Monday, August 16, 2010

Nyambari Chacha Nyangwine Kurudisha Tarime CCM..Hongera NEC Kwa Kusoma Alama Nyakati


Tangu jimbo la Tarime kubebwa na Marehemu Chacha Wangwe(CHADEMA), na makundi mawili yaliyokila Chama cha Mapinduzi Tarime, imekua vigumu kwa CCM kurudisha jimbo hilo, hata Uchaguzi mdogo ukapita ukamleta Mhe. Charles Mwera-CHADEMA (ambae sasa kakimbilia CUF) pale ,ila uteuzi wa Mwanasiasa kijana mahiri, msomi na mwandishi (miaka 34), Mhe. Nyambari Chacha Nyangwine hakika ni matumaini na tegemeo kulirudisha nyumbani jimbo la Tarime ambalo kusema kweli limerudi nyuma sana na mpaka kuwa kanda maalum ya kipolisi kutokana na uhalifu uliokithiri, pamoja na kwamba kuna na wanaCCM wengi zaidi 30,000 jimboni.



Hakika ninaipa pongezi za dhati Halmashauri kuu ya CCM (NEC) kusoma alama za nyakati, kutomleta tena Mhe. Kangoye aliyeangushwa na Mwera na kuleta mzungumzaji mzuri kijana, kampeni ya vijana kati ya kada huyu kijana Nyangwine na mgombea kijana wa CHADEMA yaani Waitara itakuwa burudani ya kidemokrasia na kwa ndugu zangu wanaoelewa siasa za Tarime, Kule bila NGUVU,Nguvu ya hoja na ukakamavu: huwezi kuwa Mbunge wa jimbo hilo ndani ya kanda maalum ya kipolisi ukiwa lelemama..Hushindi bila kuwa tafu Na fizikali fiti..



Mwaka huu ni Tarime Vijana: Nyangwine (CCM) vs Waitara (CHADEMA) & Mwera(CUF)...tusubiri raundi 12 za kampeni, ila upepo wakati huu naona kama unaelekea zaidi CCM..Mnasemaje JF?

No comments:

Post a Comment