nahisi dalili zote kuwa yaweza kuwa kweli ama uwongo pia, pande zote zaweza simama ikiwa lisemwalo lipo, ninapozungumzia uwongo namaanisha yaweza kuwa mbinu ya hawa majangili wa madaraka, kuandaa kashfa kama hii wakati watu wakielekeza macho na masikio yao kwenye hili tuu wao waendeleze walilokwisha panga siku nyingi,, ni wazi na ushahidi upo bakhresa ni swahiba wa huyu jamaa, na sasa wanataka kutuchanganya waislamu nchini na hizi hila zao,. uislam utabaki kuwa safi na huu uchafu wao utapita,,

na pengine haya yote yanatokea kwa sababu hata matumizi ya mbinu za wizi hayakukamilika vizuri kutokana na ukweli kwamba hawakutegemea hata kidogo nguvu kama hii aliyonayo Mh Dr. Slaa (Weapon) kutokea baada ya wao kupata ushindi wa kinafiki kama ule wa 2005 wakidhani mambo yatabaki vilevile..na sasa upepo ghafla ukabadilika hivyo kukosa mikakati ya kueleweka kufanya haya ndio maana imekuwa rahisi kwa wao kukamatwa...

lingine ambalo ni dhahiri kabisa ni kwamba kuna uwezekano taarifa kama hii kufichwa na vyombo vya habari kwa vitisho., pengine tungoje kutoka bbc coz hata leo hii walitangaza taarifa iliyotowa kuhusu TANZANIA KUWA KATIKA HALI MBAYA KUTOKANA NA KUTOKUWA NA UHURU WA KUJIELEZA