DK. BILAL ASEMA NA WALIMU WA ILEJE…!!!Posted by Blog Team on September 30th, 2010
Mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal na mkewe Zakia Bilal, wakipokelewa mpakani mwa Mkoa wa Mbeya na Rukwa, baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Mkutano Mkoa wa Rukwa jana mchana Sept 29.
Mgombea Mwenza wa Urasi wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ileje, Aliko Kibona, wakati alipofika katika jimbo hilo jana Sept 29 kufanya mkutano wa kampeni.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya walimu wa Wilaya ya Ileje, baada ya kuwasili walayani humo jana Sept 29 kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Aliko Kibona.
Baadhi ya walimu wa shule za msingi wa Wilaya ya Ileje Mkoa wa Mbeya, wakiwa na mabango yenye ujumbe kuhusu kushiriki kwao katika uchaguzi ujao, wakati wa mapokezi ya Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwasili Wilayani humo jana Sept 29 kufanya mkutano wa kampeni.
Filed under: Politics | No Comments
JK NA AHADI ZA CHUO KIKUU SHINYANGA…!!!Posted by Blog Team on September 30th, 2010
Hiyo ni ahadi ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, aliyoitoa juzi baada ya kuombwa na wakazi wa wilaya za Bukombe na Kahama, kwenye mikutano ya kampeni.
Akiwa Bukombe, mgombea ubunge, Emmanuel Luhahula, aliomba chuo kikuu mkoani humo kwa sababu hawana chuo kama hicho.
Naye mgombea ubunge wa Kahama James Lembeli, aliomba chuo kikuu hicho ili kusaidia vijana wa mkoa huu.
Mbunge wa zamani wa Msalala, Ezekiel Maige ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, aliomba kujengwa chuo cha ufundi ili kutoa fursa kwa vijana wa Kahama kupata ajira ikiwamo migodini.
Akizungumza na wananchi wa Kahama kwenye uwanja wa michezo mjini humo, Kikwete , alisema ujenzi wa chuo kikuu ni lazima, lakini kwanza amalize vya Dodoma na Butiama.
“Ngoja tulitafakari vizuri, lakini ni lazima tujenge. Kwa sasa tunakamilisha Dodoma na kisha Butiama kwa heshima ya Mwalimu Nyerere … baada ya hapo, tutaliangalia hili,” alisema.
Akizungumzia tatizo la maji, alisema Kahama kwa sasa haina matatizo hayo baada ya kupata maji ya Ziwa Victoria, isipokuwa vijiji 15 vilivyopo kilometa 15 kutoka mradi huo, vitapewa maji na tayari zimetengwa Sh bilioni 12.9 kufanikisha kazi hiyo.
Kuhusu barabara za mjini hapa, aliagiza zijengwe haraka kwa sababu fedha zimetolewa na kuwataka viongozi wa Serikali wanaogombana juu ya kujengwa kwa barabara hizo, kumaliza tofauti zao haraka.
Filed under: Politics | No Comments
DK. BILAL AENDELEA KUUNGURUMA MJINI MBEYA…!!!Posted by Blog Team on September 29th, 2010
Dk.Bilal, akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Mbeya mjini jana katika eneo la Kibondenyasi.
Wananchi wa Kata ya Nsalaga Kibondenyasi, wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kukinadi chama cha Mapionduzi, wakati wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akifanya mkutano wa kampeni eneo hilo Mkoani Mbeya jana Sept 28.
Filed under: Politics | No Comments
WABUNGE CHADEMA VITI MAALUM-VIGEZO VILIVYOTUMIKA HIVI HAPA…!!!Posted by Blog Team on September 29th, 2010
Na.MO BLOG TEAM
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa chama hicho kilitumia vigezo sita kupata majina 105 kati ya 147 ya watu waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa Dk Slaa vigezo hivyo ni elimu, uzoefu wa uongozi wa siasa, uzoefu wa uongozi nje ya siasa, mchango wa hali na mali katika operesheni za chama na kampeni zinazoendelea pamoja na umri wa mgombea katika chama.
Alisema vigezo vyote hivyo vilikuwa na jumla ya alama 50, huku elimu ikiwa na alama 10, uzoefu wa uongozi wa siasa, alama 10, uzoefu wa uongozi nje ya siasa, alama tano, mchango wa hali na mali katika operesheni za chama na kampeni zinazoendelea alama alama 10, huku umri katika chama ukiwa na alama tano.
