Monday, August 16, 2010

CHADEMA mmejipangaje Iringa Mjini?


Baada ya kuenguliwa kwa Bwana Mwakalebela, wana CCM wengi wameonesha kukerwa na kitendo hicho.

Kumekua na matukio Mengi yakiwemo na kuchana kadi za uanachama Mbele ya ofisi zao(CCM) hapa iringa mjini. Binafsi nimeshuhudia haya.

Wengi wameonesha kutokubaliano ya kamati kuu kumrejesha mama Monica.

Katika pita pita zangu Wengi wameamua kuipa shavu CHADEMA.

Nimejaribu kutafuta CV ya huyu aliyeteuliwa kuwania Ubunge jimbo hili kwa tiketi ya Chadema, Lakini sijafanikiwa.

Ningeomba mwenye data kamili za huyu mheshimiwa azimwage hapa.

CHADEMA naomba muwe makini sana hapa. Mpaka sasa hili jimbo lina kila dalili la kuchukuliwa na upinzani. kinachohitajika nikujipanga vizuri tu.

No comments:

Post a Comment