Wednesday, October 6, 2010

MAPOKEZI YA DK. BILAL BAGAMOYO JANA…!!!


Msafafa wa waendesha Pikipiki ukimpokea Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwasili Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani  jana Okt 4 kwa ajili ya kufanya mkutano wa  uliofanyika katika Uwanja  wa Shule ya Msingi Majengo  Kata ya Magomeni.

Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM  Dk. Mohamed Gharib Bilal na mkewe Asha Bilal, wakiingia kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo jana Okt 4, kufanya mkutano wa kampeni.

Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya Kikundi cha Sanaa cha Sprendid cha Bagamoyo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Majengo Kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo jana Okt 4, alipofika kufanya mkutano wa kampeni n kuanadi wagombea ubunge Shukuru Kawambwa waJimbo la  Bagamoyomo na Amour Abuu Jumaa wa Jimbo la Kibaha Vijijini.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Sprendid cha Bagamoyo, wakitoa burudani wakati wa mkutano wa kampeni  wa mgombea mwenza wa urais wa CCM Dk. Mohamed Gharib Bilal, uliofanyika jana Okt 4 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo.

Dk. Bilal, akifurahia staili ya msanii wa kikundi cha Sanaa cha Sprendid wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Kata ya Magomeni.
Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Sauda Mpambaliyoto, akisakata ngoma na msanii wa kikundi cha Sprendid wakati wa hafla ya mkutano huo jana Okt 4.

Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM  Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa  Kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo jana Okt 4, wakati wa  mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Majengo.

Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM  Dk. Mohamed Gharib Bilal akimnadi mgombea ubungea wa Jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika  kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo jana.
Filed under: Politics | No Comments

DK MOHAMED GHARIB BILAL AILIPUA KAMBI YA CUF…!!!


Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza wakatei alipowa fanya mkutano na kuzungumza na wazee Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani jana Okt 4 kabla ya kuondoka Kisiwani humo kuelekea Bagamoyo kuendelea na ziara yake ya mikutano ya kampeni.
************
Na.Mwandishi wetu.
Mgombea mwenza wa mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, amewataka  wananchi wa Wilaya ya Mafia, kuwa makini dhidi ya viongozi wa CUF kwa kuwa chama hicho kimejaa viongozi waongo na wasiotaka Tanzania ipate maendeleo.
Kauli hiyo  ya Dk Bilal inakuja  baada ya mgombea Urais kwa  tiketi ya CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, kufanya mikutano yake ya kampeni kisiwani hapa na kudai kuwa ujenzi wa uwanja wa ndege, gati na barabara ni geresha tu ya CCM na kwamba wananchi wawachague wao kwa kuwa ndio wanaofahamu umuhimu wa maendeleo.
Akizungumza katika kikao cha  wazee wa mji wa Mafia, Dk Bilal alisema  CUF hawastahili kukabidhiwa serikali kwa kuwa hawana uwezo na hata pale walipokabidhiwa nafasi hawakuitumia vizuri zaidi ya kuwaumiza wananchi wanaoishi katika kata wanazoongoza zikiwemo za Mafia.
Mapema, mgombea mwenza huyo alikabidhiwa ripoti kuhusu uongozi wa Kata ya Jibondo inayoongozwa na CUF, na ripoti hiyo ilisema miradi mbalimbali ya maendeleo imesimama  yakiwa ni matokeo ya misimamo ya uongozi wa CUF.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule na ile ya maji hali, inayowafanya wananchi kubaki nyuma kimaendeleo.
Wazee wa wilaya ya Mafia wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipofika kufanyanao mazungumzo jana Okt 4
Filed under: Politics | No Comments

DK SLAA AMPA 5 MWAKYEMBE LAKINI MHH….!!!