Dk Slaa alibainisha kuwa licha ya majina hayo kupitishwa, chama hicho hakitayaweka bayana kutokana na kuhofia kuvuruga hali katika kampeni zinazoendelea.
Alisema baada ya kupatikana kwa majina hayo, kamati kuu ya chama hicho, imeiagiza sekretarieti yake kuhakikisha inayapeleka majina hayo Tume ya Uchaguzi (Nec ), kabla ya Septemba 30 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya vigezo hivyo vya uteuzi wa wabunge iliyotolewa jana na Dk Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa mwenyekiti wa uteuzi huo, mgombea yeyote ambaye amewahi kushika wadhifa wa ubunge aliwekewa alama 10 ambacho ni kigezo kimojawapo kati ya sita.
Kwa mujibu wa karatasi inayoonyesha alama za wagombea na kuficha majina yao, alama 10 kwenye kigezo cha mgombea aliyewahi kuwa mbunge zipo sita, hivyo kumaanisha kuwa waliopata kuwa wabunge wote wamepewa nafasi za mwanzo.
Nafasi zilizowekewa alama 10 katika kigezo hicho ni nambari moja, mbili, tano, saba, nane na nambari tisa. Kwa mantiki hiyo waliokuwa wabunge katika bunge lililopita ambao ni Suzane Lyimo, Halima Mdee, Lucy Owenya, Grace Kiwelu, Mhonga Ruhwanya na Anna Komu watarejea kwenye chombo hicho cha kutunga sheria kwa tiketi ya Chadema.
Kigezo kingine ambacho kinadhihirisha ushindi wa wabunge hao ni pamoja na kile cha elimu. Kwa mujibu wa vigezo hivyo, wanawake watatu kati yao wanaonyesha kuwa na elimu ya shahada za uzamili alama zao zikionyesha nane, mmoja akiwa na alama sita ikimaanisha shahada ya kwanza na wawili wakiwa na elimu ya kidato cha nne au astashahada wenye alama mbili.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo katika tovuti ya Bunge, Lyimo ana shahada ya uzamili, Halima Mdee anayo shahada ya uzamili, Lucy Owenya ana shahada ya uzamili ya uongozi wa biashara, Grace Kiwelu ana elimu ya astashahada, Mhonga Ruhwanya ana shahada ya kwanza na Anna Komu ana elimu ya stashahada.
Kuhusu uamuzi wa kuficha majina hayo, Dk Slaa alisema hofu yao pia inatokana na baadhi ya wagombea wa viti maalum pia kuamua kupambana kwenye majimbo. Wanawake waliokuwa wabunge wa viti maalum kutoka karibu vyamna vyote, mwaka huu waliamua kupambana kwenye majimbo badala ya utamaduni wa kusubiri nafasi za upendeleo maalum.
“Tukitoa majina na kusema kuwa Mdee (Halima Mdee) ameshinda, wananchi watasema sasa kuna sababu gani za kumpigia kura wakati ameshakuwa mbunge tayari,” alifafanua.
Filed under: Politics | No Comments
DK. BILAL AUNGURUMA MKOANI MBEYA..!!!Posted by Blog Team on September 28th, 2010
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa CCM wa Kijiji cha Chimala Isitu, wakati alipowasili kwenye eneo la Stendi ya zamani ya mabasi ya Chimala, Wilaya ya Mbalali Mkoa wa Mbeya kufanya mkutano wa kampeni leo Sept 28.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilala, akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbalali, Modestus Kilufi, wakati alipokuwa akifanya mkutano wa kampeni kwenye eneo la Stendi ya zamani ya Mabasi Wilaya ya MbalaIali leo Spt 28.
Wananchi wa Kijiji cha Chimala Wilaya ya Mbalali Mkoani Mbeya, wamsikiliza Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akifanya mkutano wa kampeni katika kijiji hicho.
Wananchi wa Kijiji cha Chimala Wilaya ya Mbalali Mkoani Mbeya, wakishangilia wakati Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akifanya mkutano wa kampeni katika kijiji hicho.
Mgombea Mwenza wa urais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Jeras Fungo, ambaye ni mlemavu wa miguu Mkazi wa Kijiji cha Ihai, Kata mpya ya Ihai, aliyefika katika mkutano wa kampeni kijiji cha Chimala, baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika katika eneo la Stendi ya zamani ya Mabasi Wilaya ya Mbalali Mkoani Mbeya leo Sept 28.
