Kuelekea Uchaguzi Jumapili:.List ya Ahadi za Dkt. JK vs Dr. Slaa
Ahadi za Dkt. JK:- Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
- Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
- Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
- Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) na NYANZA- Shinyanga na Mwanza
- Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
- Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
- Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
- Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
- Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
- Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
- Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
- Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
- Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
- Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
- Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
- Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
- Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
- Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
- Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
- Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
- Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
- Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
- Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
- Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
- Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
- Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
- Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
- Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
- Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
- Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
- Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
- Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
- Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
- Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
- Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
- Kulinda haki za walemavu- Makete
- Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
- Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
- Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
- Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
- Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
- Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
- Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
- Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
- Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
- Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
- Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
- Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
- Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
- Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
- Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
- Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
- Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
- kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
- kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
- ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
- Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
- Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
- Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
- Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
- kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
- Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
- Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
- Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
- Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
- Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
- Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
- Kuwapokonya eneo TanzaniteOne baada ya 2012
- Kujenga Maabara kubwa na ya kisasa kuliko zote dunia -Tanga
Ahadi za Dk Slaa:
1. Kujenga nchi isiyo na ufisadi
2. Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
3. Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
4. Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
5. Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
6. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
7. Kutoa huduma bora za afya na elimu bure
8. kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
9. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
10. Kubana matuzi Ikulu (Yuko tayari kula mihogo)
11. Kupunguza idadi ya baraza la mawaziri hadi 15
12. Mawaziri kuteuliwa nje ya Bunge
Tumia AKILI yako kupima mgombea anayekufaa na TUMIA haki yako kumchagua
|
No comments:
Post a Comment