DK. BILAL ATUA NGARA MKOANI KAGERA..!!!Posted by Blog Team on September 23rd, 2010
Mgombea Mwenza wa Urais kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib, akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Kanazi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Luganzo uliopo Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera jana Sept 22, ambapo leo ameanza ziara ya mikutano ya kampeni katika mkoa huo.
Diwani wa Viti maalum, Catherine Edward, akipiga magoti kuomba kura mbele ya Mgombea Mwenza wa urais Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Kanazi leo asubuhi.
Wananchi wa Kijiji cha Kanazi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji hicho leo asubuhi.
Filed under: Politics | No Comments
RESEARCHES: CEREBRAL MALARIA MAY HAVE PASSED FROM GORILLAS TO US!!!…..!!!!Posted by Blog Team on September 23rd, 2010
Humans may have originally caught malaria from gorillas, scientists say.
Until now, it was thought that the human malaria parasite split off from a chimpanzee parasite when humans and chimpanzees last had a common ancestor.
But researchers from the US, three African countries, and Europe have examined malaria parasites in great ape faeces.
They found the DNA from western gorilla parasites was the most similar to human parasites.
Cerebral malaria Malaria is caused by a parasite called Plasmodium, and is carried by mosquitoes.
The most common species found in Africa, Plasmodium falciparum, causes dangerous cerebral malaria. Over 800,000 people die from malaria each year in the continent.
Until now, scientists had assumed that when the evolutionary tree of humans split off from that of chimpanzees – around five to seven million years ago – so had Plasmodium falciparum.
This would have meant that humans and malaria co-evolved to live together. But new evidence suggests human malaria is much newer.Members of the team Dr Martine Peeters and Dr Eric Delaporte of the University of Montpelier in France are working with hunters and loggers in Cameroon, who spend a lot of time in the forests.
They will investigate whether these workers carry malaria parasites from the gorillas, which would suggest that new infections from other species can still happen.
They also do not yet know how badly apes are affected by malaria. Dr Hahn said that the team would now like to find out whether apes are able to catch the malaria parasite, without getting ill or dying in the way that humans do.
source: BBC
Blog team: The relationship between gorillas and human is much closer than others think ,due to the fact most of diseases exist in human are found to them too. But who passes to another, is it gorilla to us or us to gorilla?
Filed under: Politics | No Comments
MO AANZA KAMPENI SINGIDA….!!!Posted by Blog Team on September 22nd, 2010
Jamani sio kiduku bali…MO akicheza ngoma ya uzinduzi wa kampeni katika Kijiji cha Unyamikumbi.
Mgombea Ubunge jimbo la Singida mjini MO akizungumza na wananchi wa Kata ya Majengo kwenye mkutano wa kampeni.
**************
Na Hillary Shoo,
Singida.
MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Singida mjini (CCM) Mohammed Dewji amesema kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa Mbunge wao kwa awamu nyingine ataboresha zaidi sekta ya elimu kwa kuhakikisha kuwa kila Tarafa inakuwa na shule ya kidato cha tano na sita.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Unyamikumbi Dewji maarufu kwa jina la MO alisema katika kipindi cha miaka mitano akiwa kama mbungew wa jimbo hilo ameweza kutumia kiasi cha shilingi milioni 500 kwenye sekta ya elimu pekee.
Alisema kiasi hicho cha fedha kulitumika kwa ajili ya kusomesha wanafunzi 2,200 ambao wazazi wao hawana uwezo pamoja na yatima.
Dewji alisema alitumia shilingi milioni 44 kwa ajili ya kusomesha wanafunzi hao huku akitumia kiasi cha shilingi milioni 5 alitumia kwa ajili ya kununua jumla ya madaftari 23,000 kwa shule zote za msingi za serikali na binafsi zilizopo katika jimbo la singida mjini.
Aidha MO alisema kuwa hatua hiyo imetokana na ushirikiano baina yake na wananchi wa jimbo hilo kwa kumpa sapoti katika kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.
Hata hivyo alisema mara baada ya wananchi kumpa ridhaa ya kuwa Mbunge wao mwaka 2005, Mkoa wa Singida ulikubwa na njaa, ambapo yeye akiwa kama Mbunge wao alitoa msaada wa chakula ambapo wanafunzi wote wa shule za msingi walipewa uji bure kwa kipindi cha miezi minne mfululuzo.
Alisema msaada huo ulimgharimu kisi cha shilingi milioni 30, ambapo pia idadi ya mahudhurio kwenye shule hizo yaliongezeka kwa asilimia kubwa.
MO akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Majengo Salu Mahami.
MO akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Unyamikumbi Moses Ikaku.
Mojawapo ya mabango ambayo yanatumika kumnadi MO.
DK. BILAL AANZA KAMPENI MKOA WA KIGOMA…!!!Posted by Blog Team on September 22nd, 2010
Mgobea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kigoma mjini, Peter Selukamba, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwanga mjini humo jana Sept 21.
Mgombea Mwena wa urais kupitia tiketi y CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya Kabila la Waha, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma jana mchana kwa ajili ya kufanya mikutano ya kampeni katika mkoa huo.
Mgombea Mwenza wa Urais kupitia tiketi ya CCM, Dkmed Gharib Bilal, akisalimiana na mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Peter Selukamba baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mjini Kigoma jana mchana Sept 21 kwa ajili ya kufanya mikutano ya kampeni.
Mgombea Mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM wa Mkoa wa Kigoma wakati akiingia kwenye Viwanja vya Mwanga mjini Kigoma jana Sept 21 kufanya mkutano wa kampeni ikiwa ni pamoja na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo Peter Selukamba.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kigoa katika mkutano uliofanyika Viwanja vya Mwanga mjini humo jana Sept 21.
Wananchi wa Kigoma wakishangilia.
Dk. BILAL AMNADI RAGE TABORA MJINI..!!!Posted by Blog Team on September 21st, 2010
Mgombea Mwenza wa Urais Kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Tabora mjini, Aden Ismail Rage, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Uyui leo Sept 21.
Mgombea mwenza wa Urais kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ndala mkoani Tabora wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana kabla ya kuingia Tabora mjini Sept 20.
Mgombea mwenza wa Urais kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Tabora mjini wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekonda Uyui jana Sept 20. (Picha na Muhidin Sufiani)
KIVAZI CHA LEO…!!!Posted by Blog Team on September 21st, 2010
DK. BILAL ATUA TABORA AUNGURUMA JIMBO LA ROSTAM AZIZ…!!!Posted by Blog Team on September 21st, 2010
Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombe ubunge wa Jimbo la Igunga, Rostam Aziz, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Choma Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora.
Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya kabila la wasukuma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Lusu Nzega Ndogo , akitoke Visiwani Zanzibar alikokwenda kuhudhulia uzinduzi wa kampeni za urais, ambapo jana Sept 20 ameanza ziara yake ya kampeni katika Mkoa wa Tabora.
Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nkinga Wilaya ya Igunga wakati akiwa njiani kuelekea Kijiji cha Ndala kufanya mkutano wa kampeni ikiwa ni pamoja na kumnadi mbombea ubunge wa jimbo la Nzega, Hamis Kingwangala Sept 20. Kulia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Igunga, Rostam Aziz.
Mgombea ubunge wa jimbo la Igunga, akiomba kura kwa wananchi wa Kijiji cha Nkinga, wakati msafara wa mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, ulipokuwa ukipita mahala hapo kuelekea Kijiji cha Ndala.
Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiagana na mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga, Rostam Aziz, baada ya kumaliza mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Kijiji cha Choma Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora jana Sept 20.
CHAGUENI CCM TUMALIZE KAZI – DKt.BILAL..!!!Posted by Blog Team on September 17th, 2010
Mgombea mwenza wa urais wa Tanzania Dkt, Mohamed Ghalib Bilal akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji jana kwenye viwanja vya stend ya zamani
******************
Na Hillary Shoo, Singida.
MGOMBEA mwenza wa nafasi ya Urais (CCM) Dk. Mohamedi Bilal ameomba wananchi wa Singida kuchagua wagombea wa CCM, ili kuunga mkono mafanikio ya ujenzi wa barabara za lami zilizotekelezwa kwa sera ya chama hicho,mkoani hapa.
Dk.Bilali aliyasema hayo juzi, kwenye mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 31 mwaka huu, uliofanyika katika kituo cha zamani cha mabasi, mjini Singida.
Alisema kuwa, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita serikali ya CCM ilijitahidi kutekeleza ilani yake ipasavyo, ikiwemo ujenzi wa barabara za lami, maji, afya na elimu ambavyo vyote vitasaidia sana kuongeza kasi ya maendeleo ya mkoa.
“Watanzania wenzagu, kutokana na ushirikiano wenu mkubwa mliouonyesha kwenye uchaguzi mkuu uliopita, kwa kuchagua Chama Cha Mapinduzi na mkashika nafasi ya pili kitaifa, nawaomba sana tena safari hii mkafanye hivyo hivyo….;”alisema Dk.Bilali.
Aliomba waichague CCM ili iendelee kutekeleza ilani ya uchaguzi mwaka 2010-2015, ikiwemo kila kijiji kuwa na zahanati yake, vituo vya afya kwenye kata, kila mkoa kuwa na hospitali ya rufaa, huku hospitali zote za wilaya nazo zikiimarishwa.
Alisema katika miaka mitano ijayo serikali ya CCM kupitia sera zake safi,kila mwananchi wa vijijini atapata huduma ya maji safi angalau asilimia 65 na wale wa mijini asilimia 75, huku sekta za miundo mbinu na kilimo nazo zikipewa umuhimu mkubwa.
“Kasi ya maendeleo Tanzania ni nzuri ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika kutokana na rasilimali nyingi tulizonazo, ikiwemo madini ya uranium ambayo yatatufanya tuwe wa sita kwa uzalishaji Duniani……,muhimu kabisa kuharakisha maendeleo,”alisema Dk.Bilali.
Aidha alitumia fursa hiyo kunadi wagombea udiwani na mbunge jimbo la Singida mjini Mohamed Gulam Dewji, akiwataka wananchi kuhakikisha wanampa kura zote Dewji, ili alete maendeleo, kama alivyofanya katika sekta ya afya,elimu na maji.
Dk.Bilali alitarajia kukamilisha ziara yake mkoani hapa jana ijumaa jioni, kwa kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni katika kijiji cha Shelui, wilayani Iramba na baadaye kuendelea na safari zake katika maeneo mengine nchini.
Mgombe Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitoka kwenye uwanja wa mkutano wa Stendi ya zamani ya Mabasi baada ya kumaliza mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida mjini Mohamed Dewj (kulia).
Wananchi waliofurika kushuhudia kampeni hizo za CCM.
Wananchi wa Singida Mjini, wakiwa na mabango yenye picha za mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mohamed Dewji, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Stendi ya zamani ya mabasi.
Msafara wa mapikipiki ukimpokea mgombea mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiingia Singida mjini kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea wa jimbo hilo Mohammed Dewji.
Mabango ya Mohammed Dewji yakitawala mjini Singida.
Mbwembwe za uchaguzi hili ni gari la mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mohamed Dewj, likiwa limepi gwa rangi ya CCM na kubandikwa picha za mgombea huyo.
Filed under: Politics | 2 Comments
CUF NA NCCR- MAGEUZI WAWASHA TAA KUELEKEA UCHAGUZI 2010 VISIWANI…!!Posted by Blog Team on September 16th, 2010
Na MO BLOG TEAM.
CHAMA cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi, leo vitazindua kampeni zao kusaka kura za wananchi katika uchaguzi ujao.
Wakati CUF itazindua kampeni zao katika viwanja vya Kibanda-maiti katika Jimbo la Amani asubuhi ya leo, NCCR- Mageuzi itakuwa katika viwanja vya Komba-wapya katika Jimbo la Rahaleo.
“Tunatarajia kuzindua kampeni Siku ya alhamisi na kila kitu kiko sawa sawa,” alisema Issa Kheri ambaye ni Meneja wa Kampeni za CUF.
Haji Ambar Khamis, mgombea urais wa Zanzibar kupitia NCCR-Mageuzi, kwa upande wao “maandalizi ya kampeni yamemalizika pamoja na kuwa na matatizo ya kifedha, tutapigana kushinda uchaguzi.”
Wakatio huo huo, Makamu wa Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali aliwataka wapigakura hasa wanawake kudharau mwito wa kuacha kupiga kura.
“Kuna taarifa kwamba baadhi ya watu wanatembea kuwakatisha tamaa Wazanzibari wasipige kura,” alisema Ali.
Filed under: Politics | No Comments
KILIMANJARO KULIKONI NA KAMPENI 2010….???Posted by Blog Team on September 16th, 2010
Na MO BLOG TEAM.
