Monday, August 23, 2010

Mmepoteza Ubunge kwanini bado ninyi mawaziri?


Tangu wiki iliyopita mwishoni na hata leo nimeendelea kusikia ati "Waziri" fulani kafanya jambo hili au lile. Hivi Mwanasheria Mkuu hawezi hata kutoa maelekezo kuwa sasa hivi nchi haina mawaziri au waziri mkuu? Baada ya Bunge kuvunjwa rasmi kwa kuanza kampeni ya uchaguzi Augusti 20 wabunge wote walipoteza ubunge wao na hivyo waliokuwa mawaziri nao wamepoteza uwaziri wao. Haijalishi kama baadhi yao wamepita bila "kupingwa" lakini siyo wabunge hadi siku watakapoapishwa.



Hivyo, aidha Rais Kikwete awateua baadhi yao na kuwaapisha kuwa mawaziri sasa kwa mujibu wa katiba (japo sioni haja ya kufanya hivyo) ama wale wote wanajiona ni bado "mawaziri" wapigwe makonzi na kuambiwa waondokane na fikra hizo kwani wao siyo mawaziri na uhondo wote na madaraka yao ya uwaziri hayapo sasa na wizara zao ziko chini ya Makatibu Wakuu.



So.. sitaki kusikia chombo cha habari kinatuambia ati "Waziri wa Ulinzi na JKT Dr. Hussen Mwinyi" amefanya hili au lile au "Waziri wa Nishati Bw. William Ngeleja amefungua". Hawa watu SIYO MAWAZIRI!!!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment