Monday, August 16, 2010

WATEJA WAHAMA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Wateja bandari ya Dar wahamia nchi za nje Send to a friend


Tuesday, 17 August 2010 08:38

0

diggs

digg



Fredy Azzah

SERIKALI imekiri kwamba vitendo vya wizi wa mizigo ya wateja katika bandari ya Dar es Salaam, vinakuwa kwa kasi na kusababisha baadhi ya watu wanaoitumia bandari hiyo kutoka ndani na nje ya nchi kuhamia bandari za nchi jirani.



Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Miundombinu Dk Shukuru Kwawambwa, alipokuwa akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).



“Moja ya ajenda ya bodi hii iwe kuondoa kero ya udokozi ya mizigo ya wateja iliyokithiri hapa, kuna baadhi ya wateja wanatishia kuihama bandari kwa sababu hii, mimi nitakiweka hiki kama kigezo cha ufanisi wa bodi hii,” alisema Kawambwa.

Baadhi ya wateja wamekuwa wakilalamika, kuibiwa kwa mizigo yao huku wengi wakilalamikia udokozi wa vifaa vya magari yanayopitia bandari ya Dar es Salaam.



Waziri Kawambwa aliitaka pia Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuhakikisha nyaraka muhimu zinapatikana kwa wakati ili wateja waweze kutoa mizigo yao bandarini kwa wakati.



Kwawamba aliwaeleza wakurugenzi wa bodi hiyo wahakikishe kuhakikisha meli zinaingia moja kwa moja bandirini bila kusubiri kama ilivyo hivi sasa.

Aliiagiza bodi hiyo, itafute makampuni ya kupakuwa makontena ili kuongeza ufanisi.



Alisema baada ya kipengele kilichokuwa kikiipa TICS mamlaka pekee ya kupakua mizigo bandarini kuondolewa, hivi sasa watumie fursa hiyo vema kutafuta wawekezaji wengine watakaofanya kazi hiyo, bila ubabaishaji.







Aliitaka bodi hiyo, kuwatafuta makampuni makini yatakayopakua mizingo bandarini ili kuepuka kuingia katika mikataba mibovu kama ilivyokuwa kwa TICS.

Kwa mujibu wa Kawabwa, mchakato wa kujenga magati mawili ya kupakuwa mizigo bandarini hapo, unaendelea.





Alisema ili kuhakikisha kero ya msongamano wa makontena bandarini unamalizika, vituo 10 venye uwezo wa kuhifadhi makontena 9,000 kwa wakati mmoja vimeanzishwa.

No comments:

Post a Comment