Hii ni mara ya pili sasa tunasikia ndani ya kipindi hiki cha kampeni mkoani Kilimanjaro kuzuka vurugu. Mara ya kwanza zilikuwa baina ya CCM na Chadema ,ambapo msimu huu wafuasi na wanazi wa vyama vya CCM na TLP kwenye mji mdogo wa Himo mkoani humo jana asubuhi ilibidi waweke mabango yao kandona kuzidunda kavukavu kwa takribani saa moja baada ya kuzuka kwa mvutano baina yao saa chache kabla ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete kuwasili eneo hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, wafuasi hao walichapana makonde hayo baada ya wafuasi wa mgombea ubunge Jimbo la Vunjo, Augustino Mrema kupandisha bango kubwa linalomnadi katika lango la kuingilia mjini humo, ambapo wafuasi wa CCM waliwazuia na kuwalazimisha kulishusha.
Habari zinasema bango hilo limekuwa likiwekwa mahali hapo tangu mwanzo wa kampeni Agosti mwaka huu, huku mgombea huyo wa TLP akitumia vijana aliowaajiri kulibandika bango hilo linalosomeka “Mchague Augustino Mrema, awe mbunge wa Vunjo kwa tiketi ya TLP” kila asubuhi na jioni kuliondoa kuhofia kuharibiwa.
Lakini jana asubuhi wakati wafuasi hao wa Mrema wakilipandisha bango hilo, ndipo vijana wa CCM uvumilivu ulipo washinda nakuamua kuwazuia na kusababisha kuibuka kwa tafrani hiyo ya nguo kuchanika.
Blog team: Swali ambalo inabidi tujiuliza je huko Kilimanjaro ndio kuna upenzi mkubwa wa siasa au kwa sababu baadhi ya viongozi ni wazaliwa wa huko ndio maana vurugu kwao lazima pamoja na viongozi wao kuwaomba kuwa wastarabu??
Filed under: Politics | No Comments
KAMPENI ZA JK SAME NA ROMBO LEO..!!!Posted by Blog Team on September 15th, 2010
JK akimnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango alipofanya mkutano wa kampeni tarafa ya Ndungu kwenye jimbo hilo.
Umati wa wanaCCM ukiongozwa na Mgombea ubunge wa jimbo la Same Mashariki,Anne Kilango wakimsubiri JK awasili kwenye uwanja wa mkutano akitokea Mombo mkoani Tanga.
Wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakimshangilia JK wakati akimwaga sera katika jimbo la Same Mashariki leo.
JK akisalimiana na mgombea ubunge wa Jimbo la Rombo Mh. Basil Mramba wakati wa mkutano wa kampeni katika jimbo hilo.
Wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Rombo,wakimsikiliza JK alipokuwa akiwahutubia katika jimbo hilo leo.
Wanachama wa CCM jimbo la Rombo wakila kiapo.
Kina mama wa Same wakicheza na Kuimba ngoma za Kipare kukisifu chama cha Mapinduzi CCM.(Picha kwa hisani ya Kikosi cha kazi)
JK AMNADI JANUARY MAKAMBA BUMBULI…!!!Posted by Blog Team on September 14th, 2010
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa wananchi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Bumbuli Bwana January Makamba wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Bumbuli jana jioni.Bwana Makamba amepita bila kupingwa katika kinyang’anyiro hicho.
Mgombea ubunge Jimbo la Bumbuli January Makamba akisalimiana na wananchi wa Bumbuli mbele ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Mgombea Urais kupitia CCM wakati wa mkutano mkubwa wa kampeni jimboni hapo.
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wanachama wa CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Bumbuli, wilayani Lushoto jana jioni.
Wanachama wa CCM wakiimsikiliza mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Bumbuli,wilayani Lushoto jana jioni.(Picha na Freddy Maro na Kikosi kazi)
CCM WALALAMA POLISI,CHADEMA KUTUMIA WATOTO KUNG’OA MABANGO YA MGOMBEA WAO..!!!Posted by Blog Team on September 14th, 2010
Na Hillary Shoo,
Singida.
CCM imelalamika polisi kuwa CHADEMA wameanza kampeni chafu kwa kuwatumia wanafunzi wa shule za msingi kung’oa mabango ya mgombea wake katika jimbo la Singida mashariki.
Hali hiyo imebainika baada ya katibu wa CCM wilaya ya Singida, Cosmas Kasangani kutoa taarifa polisi kuwa mabango ya mgombea wao wa ubunge jimbo la Singida mashariki, Jonathan Njau katika kijiji cha Makiungu, yameng’olewa na watoto.
