  ana mpango wa kugawa vyandarua viwili kila nyumba ili kukomesha ugonjwa wa malaria.

“Tupambane na kukomesha maralia kwani ndio gonjwa linaloweza kuzuilika kuliko Ukimwi,” JK
“Kuna suala la kiwanda cha makaa ya mawe cha Kiwira kiwanda hiki kilikumbwa na matatizo makubwa yakiwemo ya kisiasa, kiasi cha uzalishaji kusimama,” alisema Kikwete na kuongeza:  “Lakini sasa tumeshatafuta fedha kwa ajili ya kuanza uzalishaji mkubwa wa umeme wa megawati 200, tutawalipa wafanyakazi fedha zao wanazodai na pia tutaongeza wafanyakazi wengine.”
Kiwanda cha Kiwira kilichoko katika wilaya za Kyela na Ileje, kilikumbwa na matatizo mbalimbali yakiwamo ya uwekezaji na kusababisha uzalishaji kusimama na hivyo wafanyakazi kudai mabilioni ya fedha.

SLAA NA POSHO ZA WABUNGE…!!!


MGOMBEA aliyopo  katika michakato ya urais kwa tiketi ya  Chadema  Dk Wilbroad Slaa amesema, miongoni mwa mambo atakayo yafanyia kazi akipewa nafasi ya kuingia ikulu kama Rais  wa Tanzania, nitashusha bei za vifaa vya ujenzi ili kuwezesha wakazi wa Dodoma kujenga nyumba za kisasa na kuondokana na nyumba za tembe wanazo zitumia kwa sasa. Aliyasema hayo  alipohutubia wananchi wa kijiji cha Winza Kibakwe wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya kampeni zake.

“Nikichaguliwa kuwa Rais, Serikali yangu  itapunguza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika vifaa vya ujenzi hasa vinavyotengenezwa nchini, kama vile saruji, ili kuwezesha masikini kujenga nyumba bora”,na vilevile  hatuta ishia hapo tu pia tuitapunguza marupurupu kwa wabunge na kuelekeza fedha hizo katika mfuko wa miradi ya maendeleo”.

NYAMAGANA YA PATA MPINZANI……!!!!

Muheshimiwa, Lawrence Masha  itabidi apande  ulingoni kupambana na mgombea wa Chadema Bw Ezekiel Wenye katka kuligombania jimbo la Nyamagana.
Ikumbukwe kuwa muheshimiwa Masha aliweka pingamizi dhidi ya mgombea huyo wa upinzani kwa kigezo kuwa si raia watanzania, lakini tume ya uchaguzi imetoa uamuzi wa kumrudisha mpinzani huyo katika kinyang’anyiro hicho.
Kutokana na uamuzi huo wa Nec, Chadema jana ilikuwa ni nderemo na vifijo baada ya kupata maamuzi hayo ambaye yanaonyesha upepo wa upinzani kuzidi kuvuma kwa kasi.
Mwenyekiti wa kamati ya wagombea wa Chadema, Dadi Igogo alinukuliwa akisema jana  kuwa wamepokea uamuzi huo  kwa furaha na kwamba, sasa wanajipanga kupata ushindi wa kishindo.”Tunafurahi kwa uamuzi huo kwa kuwa sasa imebainika kuwa ushahidi uliotolewa na mlalamikaji kuwa Wenje sio raia haukujitosheleza,” alisema Igogo.
Muheshimiwa  Masha alisema kuwa yupo tayari kupanda ulingono na  Wenje  na anaamini ushindi utakuwa wa kwake.Aliongozea ya  kuwa uamuzi wa tume ni uamuzi, atauheshimu.

DONDOO ZA KISIASA…..!!!!

Kama tunavyo fahamu mchakato mzima wa kuelekea uchaguzi mkuu 2010 umekwisha anza na unaendelea kushika kasi kubwa na wagombea wa nafasi tofauti wapo tayari kwenye kampeni nzito hivi sasa.

CCM

Akizungumza na wakazi wa ileje katika harakati zake za kupiga kampeni ili wanachi wa mrudishe madarakani kwa ungwe ya pili, mgombea uraisi muheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliwataka Watanzania wasifanye kosa la kuchagua wapinzani ambao hawawezi kufanya kazi na wananchi kwa kipindi kirefu kama inavyofanya chama chake. “ Kuna vyama utaviona wakati wa uchaguzi tuu na baada ya hapo vinaingia mitini vyama vya aina hiyo havifai na havita weza kuwaletea maendeleo zaidi ya kutaka madaraka tu” alisema JK

MSAJILI WA VYAMA

Bw John Tendwa amewatabiria mazuri vyama vya upinzani katika bunge lijalo kama tu wataweza kuzichanga karata zao vizuri. Amesema hayo wakati hali ikionekana wazi kuwa upinzani umezidi kukuwa ukilinganisha na hapo awali na hiyo imechangiwa na baadhi ya wabunge kutoka chama tawala kuhamia upande wa upinzani. Katka utabiri wake huo alisema upinzani wanaweza kupata nafasi hata mpaka mia moja bungeni.

