Je Kikwete atakubali matokeo au atakuwa kama Mugabe
Wengi tunajua historia ya Zimbabwe kwa takriban chaguzi mbili hivi Mugabe anashindwa na mpinzani wake wa karibu Tsvangirai. Kwenye uchaguzi uliopita pamoja na chama cha MDC kuwa na wabunge wengi lakini Mugabe kwa ubabe wake bado anang'ang'ania ikulu.
Tunamuomba Kikwete asiige wala asithubutu kufanya hivyo maana ataliangamiza taifa na kuandika historia mpya. Hatutaki yatokee ya Zimbabwe na Kenya, kama alivyoingia salama ndivyo hivyo atakavyotoka salama na heshima yake italindwa, ni angalizo tu.
No comments:
Post a Comment