Watoto wanaodaiwa kuyango’oa mabango hayo, wametajwa kuwa ni wanafunzi wa shule ya msingi na wana umri kati ya miaka sita hadi 12.
Jimbo hilo lipo katika mchuano mkali likiwaniwa vikali na wanasheria wawili ambao pia ni ndugu, Tundu Lissu wa chama cha CHADEMA na Jonatha Njau kutoka chama cha CCM.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Celina Kaluba mwishoni mwa wiki iliyopita alisema kuwa, Kasangani alitoa malalamiko hayo septemba 8 mwaka huu, baada ya kupokea ujumbe wa simu toka kwa viongozi kata ya Mungaa akiwemo katibu Tarafa hiyo William Swai.
Kaluba alisema, Kasangani aliwaeleza polisi kuwa, katika kijiji cha Makiungu kuna fujo zilizopelekea kuchanwa kwa mabango ya picha za mgombea wao wa ubunge Jonathan Njau, ambayo yalikuwa yamebandikwa kwenye moja ya kuta za nyumba.
Alisema,polisi walifika Makiungu na kuonyeshwa watoto wanaodaiwa kuchana mabango ambapo waliwachukua hadi Singida mjini,kabla ya kuwaachia huru kesho yake kutokana na watoto hao kushindwa kuwatambua watu waliowashawishi kung’oa mabango.
Aliwataja watoto hao kuwa ni Costantine Clement (12) na Justine Isdori (7) wote wanafunzi wa shule ya msingi Muyanji, pia Pascal Faustine (6) anayesoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Makiungu; wote katika kata ya Mungaa.
Alisema baada ya mahojiano hayo, watoto hao walidai kuwa walitumwa na watu wa CHADEMA kuuyang’oa mabango hayo.
Katika hatua nyingine, Kaluba alisema kuwa tukio kama hilo pia limetokea Ikungi ambapo mabango ya mgombea huyo yaliyobandikwa kwenye nyumba ya kulala wageni Hande, yaling’olewa na mmoja wa wapangaji;Hakuna anyeshikiliwa kwa tukio hilo.
Kufuatia tukio hilo, Kaluba ametahadharisha viongozi, wanachama na wapambe wa vyama vya siasa vilivyosimamisha wagombea wao wa udiwani na ubunge, kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu za kampeni ili kuepuka vurugu.
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AINGIA KOROGWE KIKAMPENI ZAIDI…!!!Posted by Blog Team on September 13th, 2010
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Majimarefu Mgombea ubunge Korogwe vijijini kwa tiketi ya CCM wakati aliposimama katika kijiji cha Mashewa Korogwe vijijini leo asubuhi.
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwahutubioa wakazi wa kata ya Mashewa wilayani Korogwe vijijini leo.
Aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Kerege Bwana Mjata Mohamed akirudisha kadi za wananchama waliokihama chama hicho na kuhamia CCM wakati Mgombea Urais wa CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete aliposimama kuwasalimia wananchi kijijini hapo leo asuhuhi.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimsabahi Bi Halima Abdallah mwenye umri wa miaka mia moja na mbili (102) wakati aliposimama kuwasalimia wananchi katika kata ya Kerege wilaya ya Korogwe vijijini leo asubuhi.(Picha na Freddy Maro)
MAMA SALMA KIKWETE KATIKA ZIARA MKOANI MARA…!!!Posted by Blog Team on September 13th, 2010
Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake (WAMA) Mama Salma Kikwete (kati) akisalimiana na Wanachama wa UWT Mkoa wa Mara jana,pindi alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma . Mama Salma Kikwete yupo mkoani hapo kwa ajili ya kukutana na wanachama wa UWT katika mikutano ya ndani kuhusu kuwahamasisha umuhimu wa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu Ujao mwaka huu.(kulia) Mwenyekiti wa UWT mkoa Mara Nancy Sessani.
Katibu wa UWT Mkoa wa Mara,Helena Chacha (aliesima shoto) akimkaribisha Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (hayupo pichani)alipowasili mkoani Mara jana kwa ajili ya kufanya mikutano ya ndani na kuzungumza na wanachama wa UWT kuhusu umuhimu wa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Kikundi cha wakiana mama Musoma Mjini wakimshangilia Mama Salma Kikwete alipowasili katika uwanaja wa ndege wa Musoma.(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
No comments:
Post a Comment