Wednesday, August 18, 2010

ccm wajipanga kumzuia dr slaa




• waandaa mamluki kumdhamini

• waomba msaada wa vyama vidogo



na saed kubenea



mkakati umesukwa na viongozi ndani ya ccm ili kuzima safari ya dk wilbrod slaa kwenda ikulu, mwanahalizi limeelezwa.



Taarifa zinasema, kwa kushirikiana na vyama vidogo vya upinzani, ccm imesuka njama za kumkwamisha dk slaa katika hatua ya kurejesha fomu za kuwania urais.



“kama hatukufanikiwa kumkosesha wadhamini halali, basi tutakwenda mahakamani….lakini hapiti,” kimeeleza chanzo cha gazeti hili kikimkariri mmoja wa viongozi waliopewa jukumu la kumzamisha dr slaa.



Mwanahalisi lina taarifa kamili juu ya njama hizo zinazodaiwa kuhusisha baadhi ya viongozi wa ccm, serikali na vyama vya upinzani.



Dk slaa aliibuka wiki tatu zilizopita, pale alipotangazwa na chadema kuwa mgombea urais kwa tiketi hiyo.



Kuingia kwa dk slaa ulingoni kulibadili upepo wa kisiasa nchini, na kuleta kiwewe ndani ya ccm na hata kufanya viongozi wastaafu wa chama hicho kutamka hadharani kuwa “slaa ni makini…. Hashikiki.”



hatua ya kwanza ya mkakati wa kumwangamiza dk slaa kisiasa inahusisha kumchomekea “wadhamini feki” katika fomu zake za kutaka kuwania urais.



Hatua hii inahusisha maandalizi ya genge la vijana ambao uraia wao una utata. Hawa watapelekwa mikoa mbali mbali nchini ili watie saini fomu zake za udhamini.



Kwa mujibu wa mtoa taarifa, wadhamini hao “feki” watafika kwa maofisa wa chadema wanaoendesha zoezi la kuandikisha wadhamini wakiwa na vitambulisho vyao vya kupiga kura, kwa lengo la kutimiza jukumu walilopewa.



“vijana hao wakimaliza kujiandikisha, wataripoti kwa maofisa wa chama xhao (ccm) ambao watarekodi kadi zao. Kwa kutumia kadi hizo za wasio watanzania, dk slaa atawekewa pingamizi,” ameeleza mtoa habari.



“nakukuhakikishiua, chadema wasipokuwa makini, dk slaa hawezi kuwa mgombea urais. Tayari vijana wametumwa mikoani kutimiza azma ya kumkwamisham” ameeleza kiongozi mmoja wa ccm ambaye hakutaka kutajwa.



Sheria ya uchaguzi inamtaka kila mgombea wa urais awe na wadhamini 200 kutoka mikoa 10 nchini, ikiwamo miwili ya visiwani.



Kwa taarifa za juzi jumatatu, jukumu la kumwekea pingamizi dk slaa litakabidhiwa kwa “wagombea urais wa vyama pinzani.” haijafahamika ni kina nani watapewa jukumu hilo.



Wadau, stori kamili katika front page ya mwanahalisi ya leo. Mwenye soft copy yake atuwekee hapa.

No comments:

Post a Comment