Dk. Bilal, akimvisha Skafu ya CCM, Jeras Fungo, mkazi wa Kijiji cha Ihai ambaye ni mlemavu wa miguu, baada ya kumaliza mkutano wa kampeni leo Sept 28.
Filed under: Politics | No Comments
MO AKIWA KATIKA MCHAKATO WA KAMPENI…!!!Posted by Blog Team on September 27th, 2010
MO akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa kampeni kata ya Mandewa jana huku akilindwa na bodigadi mwanamke.
Mo akimnadi mgombea udiwani kata ya Mandewa Bw,Shabani Omary Kiranga.
MO akiomba kura kwa mlemavu wa miguu Hamis Issa aliyefika kwenye mkutano wa kampeni katika Kitongoji cha Ng’aida kijiji cha kisaki alipofika kuomba kura kwa wananchi kukichagua Chama cha Mapinduzi.
Baada ya kutoka katika mkutano wa kampeni huko Kisasida jana MO njiani alikutana na mama mmoja akiteka maji kwenye kisima ambacho akiwa kama mbunge alichangia kukichimba.
LOWASA ANGIA KATIKA MPAMBANO….!!!Posted by Blog Team on September 27th, 2010
Mgombea wa ubunge wa jimbo la Monduli[CCM],Edward Lowassa akiingia katika mji mdogo wa Mto wa Mbu tayari kuanza mkutano wa kuzindua kampeni zake.
*****************
MGOMBEA wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Monduli kupitia tiketi ya CCM, Edward Lowassa, jana alikata utepe rasmi kuashiria ufunguzi wa kampeni zake huku akiwa na kauli mbiu isemayo ‘tulifurahi pamoja, tukahuzunika pamoja, tutasonga mbele pamoja na tutashinda.’Kaulimbiu hiyo, inalenga katika kuzungumzia tukio lililomfanya alijiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu
Akiwahutubia umati wa watu waliofurika katika mji wa mto wa mbu , Lowassa alisema katika kipindi chake cha ubunge,amejitahidi kutekeleza kwa asilimia 99 ilani ya chama chake.Kinachofuata sasa ni kutekeleza na kubuni miradi mingine mipya kwa upande wa afya,maji na elimu.
“Kama mlivyomuahidi Rais, naomba katika uchaguzi huu tuvunje rekodi ili jimbo letu liongoze kwa kumpigia kura nyingi,”alisema Lowassa. Huku akishangiliwa kwa nguvu zote Mbali na mipango ya kuboresha sekta ya maji elimu na afya pia mgombea huyo aligusia swala la mikopo kwa wafugaji na vijana.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole, aliwataka wale wote wanaowania viti vya udiwani na ubunge katika Mkoa wa Arusha, kushughulikia kero za wananchi kama watachaguliwa.
Filed under: Politics | No Comments
DK. BILAL AZINDUA SHINA LA WAKEREKETWA-KANYIGO…!!!Posted by Blog Team on September 26th, 2010
Mgombea Mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCMm Dk. Mohamed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Shina la wakereketwa lililojengwa katika Ofisi ya kwanza ya iliykuwa TANU na baadaye CCM iliyoanzishwa 1955i, katika kijiji cha Ruzinga Wilaya ya Misenyi mkoaa wa Kagera, wakati alipofika kijijini hapo jana kufanya mkutano wa kampeni.
Mgombea Mwenza wa Urais Kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Mbuzi Rashid Malinzi, mtoto wa Marehemu Rashid Mbakilek, aliyekuwa mmoja kati ya waasisi wa Tano 1955, mara baada ya Dk. Bilal kuzindua shina la wakereketwa katika Kijiji hicho cha Ruzinga-Kanyigo, jana mchana.
Filed under: Politics | No Comments
DK. BILAL NJIANI KUELEKEA IRINGA…!!!Posted by Blog Team on September 26th, 2010
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Fufu Wilaya ya Mpwapwa leo Sept 26, wakati akiwa njiani kuelekea Mkoani Iringa.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiondoka kwenye eneo la mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Kijiji cha Fufu Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma leo Sept 26, wakati akiwa njiani kuelekea Mkoani Iringa.
Filed under: Politics | No Comments
ELIMU ITATOLEWA BURE – CUF…..!!!!Posted by Blog Team on September 25th, 2010
Na.MO BLOG TEAM.
