Gazeti la uhuru linaongoza maoni yake
Katika maswali wanayouliza ni kama ifuatavyo?

Toa Maoni Yako
Hali ya Kisiasa Tanzania:
1. Inaridhisha
2. Ni Ubabaishaji
3. Hairidhishi kabisa
4. Inahitaji Kuboreshwa
5. Inahitaji uongozi Mpya
6.Katiba Irekebishwe

Walioongoza ni wale waliosema Inahitaji uongozi Mpya - Ni 29%
waliofuata walisema Ni Ubabaishaji asilimia 26.9
Wanaotaka katiba irekebishwe ni 15.5%
Walisema inaridhisha ni asilimia 12%
Hii sio synovate ni gazeti la chama cha mapinduzi UHURU.
Naomba maoni yaliyoko kwenye gazati la chama yaheshimiwe na watanzania. Wana CCM naomba myaheshimu maoni ya wanachama wenu.
UNAWEZA KUJIONEA MWENYE
Hali ya Kisiasa Tanzania

KUTOKANA NA HAYO HAPO JUU
Mimi sasa nimekubali kuwa kama viongozi walioko madarakani hawawezi kusoma hata sauti ya watu iliyoko katika vyombo vyao basi sikio la kufa halisikiii dawa.
1. Najaribu kuwaza kuwa lazima Raisi wetu mpendwa naye kwa kuwa ana busara na ni mwuungwana basi ameanza kujiandaa kuachia madaraka kwa amani.
2. Wawepo watu wa kumshauri kuanza kusema kuwa akishindwa yuko tayari kukubali matokeo na pia washauri wamsaidie kuandika hotuba ya kukubali kushindwa na kuwashukuru watanzania waliosimama nae.
3. Dr. Slaa katika hotuba zake apunguze kauli zinazoweza kumtia hofu Rais wetu na hata marais wastaafu. Asiendelee kuzungumza habari za kuwapeleka mahakamani. Akubali tu kuwa kule kuhukumiwa na wananchi kunatosha kuwa fundisho.
4. Namshauri Dr. Slaa asiwapeleke mahakamani hata Mkapa. Ila watumie tu utaratibu wa kuwaonyesha mahali matatizo yalipokuwa. Bado wanaweza kuwa na mchango wao katika taifa.
5. Dr. Slaa bado atawahitaji mahali fulani hawa viongozi waliopita hivi ASIJENGE UKUTA AJENGE MADARAJA.