Bunge la 2005-2010: Mhagama, Slaa ndio wachangiaji hodari. Rostam Aziz ashika mkia.
Kwa kipindi cha bunge 2005-2010, Mhe. Jenista Mhagama (CCM, Peramiho) amekuwa mbunge hai (active) kati ya wabunge wote (zaidi ya 270). Katika bunge hilo (2005-2010) Mhe. Mhagama aliuliza maswali ya msingi 25, maswali ya nyongeza 65, na ya kuchangia 272 na hivyo kuweka jumla ya michango yake kufikia 362.
Yeye anafuatiwa na Mhe. Ndugai (CCM, Kongwa) aliyekuwa na jumla ya michango 286, na nafasi ya tatu ikishikiliwa na Mhe. Dr Slaa (Chadema, Karatu) mwenye michango 265. Wa nne ni Zitto Kabwe (Chadema, Kigoma Kaskazini) aliyekuwa na michango 239.
Mhe. Rostam Aziz ameshika mkia kwa kutokuwa na ushiriki wowote wa kuuliza maswali ya msingi, maswali ya nyongeza, au michango kwa kipindi chote cha ubunge wake (kati ya 2005-2010) . Mbunge huyu ni pekee kutofanya hivyo katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.
No comments:
Post a Comment