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa  hakusita kuonyesha hisia zake kwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kyela kwa tiketi ya CCM, Dk Harrison Mwakyembe  alipowataka wananchi kumchagua aendelee kuwawakilisha.Dk Slaa, ambaye pamoja na Mwakyembe walijulikana kama vinara wa upambanaji dhidi ya ufisadi katika Bunge la Tisa, alisema hayo hali akijua kuwa Chadema ina mgombea kwenye jimbo hilo anayeitwa Eddo Mwamalala.
Lakini uamuzi wake wa kumpigia debe Dk Mwakyembe uliambatana na masharti matatu, moja likiwa gumu kutekelezwa na mteule huyo wa CCM katika mkakati wake wa kurejea kwenye chombo hicho cha kutunga sheria.
“Sharti la kwanza, Dk Mwakyembe atatakiwa kutompigia kampeni (mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya) Kikwete,” alisema Dk Slaa kwenye mkutano uliofanyika Uwanja wa Mwakangale na kuhudhuriwa na watu wengi kiasi.
“Dk Mwakyembe ni rafiki yangu wa damu, kama kweli unautaka ubunge wa hapa, lazima asimpigie kampeni mgombea urais wa CCM na badala yake uninadi mimi ili niweze kuikomboa nchi hii.”
Mbunge huyo wa zamani wa Karatu alitaja sharti la pili kuwa ni kuweka maslahi ya wananchi mbele badala ya kuweka mbele maslahi ya CCM.
Dk Slaa alitaja sharti la tatu kuwa ni Mwakyembe kuacha kile alichokiita unafiki wa CCM wa kujigamba kwamba chama hicho kimefanya mambo mengi wakati hakuna lolote.
Chadema imesimamisha mgombea Mwamalala, lakini inaonekana wananchi wengi wa Kyela bado wanamtaka Dk Mwakyembe aendelee.
“Huu ni mkataba tumewekeana leo, kama Dk Mwakyembe anautaka ubunge asikiuke kwani akifanya hivyo tu, mpigieni kura mgombea wa Chadema,” alisema Dk Slaa ambaye alisema hana ugomvi na Dk Mwakyembe.
Filed under: Politics | No Comments

Dk. BILAL AFUTA YA LIPUMBA KISIWA CHA MAFIA…!!!



Mgombea Mwenza wa Urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiagana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafia, Abdulkarim Shah, mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kilindoni Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani leo jioni, ikiwa ni pamoja na kumnadi mgombea huyo na Madiwani wa Kata za kisiwa hicho.
Filed under: Politics | No Comments

JK AWALIPUA WAPINZANI KWA MARA NYINGINE TENA…!!!

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete amewashukia wanasiasa wa vyama vya upinzani, na kuwataka Watanzania wawapuuze kwa sababu ni waongo na wamechanganyikiwa.
Aidha, amewapokea wanachama zaidi ya 50 wa vyama vya upinzani mkoani Singida waliorejea CCM, wakiwemo wanachama 41 waliokuwa Chadema.
Kwa upande mwingine, aliyekuwa mgombea katika kura za maoni za uteuzi wa wagombea ndani ya CCM Jimbo la Singida Magharibi ambaye alihamia Chadema baada ya kutopitishwa kuwania jimbo hilo, amesema chama hicho cha upinzani hakina sera na siku 29 alizokaa huko, zilijaa mateso makubwa na upweke.
Katika mikutano yake miwili kwenye majimbo ya Iramba Magharibi uliofanyika mjini Puma na Iramba Mashariki katika mji wa Ikungi , Rais Kikwete aliwataka Watanzania wawapuuze wapinzani kwa sababu ya uongo.
“Kwa nini hamuwaambii ukweli, wanadanganya mchana kweupeee… wapuuzeni, ni waongo, wamechanganyikiwa,” alisema, na kuongeza kuwa Watanzania watawathibitishia kuwa ni waongo itakapofika Oktoba 31, mwaka huu; siku ya kupiga kura.
Alisema wapinzani ni waongo kwa sababu wamekataa kuona maendeleo yaliyofanyika Tanzania tangu Uhuru, wakidai hakuna lolote la maendeleo CCM ililolifanya.
“Mtu anawadanganya, anawafanya watoto wadogo…hivi hii barabara tuliyojenga (Dodoma-Manyoni-Singida) haioni? Zamani ilikuwepo? Ni bora angesema yeye atajenga barabara ya lami juu na magari yatapita huko,” alieleza.
Filed under: Politics | No Comments

KUELEKEA OKTOBA 31 WANAFUNZI WA CHADEMA WAJA JUU…..!!!!