APPT-MAENDELEO

Kampeni hazichagui mahali pakuzinadi. Na hili lilionekana zahiri pale mgombea uraisi kwa chama cha APPT kukata utepe wa kampeni zao katika kituo cha mabasi ya daladala cha rozana pale Buguruni. Ukilinganisha na vyama vingine vya siasa ambavyo vimesha zindia kampeni zao na kuvutia maelfu ya watu kwa upande wa APPT ilikuwa tofauti ambapo hapakuwa na watu wengi walio kuwa tayari kusikiliza sera za chama hicho.

JAJI MKUU

Kesi zilizopo mahakamni haziruhisiwi kuzungumzwa katika ulingo wa upigaji kampeni alisema jaji mkuu wa Tanzani  Augustine Ramadhani. Na hilo ni baada ya chama cha Chadema kuzungumzia kesi za EPA wakati wa uzinduzi wa kampeni zao sikiu ya tarehe 29.08.2010. Jaji mkuu aliyasema hayo katika semina ya siku tatu inayo wa husisha majaji wa mahakama toka nchi 12 za Afrika ambapo Raisi wa Zanzibar Abeid Amani Karume aliizindua rasmi.

CHADEMA

Wameruka vihunzi kutumia lugha isiyotakiwa katika uzinduzi wa kampeni zao katka viwanja vya jangwani Dar es Salaam na kusema kuwa wanaona hawakutendewa haki na televisheni ya TBC ya kuto kurusha hewani matangazo yanayo husu mkutano yao. Mwenye kiti wa kamati ya kampeni ya chama hicho Profes Mwesiga Baregu alikuwa akitoa tarifa juu ya kampeni zao zinazo endelea kwasasa na kupinga baadhi ya tuhuma toka kwa chama tawala CCM.
Filed under: Politics | 6 Comments

MAMA SALMA KIKWETE AWANADI WAGOMBEA SINGIDA…!!!

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akikagua gwaride Agosti 31,2010 mara alipowasili Itigi Mkoani Singida katika shughuli zake za kuwahamasisha wanawake wa UWT kuhusu Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akimtambulisha mgombea Ubunge kupitia CCM Kondoa Mashariki Mkoa wa Singida John Lwanji Agost i 31,2010. Mama Salma yupo mkoani Singida kuwahamasisha wanachama wa UWT kuhusu uchaguzu Mkuu ujao.
Mgombea Ubunge Viti Maalumu Wanawake Mkoani Singida Martha Mlata akiwaomba wanawake wa Mkoa huo wampigie kura katika Uchaguzi Mkuu ujao. Pichani nyuma ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akiwa amewabeba watoto mapacha Agost 31,20101 alipowasili katika kijiji cha Kinya Mshindi Mkoani Singida kuanza ziara yake ya kuwahamasisha wanawake kuhusu uchaguzi mkuu.(Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

CHADEMA YATOA UFAFANUZI JUU YA WAGOMBEA WAKE…!!!

Mwenyekiti wa kamati ya Taifa ya kampeni (CHADEMA) Prof.Mwesiga Baregu akitoa ufafanuzi ofisini kwake juu ya mgombea mwenza wa chama hicho kuwa ni mwasisi wa muda mrefu wa chama cha Chadema pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar ni mwaminifu katika chama na “sisi katika chama chetu tunamtaka mtu anayejua kusoma na kuandika tunaamini anaweza akatufaa na kuwa Kiongozi vilevile”  aliongezea kusema katika uchaguzi wa mwaka huu kama kuna mtu anafikiria kuiba kura basi tunaomba asifikirie kabisa kwani yasijeyakatokea kama yaliyotokea nchini Kenya alimaza kwa kusema kwani si mliyaona yaliyotokea nchini kenya.
Filed under: Politics | 6 Comments

DONDOO ZA KISIASA…!!!

