Je CCM imemsindikiza Arcado Ntagazwa kwenda Chadema?
Kada wa muda mrefu wa CCM Arcado Ntagazwa ameamua kujiunga rasmi na chama cha Chadema.
Mzee Ntagazwa amewahi kuwa waziri katika awamu ya kwanza na ya pili ya serikali ya Tanzania.
Katika mahojiano yake na BBC mzee Ntagazwa amesema kwamba sababu kubwa yeye kujiunga na Chadema ni kwamba chama hicho kinatekeleza maudhui ya mwaka 1975 ambayo chama cha TANU kilikuwa nayo na baadae CCM ya hayati mwalimu Nyerere na sasa CCM haifuati maudhui hayo.
Maudhui hayo ni pamoja na swala la kupinga rushwa na kukata kabisa mizizi yake.
Hivi karibuni makamu mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa alisikika akisema kwamba CCM itakuwa tayari kuwasindikiza wale wote ambao wataamua kujiengua na chama hicho na ikibidi kuwasindikiza kwenda huko kwenye vyama vingine.
Swali je CCM imemsindikiza mzee Ntagazwa ambae nnamwona kwamba ni mmoja wa "heavyweight" au "sepremo" katika siasa?
No comments:
Post a Comment