Ilikuondoa tabaka la walionacho na wasionacho hatuna budi ni lazima elimu kuanzia ngazi ya msingi hadi chuo ikatolewa bure. Kwa kuona umuhimu huo cha hicho kimesema kitatoa kipaumbele katika swala hilo pale tu itakapo ingia madarakni. Naibu mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho Shaweji Mketo alisema hayo juzi jijini Dar es salaam katika kipindi cha tv kijulikanacho kama Uchaguzi kupitia TBC1.
Alisema nafasi hiyo ya kupata elimu bure itakuwa ni kwa watoto wa kitanzania iliwapate haki yao ya msingi na kuepusha jamii dhidi ya kisingizio cha umasikini ndio kuwa chanzo kikuu cha ujinga. Akipinga sera ya sasa ya serikali alisema” Serikali incho kifanya ni kama inawakusanya watoto kwenye vituo ili iwaangalie namna wanavyokuwa toka utotoni hadi kuwa vijana kasha wawarudishe kwa wazazi wao”
Aliongeza” endapo wananchi wataipa mamlaka CUF ya kuongeza nchi badala ya kujenga shule katika kila kata wao wateja shule tano za sekondari katika kila wilaya”
Filed under: Politics | No Comments
MIAKA MITANO SINGIDA IMEPAA KIMICHEZO, KINDAI YABEBA KOMBE LA TAIFA..!!Posted by Blog Team on September 25th, 2010
Mgombea Ubunge jimbo la singida mjini CCM (MO) akizungumzia jinsi ambavyo amesaidia sekta ya michezo katika kuteleleza ilani ya chama chake katika kipindi cha miaka mitano ya Ubunge katika jimbo hilo.
***************
Na Hillary Shoo,Singida.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO) amesema kuwa alitumia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 35 kwa ajili ya kuendeleza sekta ya michezo katika Mkoa wa Singida katika kipindi cha miaka saba iliyopita.
Dewji aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Unyambwa.
Alisema katika kipindi hicho, alianzisha mashindano ya kuibua vipaji vya vijana wa kata zote 13 za Manispaa ya Singida ambayo yalijulikana kwa jina la ‘kombe la Mohammed Dewji’ MO CUP
Mgombea huyo alisema fedha hizo zilitumika kwa ajili ya kununulia vifaa mbalimbali vya mchezo wa soka ikiwemo mipira na zawadi za washindi.
“Mshindano hayo yaliibua vijana wenye vipaji ambao wamechangia kuuletea mkoa wa Singida heshima ya kunyakua ubingwa wa kombe la taifa mwaka huu.Huo ni ubingwa wa kwanza kwa mashindano ya kombe hilo, kwa mkoa wa Singida toka nchi hii ipate uhuru.”Alisema Mo.
Alisema wachezaji wengi waliounda timu ya mkoa wa Singida Kindai Shooting Star, walitokana na mashindano yake ya kombe la Mohammed Dewji Cup.
Aidha,Dewji alisema mashindano ya kombe la Mohammed Dewji, yamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni yale ya vijana wa kiume na pia yapo kwa ajili ya vijana wa kike kuonyesha vipaji vyao kwenye mchezo wa soka.
“Endapo wananchi watanipa ridhaa tena ya kuwa mbunge wao katika kipindi cha tatu, mashindano haya nitayaboresha zaidi kadri uwezo utakavyoniruhusu”alisema mgombea huyo.
MO akimnadi mgombea udiwani kata ya Mwankoko Hamis Nkulungu kwa wananchi.
Wananchi wakimpa mikono mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Mwankoko.
Wanafunzi pamoja na wananchi waliofika kwenye mkutano wa kampeni shule ya msingi Mwankoko.
Wengine alisalimiana nao njiani huku wakimpa mikono ya heri wakati akirejea kutoka Kata ya Mwankoko(Picha zote na Jofrey Mwakibete).
KIKWETE APIGA BOMU KWA VYAMA PINZANI…..!!!!Posted by Blog Team on September 25th, 2010
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Rais Jakaya mrisho Kikwete akiwahutubia maelfu ya wanachama wa CCM mjini Tarime jana jioni.
***********************
Na.Mwandishi wetu.
MGOMBEA urais kwa tiketi ya kupitia CCM, Jakaya Kikwete jana alivipiga kombora vyama vinavyoshindana kuwania kushika madaraka, akivifananisha fotokopi na kuwataka wananchi kuviepuka.