CCM

Chama tawala kimefanikiwa kuisambaratisha ngome ya upinzani  ya Chadema huko Mbalizi Mbeya vijijini. Ambapo takribani ya viongozi sita na wanachama wapatao 367 walijiunga rasmi na chama cha mapinduzi. Mwiongoni mwawalio jiunga na CCM ni katibu wa zamani wa Chadema ambae alikuwa katibu mkoa Bw Ipyana Seme akiwa na mkewe. Tukio hilo lilitokea wakati mgombea kiti cha uraisi kwa tiketi ya chama tawala mheshimiwa Jakaya Kikwete alipokuwa akinadi sera za chama chao. JK ameahidi kutoa kumwaga pikipiki za miguu mitatu almarufu kama (Bajaji) takribani 400 kwa ajili ya wagonjwa kwa nchi nzima na gari mmoja la wagonjwa la kituo cha afya cha Mkwajuni ilikuwasafirisha wajawazito wilaya ya chunya,na ahadi hiyo itatekelezwa pindi atakapo cha guliwa kurudi madarakani.

CUF

Profesa Ibrahimu Lipumba nae hakuwa nyuma katika heka heka za upigaji kampeni. Ambapo marahii alikuwa Mjini Kilwa na kuvuta umati mkubwa wa watu , akimwaga sera zake kwa wanakilwa aliwasihi wawachague madiwani na wabunge toka CUF kwa ajili ya kuwaletea maendeleo. Aliongeza kwa kusema anayafahamu malalamiko yao ambao hayajaweza tatuliwa kwa hiyo huu ndio wakati muafaka wa kufanya mabadiliko katika uchaguzii wa mwaka huu.

SAU

Kwa upande wa visiwani Zanzibar chama cha Sauti ya Umma kimechemsha kumsimamisha mgombea  kwa upande wa uraisi na hiyo nibaada ya kutofanikiwa kurejesha fomu kwa wakati unaotakiwa katika tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC). Mgombea uraisi kwa tiketi ya chama hicho alikuwa Bw Haji Mussa Kitole.

CCM

Mama Salma Kikwete nae hakuwa nyuma katika mchakato mzima wa uchaguzi. Akimuonga mkono mumewe katika vita ya kurudi ikulu alisema sikweli kuwa wapinzani ndio ndio wapo mbele katika mpambano dhidi ya rushwa! nalipinga hili rushwa ilianza kukemewa tangu miaka hiyo ya TANU na hakukuwa na upinzani wowote. Aliyasema hayo wakati akihutubia wanaccm wilaya ya Dodoma mjini.

CHADEMA

Halima Mdee ambae ni mgombea ubunge jimbo la kawe kupitia Chadema aliwambia wanachi waliojitokeza wakati akipiga kampeni huko bunju B kuwa akishinda wasimwite muheshimiwa. Akipigia debe sera zake alisema ameamua kugombea ili aweze kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayo wakabili na uzuri matatizo yenyewe anayafahamu.
Filed under: Politics | 6 Comments

NDESAMBURO AKATA UTEPE MJINI MOSHI…!!!


Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Philemon Ndesamburo akihutubia wananchi wa Jimbo hilo waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho hivi karibuni kwenye viwanja vya Manyema.
Umati mkubwa wa wafuasi wa Chadema na Wananchi wa Jimbo la Moshi mjini waliofurika viwanja vya Manyema katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni wa mgombea Ubunge wa chama hicho,Philemon Ndesamburo hivi karibuni.
Filed under: Politics | 4 Comments

MAMA MWANAMWEMA AMPIGIA DEBE MUMEWE Dk.SHEIN..!!!


Mke wa Makamu wa Rais na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Mama Mwanamwema Shein, akihutubia Wanawake wa Jumuiya ya UWT Mkoa wa Kusini Unguja kwenye mikutano ya ndani ya CCM uliofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati Dunga
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Mama Mwanamwema Shein kulia, akisalimiana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa Mkoa wa kusini Unguja alipowasili katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja Dunga kwa ajili ya kuwahutubia wananchi hao mkutano wa ndani leo.
Filed under: Politics | 8 Comments

RAIS JAKAYA KIKWETE AWATEKA WANANCHI WA SUMBAWANGA MJINI…!!!


Rais Jakaya akishuka kwenye Helkopta mara baada ya kuwasili Sumbawanga mjini tayari kwa mkutano uliofanyika jana kwenye uwanja wa Mandele mjini humo.

Rais Jakaya akigombewa na wanaCCM na wananchi wa Sumbawanga ili kupata japo nafasi ya kumsalimia.
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete akimnadi kwa wananchi mgombea Ubunge wa jimbo la Sumbawanja mjini kupitia chama hicho,Bw.Khalfan Hayeshi pindi alipokuwa katika mkoa wa Rukwa jana.

Hizi ni picha  tofauti zikionyesha umati wa wakazi wa Sumbawanga mjini waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni ili kumsikiliza rais Jakaya Kikwete jana wakati alipohutubia wakazi wa mji huo

No comments:

Post a Comment