WANAFUNZI hao  wa elimu ya juu ambao ni wafuasi  wa Chama Cha CHADEMA wameitaka serikali kufungua vyuo hivyo kabla ya siku maalumu ya kupiga kura la sivyo watahamasisha wananchi kupiga kura ya mabadiliko hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya wahitimu na wanafunzi wa elimu ya juu ya Chadema, Richard Manyanga, na kwa upande wapili  chama hicho pia kimesema kitawatumia wanafunzi hao kulinda kura za wagombea wake.
Mwenyekiti huyo alidai sababu ya kutoa kauli hiyo ni kutokana na  hofu yao kwamba wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 60,000 watakosa haki ya kupiga kura ikiwa vyuo vitafunguliwa baada ya uchaguzi mkuu.
“Vyuo vingi vilitumika kama vituo vya kujiandikishia wanafunzi wakati wa uboreshaji wa daftari la kupiga kura  na fedha nyingi ilitumika kwa ajili ya kazi hiyo, sasa vyuo vikifunguliwa baada ya uchaguzi, haki ya wanafunzi kupiga kura haitoonekana, tunaiomba serikali isikie mwito wa kufungua vyuo kabla ya uchaguzi”.
Alisema, anaamini kuwa vyuo havijakosa fedha za uendeshaji hadi wasogeze muda wa kufungua mpaka baada ya uchaguzi na kuwataka wanafunzi wa vyuo hivyo popote walipo kutafuta kura zaidi ya moja na iwe kura ya mabadiliko.
Manyanga alisema, katika kura hiyo ya mabadiliko, kila mwanafunzi anatakiwa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi na kuwahamasisha kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa na vya upinzani ni kwa ajili yao ili wapige kura katika vyama vinavyolenga kuwakomboa wao.
Filed under: Politics | No Comments

DK. BILAL AUNGURUMA KISIWA CHA MAFIA LEO..!!!


Mgombe Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Mafia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Kilindoni Mkoa wa Pwani Visiwani humo leo Okt 3.

Wananchi Wilaya ya Mafia eneo la Kilindoni Mkoa wa Pwani  wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Visiwani humo leo Okt 3.
Filed under: Politics | No Comments

ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE MKOANI KAGERA…!!!


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiendelea na zaiara yake Mkoani Kagera, kuhamasisha wanachama wa UWT pamoja na wakinamama wakereketwa kuhusu umuhimu wa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Uchaguzi Mkuu,Oktoba 31,mwaka huu.Upigaji kura ni haki kwa mwananchi wote wa Tanzania Pichani anaonekana akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Nkenge Bukoba Vijijini Mama Assumpta Mshana.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwanadi wagombea udwani ,viti maalumu na mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba Mjini Khamis Kagasheki.
Kikundi cha watoto wa shule ya awali ya Kitobo Misenyi Bukoba vijijini wakimkaribisha Mke wa Rais Mama SALMA Kikwete.
Palikuwa hapatoshi Bukoba vijijini kwani ngoma ya asili ya Kihaya ilikuwepo na ikatumbuizwa katika mkutano huo.
Wanawake wa jimbo la Bukoba Vijijini wakimsikiliza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete 2-10-2010.


Filed under: Politics | No Comments

DR SLAA APOKELEWA KWA KISHINDO JIMBO LA IRINGA MJINI..!!!


Mgombea urais kupitia Chadema Dr Willibrod Slaa akishangaa umati mkubwa wa wakazi wa jimbo la Iringa mjini ambao wamefika katika uwanja wa Mwembetogwa Iringa mjini kumsikiliza katika muendelezo wake wa mikutano ya kampeni za chama hicho.

Wananchi wa Iringa mjini wakirekodi hotuba ya Dr Slaa kwa kumbukumbu zao.

Ulikuwepo ulinzi wa kutosha uwanja wa Mwembetogwa Iringa.

Umati wa wananchi wa jimbo la Iringa mjini waliojitokeza katika uwanja wa Mwembetogwa mapema jana kumsikiliza Dr.Slaa kwenye moja ya mikutano ya kampeni zake mjini humo.

Wananchi wakitazama Helkopta ya Dr Slaa ikitua katika uwanja wa Mwembetogwa tayari kwa kuanza mkutano wake wa kampeni mjini Iringa mapema jana. Picha kwa hisani ya Francis Godwin
Filed under: Politics | No Comments

SIKUJUA KAMA JOSEPHINE AMESHAKUWA BOOKED – DK . SLAA..!!!

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk. Willibrod Slaa, amewasilisha Mahakama Kuu maelezo ya utetezi wa tuhuma zinazomkabili za kupora mke wa mtu aliyemtambulisha mara kadhaa katika majukwaa ya siasa kuwa mchumba wake, Josephine Mushumbusi, akidai kuwa hakujua kuwa ni mke wa mtu.
Aidha, Dk. Slaa amekataa kumlipa fidia ya Sh bilioni moja mdai wake, Aminiel Mahimbo, aliyeiomba Mahakama hiyo imtake amlipe kwa hasara aliyoipata kwa kuporwa mke. Habari za Josephine kuwa mke wa mtu nilizikia kutoka katika vyombo vya habari na hakuwahi kunidokeza yakuwa aliwahi kuolewa alidai Dk Slaa.
Dk. Slaa anaiomba Mahakama iitupe kesi hiyo kwani haina msingi wowote kwa sababu mdai mwenyewe alijidhalilisha kwa kukubali kutumiwa na chama cha siasa (hakukitaja) kutoa habari hizo kwenye vyombo vya habari na kukubali kuhamia nyumbani kwa mwanamke ambaye ni kiongozi wa chama hicho..
Filed under: Politics | No Comments

DK, BILAL AFURAHIA NGOMA YA WAFIPA…!!!



Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya utamaduni yaKizuite ya kabila la Wafipa, wakati wa mapokezi yake alipowasili kwenye uwanja wa Kijiji cha Mtimbwa Kata ya Kasense Wilaya ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa, kufanya mkutano wa kampeni,Sept 30.

Wasanii wa Kikundi cha Ngoma ya Utamaduni cha Kanondo, wakionyesha umahiri wao wa kecheza ngoma hiyo mbele ya Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, baada ya kuwasili Kijiji cha Mtimbwa Kata ya Kasense Wilaya ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa kufanya mkutano wa kampeni Sept 30.

Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Sumbawanga mjiji, Aesh Khalfan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Spet 30 kwenye Kijiji cha Mtimbwa Kata ya Kasense Wilaya ya Kasense.

Wananchi wa Kijiji cha Mtimbwa Kata ya Sense Wilaya ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa, wakishangilia kwa pamoja wakati mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni Sept 30.
Filed under: Politics | No Comments

WANANCHI WA MIOMBO WAZUIA MSAFARA WA DK. BILAL..!!!


Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Miombo Wilaya ya Nkasi baada ya kusimama kijijini hapo jana Sept 30 wakati wananchi hao waliposimama barabarani wakiutaka msafara kusimama eneo hilo ili wananchi waweze kumuona Dk. Bilal na kuzungumza nae, akiwa njiani kuelekea Kijiji cha Mtenga.

Mgombea Mwenza wa urais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Nkasi Kusini, Ally Kessy, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Kijiji cha Mtenga jana Sept 30.

Baadhi ya wanachama waliokuwa wanachama wa Vyama pinzani, wakila kiapo baada ya kukabidhi kadi za vyama vyao kwa Mgombea Mwenza wa urais wa CCM Dk. Mohamed Gharib Bilal na kukabidhiwa kadi mpya za Chama cha Mapinduzi CCM, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Kijiji cha Majalila Kata ya Mpanda Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Lukwa jana Sept 30.

Wananchi wa Kijiji cha Majalila wakinyoosha mikono juu kuashiria kula kiapo kuendelea kukitumikia chama cha Mapinduzi CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana Sept 30.

Mgombea Mwenza wa Uras wa CCM, Dk Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na mkazi wa kijiji cha Majalila baada ya kumaliza mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho jana sept 30.
Filed under: Politics | No Comments

CCM WATASHINDA – AUGUSTINE MREMA…!!!


Na. MO BLOG TEAM
MGOMBEA ubunge katika jimbo la Vunjo kwa tiketi ya Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, amekiri kuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Crispin Meela, atashinda kutokana na propaganda chafu zinazotolewa dhidi yake, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) zikilenga kummaliza kisiasa.
Mrema alisema hayo jana, kwenye uwanja wa Polisi uliopo mji mdogo wa Himo, mkoani Kilimanjaro wakati akihutubia mkutano wa kampeni za chama hicho, na kusindikizwa na mgombea urais wa chama hicho, Mutamwega Mgahywa.
Alisema, Chadema haijalenga kushinda katika jimbo hilo, bali imejikita kuhakikisha TLP (Mrema) haishindi, jambo linalotoa ushindi rahisi kwa mgombea wa CCM.
Mwanasiasa huyo mkongwe alisema, Chadema imekuwa ikimsakama kwa kila hali, ikidai kuwa hafai kuchaguliwa na kwamba ni mzee asiyefaa kuliongoza jimbo la Vunjo
Filed under: Politics | No Comments

KAMPENI ZA JK KATIKA MJI WA UWOYA WILAYANI URAMBO…!!!


Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapindzi CCM Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mkutano wa kampeni katika mji wa Uyowa Wilayani Urambo leo tarehe 30.09.2010, Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyiaka Oktoba 31 mwaka huu nchini kote.

Umati mkubwa wa watu wakimshangilia Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiingia Uyowa, Ulyankulu Wilayani Urambo.

No comments:

Post a Comment