Kikwete pia hakuacha kugusia swala la vita vya mara kwa mara vya koo, kuachana na chuki za kikabila akisema zinahatarisha amani ya nchi aliyasema hayo katika Uwanja wa Sabasaba mjini Tarime. Alisema chama chake kinastahili kupigiwa kura kwa vile kimedumisha amani na utulivu nchini.
“Msihangaike na vyama vya upizani ambavyo ni sawa na ‘photo copy’ wakati CCM ipo kuwaletea aendeleo,” alisema Kikwete akirejea kauli yake aliyoitoa Agosti 20 wakati akizindua kampeni za CCM kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.
Kuhusu vurugu zinazosababishwa na ukabila, Kikwete alisema suala hilo linachangia kuvunjika kwa amani miongoni mwa wana jamii.
“Angalieni kwa wenzenu hapo jirani, maana nyie mpo jirani zaidi mkivuka mpaka mnaingia kwa wenzenu.
“Angalieni kwa wenzenu hapo jirani, maana nyie mpo jirani zaidi mkivuka mpaka mnaingia kwa wenzenu.
Wameumizana sana kutokana na ukabila,” alisema akimaanisha nchi jirani ya Kenya ambayo ilikumbwa na mapigano mwaka 2007 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais.
Huku akishangiliwa na umati uliohudhuria mkutano huo, Kikwete alisema serikali itapambana kikamilifu na wezi wa mifugo na haitachoka, na zaidi wataliwezesha zaidi Jeshi la Polisi mkoani humo kupambana na wahalifu hao.
Alisema sekta ya elimu imeimarishwa kwa kuwa awali kulikuwa na shule 10, lakini sasa kuna shule 28 na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaofaulu kutoka 4,925 hadi 18,250.
JK aliahidi kuwa serikali itaboresha upatikanaji wa walimu bora zaidi, madarasa ya kisasa, maabara za kisasa na nyumba za walimu.pia, aliwataka wakazi wa Tarime kujiepusha na ugonjwa hatari wa Ukimwi kutokana na takwimu zinazoonyesha kuna asilimia kubw aya maambukizi ya Ukimwi mkoani humo.
Kikwete alirejea kauli yake ambayo amekuwa akiitoa mara kwa mara kwa wanafunzi wanaopata mimba akiwaambia wakazi wa mkoa huo kuwa wanaoambukizwa Ukimwi wanaupata kwa ajili ya tamaa na viherehere vyao.
Alisema serikali yake pia inapambana na malaria kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa.
Kuhusu huduma za maji, Kikwete alisema serikali ya CCM imejitahidi kuboresha sekta ya maji na tayari wamepata fedha kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kuimarisha miradi ya maji na kwamba ndani ya miaka mitatu kila mkazi wa mkoa wa Mara atakuwa akitumia maji ya bomba.
Kuhusu huduma za maji, Kikwete alisema serikali ya CCM imejitahidi kuboresha sekta ya maji na tayari wamepata fedha kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kuimarisha miradi ya maji na kwamba ndani ya miaka mitatu kila mkazi wa mkoa wa Mara atakuwa akitumia maji ya bomba.
Kikwete, ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, pia aliahidi kuboresha sekta ya kilimo kwa kuzalisha wataalam bora na kuweka ruzuku kwenye mazao kama kahawa.
Kikwete aliyeonyesha uchovu katika mkutano huo alishuka ghafla jukwaani na kuondoka baada ya kuwatambulisha wagombea ubunge, akiwaacha wananchi wakimsubiri.
Tukio lililotokea baada ya kupokea wanachama wapya 162 waliotajwa na katibu wa CCM wa mkoa, Ndegaso Ndekubali kuwa wametoka CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi.
Filed under: Politics | No Comments
Dk. BILAL AVUNA KADI LUKUKI ZA WAPINZANI KAYANGA, BUKOBA..!!!Posted by Blog Team on September 24th, 2010
Mgombea Mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cah Mabila Wilaya mpya ya Kyelwa Mkoa wa Kagera, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana Sept 24 na kumnadi mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Karagwe, Rustas Katagila.
Mgombea Mwenza wa urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduxi CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipokea kadi za waliokuwa wanachama wa Vyama vya TLP, CHADEMA na CUF waliotoka katika Kata mpya ya Lukula, ambao walifika katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Mabila Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera jana Sept 23, ambapo jumla ya wanachama 144 kutoka vyama vya upinzani walitarajia kurejesha kadi zao na 14 kati yao walikabidhi kadi hizo kwa mgombea mwenza.
