Tuesday, August 17, 2010

Kichefuchefu cha CCM


Waungwana



Leo nimesema hebu nitembelee hii tovuti ya hiki chama kinachoitwa majina lukuki. Orodha fupi ni kama ifuatavyo:



1. Chama Cha Majambazi - CCM

2. Chama Cha Mafisadi - CCM

3. Chukua Chako Mapema - CCM



Hiyo ni orodha fupi tu. Najua wengi mnayo majina mengine, mkipenda mtayaeleza hapa.



Kabla sijawapa link ya tovuti ya CCM (najua baadhi yenu hamuijui), ngoja nitoe kasoro zake:



1. Domain Name (jina halisi la mtandao) SIO la KIZALENDO. Domain name inaishia na .ORG. Hii ina maana kwamba, kwa vyovyote vile, tovuti hiyo inahifadhiwa nchini Marekani. Mimi ninatumia extension ya Flagfox, kwenye browser ya Mozilla Firefox. Flagfox inakuonesha mahali ambapo tovuti inahifadhiwa, na ukweli ni kwamba, tovuti ya CCM inahifadhiwa MAREKANI! Tanzania ina taasisi, inayosimamiwa na TCRA, yaani, TZ-NIC (Tanzania Network Information Centre), ambayo ina mamlaka ya kusajili na kusimamia majina yote ya mtandao, yaani, CCTLDs, kwa kirefu, Country Code Top Level Domain Names. Kwa upande wa Tanzania, domain hizo ni .AC.TZ, .OR.TZ, .NE.TZ, .MI.TZ, .GO.TZ na .CO.TZ. Domain zenye .AC.TZ ni za taasisi za kielimu (Academic); domain zenye .OR.TZ ni za asasi (Organisation); domain zenye .NE.TZ ni za watoa huduma ya mtandao (Network); domain zenye .MI.TZ ni za kijeshi (Military); domain zenye .GO.TZ ni za taasisi za serikali (Government); na domain zenye .CO.TZ ni za makampuni (Corporations). Domain sahihi ambayo CCM ilipaswa kuwa nayo ni CCM.OR.TZ! HAKUNA UZALENDO!



2. Mpangilio wote wa tovuti hiyo ni wa KITOTO! Hakuna mwongozo unaoeleweka. Maandishi ni ovyo, wametumia maandishi madogo kiasi kwamba kama una macho mabovu kama yangu hutaweza kusoma bila miwani. Rangi na picha zimepangwa kama vile ni homework ya Form 1! UTOTO MTUPU! Nasikia wamemlipa designer wa hiyo tovuti takriban dola elfu ishirini kuitengeneza. Mimi nilidhani ingekuwa BONGE LA WEBSITE! Lakini wapi! Sihitaji kujivuna, lakini nimeshawahi kudesign website bora zaidi, na moja mpya iko njiani. Nitakapoimaliza nitaitangaza hapa, mtaona ninachokisema.



3. Maelezo yaliyomo yana upungufu mkubwa. Muundo mzima wa chama haujawekwa wazi. Wameelezea karibu kila kitu, kasoro UVCCM! Ina maana kuna mtu alisahau? Hakuna hata sehemu moja iliyozungumzia kuhusu UVCCM. Majina ya viongozi, na kadhalika. Pia, hakuna orodha ya matawi ya CCM kwa ngazi ya Mkoa, Wilaya na Kata. Kimsingi, CCM haina orodha kamili ya wanachama wake. Hiki ni chama kinachotamba kuwa na wanachama takriban milioni sita! Wamekokotoa namna gani idadi hiyo bila ya kuwa na orodha kamili?



Imeandikwa kwamba, mke mzuri utamjua kwa tabia yake. Mke mzuri hahitaji kujinadi, utampenda wewe mwenyewe. Kama ningeifananisha CCM na mke mzuri, basi huyu hafai hata kuchumbiwa! Havutii machoni, anaonekana shaghalabhagala, hapendezi, mambo haye waruwaru, hana mbele wala nyuma. Amejiumbua! Ningekuwa mimi ndio JK, NINGEITOA HEWANI hiyo website, kwani INATIA KICHEFUCHEFU! Haifai hata kuangaliwa na mtu yeyote, sembuse mwanachama wa CCM!



Haya, nendeni mkatapike... bofya hapa Website Rasmi ya Chama Cha Mapinduzi - CCM



Lakini nimewaonya! Ni KICHEFUCHEFUUUUUUUUUU!



WanaCCM MMELIWA!



./Mwana wa Haki



P.S. CCM mmejitakia wenyewe. Jamani hata kuweka tovuti nzuri mmeshindwa? Hebu nendeni mkalinganishe na ya CHADEMA.... hii hapa... Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)



Oh, si mmeona? CHADEMA wameweka domain yao kuwa CHADEMA.OR.TZ! Sasa niambie, NANI MZALENDO kati ya CCM na CHADEMA?



Hii ni AIBU TELE! Kama isingekuwa kweli mngesema ninawaonea CCM. Lakini wameiweka! Duh!



Oh, kuhusu domain ya CCM.OR.TZ, nimekwenda kuitafuta kwenye mtandao! Hakuna website yenye jina hilo, lakini kwenye http://www.tznic.or.tz/index.php/home.html inaonekana kwamba kuna mtu aliwahi kuisajili, lakini kwa sasa ime-EXPIRE! Kwa hiyo, CCM wakitaka angalau kuwa na CHEMBE ya UZALENDO, waende pale Millennium Towers, wakawaone TZ-NIC, watawapa hiyo domain name, tena bure wakitaka!

No comments:

Post a Comment