Filed under: Politics | No Comments
KIKWETE 2010 TOVUTI MAALUMU KWA HABARI MOTOMOTO ZA KAMPENI ZA UCHAGUZI..!!!Posted by Blog Team on September 24th, 2010
Habari zenu Ndugu wapendwa,
Tunayofuraha kubwa kuwafahamisha ya kwamba tovuti maalumu na rasmi ya Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. M. Gharib Bilal sasa inapatikana kwenye mitandao:
Tembelea tovuti hii maalumu ya Mgombea Uraisi na Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM mwaka 2010 upate habari mbalimbali kama:
• Wasifu wa Wagombea – Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. Mohammed Gharib Bilal.
• Mafanikio katika sekta mbalimbali.
• Sera na Malengo 2010 – 2015.
• Ratiba za kampeni.
• Hotuba maalumu.
• Matoleo ya Habari.
• Video na picha.
• Mitandao ya Facebook,Twitter na Youtube.
Kupitia tovuti hii na mitandao yake utaweza kupata taarifa mbalimbali na kutoa maoni yako.
“ PAMOJA TUZIDI KUSONGA MBELE”
NITATEKELEZA ILANI YA CCM KWA KASI ZAIDI, NGUVU ZAIDI NA KUWAPA VIJANA AJIRA,MO DEWJI…!!!Posted by Blog Team on September 24th, 2010
MO akihutubia wananchi wa Kata ya Unyambwa.
*******************
Na Hillary Shoo.
Singida. Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Mohamed Gulam Dewji, amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuendelea kuwawakilisha tena bungeni, atatekeleza Ilani ya CCM kwa kasi zaidi ikiwemo kutafuta ufumbuzi wa namna ya kupunguza upungufu wa ajira kwa vijana.
Dewji alisema katika ilani uchaguzi, CCM imeainisha wazi kwamba inatambua tatizo la ajira na hasa ajira ya vijana wanaomaliza elimu ya msingi, sekondari na vyuo vikuu kila mwaka kuwa, ni kubwa mno.
“Vijana hawa wote ni nguvu kazi ya taifa ambayo inaweza kutumika katika kazi na shughuli halali za ujenzi wa nchi yetu na ikapiga hatua kubwa ya kimaendeleo”,alisema Dewji.
Mgombea huyo,alisema ili kukabiliana na tatizo hilo, CCM ina mpango wa kupanua mafunzo ya VETA yaweze kuchukua vijana wengi zaidi, ili waandaliwe kujiajiri wenyewe.
Aidha, alisema vijana watahamasishwa kuanzisha miradi ya kiuchumi na kujiunga katika vikundi vya ushirika vya kuweka na kukopa (SACCOS) ili waweze kupata mikopo kwa masharti nafuu.
“Katika miaka mitano iliyopita, nimewatafutia kazi vijana kutoka jimboni kwetu kwenye kiwanda changu cha nguo cha Afritex kilichopo mkoani Tanga., Kuajiri vijana hao, nimefanikiwa kwa kiasi fulani kupunguza idadi ya vijana wetu wanaomaliza elimu ya sekondari, kukaa vijiweni”,alisisitiza huku akishangiliwa na mamia ya wananchi.
Dewji aliyasema hayo jana katika mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Unyambwa.
Wakati huo huo,Dewji alitumia fursa hiyo kumwombea kura mgombea urais Jakaya Kikwete kwa madai kwamba ameonyesha uwezo mkubwa wa kusimamia utekelezaji wa ilani za uchaguzi. Aidha, alimnadi mgombea wa udiwani wa kata hiyo, ya Unyambwa Salum Satu na kuomba apewe kura za kutosha kumwezesha kushika nafasi hiyo.
MO, akisistiza kuwa Katika kipindi cha miaka saba michezo imeweza kupaa katika mkoa wa Singida ambapio Kindai Shooting Stars, timu ya mkoa ilibeba kombe la kilimanjaro Taifa Cup kwa mara ya kwanza katika historia ya mkoa huo.
MO akicheza ngoma ya Kinyaturu ya kutikisa mabega, maarufu kwa jina la tikisa mabega tingisha kiuno.
Wanafunzi wa shule ya msingi Unyambwa wakimpokea MO kwenye viwanja vya shule hiyo wakati alipokwenda kweye mkutano wa kampeni wa Kata hiyo.
Wanafunzi wakiwa na mabango yanayomnadi MO huko KatikaKata ya Unyambwa
No comments:
Post a Comment