Monday, August 16, 2010

Unazijua Mbinu wazitumiazo CCM kuweza kushinda uchaguzi wa October 2010?


Kitaifa: CCM wameongeza mshahara wa wafanyakazi kinyemela

Kimkoa: Kyela wapata soko la zao la kokoa,kawambwa atembela miradi ya ujenzi Mbeya.



Just last week Dr Kawambwa alikuwa uko akikagua uwanja wa ndege ili serikali ionekane iko serious ingawa Dr alilishwa thumu na TANROAD manager kuwa barabara ya Chunya inaendelea wakati mkandarasi amesimama kitambo kisa hawajalipwa hela.



CCM mkitaka win kura za wana Mbeya piga chini mkuu wa mkoa na muache kuwanyanyasa na kuwafuatilia Mwandosya na Mwakyembe bse kwa Mbeya hao wanakubalika kuwazuia hao ni sawa na kutwanga amji kwenye kinu.Mwisho ahadi zote mlizoahidi zitekelezwe mfano barabara ya kwenda matema beach mpaka leo jiiiiiiiii



Wananchi kuweni makini na hizi short term Mbinu wakishaingia madarakani tumeumia.

Soma iyo Mbinu ya COCOA



Cocoa ya Tanzania yapata soko Marekani



d

Thursday, 12 August 2010

Mwananchi

Na Sadick Mtulya



ZAO la Cocoa linalolimwa wilayani Kyela, mkoani Mbeya limepata soko nchini Marekani baada ya kampuni Askinosie Chocolate Ltd, kukubali kuwekeza na kununua zao hilo kwa ajili ya viwanda vya kutengenezea Chocolate.



Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na Waandishi wa habari, Mkurugenzi wa uhamasishaji uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Raymond Mbilinyi alisema kampuni hiyo itategeneza Chocolate itakayofungwa kwa jina la Tanzania kama njia ya kuitangaza.



“Kampuni ya Askinosie Chocolate Ltd ya Marekani baada ya kufanya uchunguzi wa kina, wameamua kununua Cocoa inayozalishwa nchini kwa kuwa haina kemikali na ni tofauti na ile inayozalishwa na nchi nyingine,” alisema Mbilinyi.



Alisema ujio wa kampuni hiyo ni matokeo ya ziara mbalimbali alizozifanya Rais Jakaya Kikwete nchini Marekani na kumteua Balozi wa heshima, Dough Piti wa nchi hiyo kwa ajili ya kuutangaza utalii na uwekezaji wa nchini.



" Kwa muda mrefu Cocoa haikuwa na soko la uhakika, hivyo siri ya kujikita zaidi katika soko la Marekani ni kuzalisha kwa ubora ili kuongeza vipato na kuondokana na hali duni ya maisha miongoni mwa wakulima,'' alisema .



Mbilinyi alisema kupitia mpango wa Kilimo Kwanza, nchi inatakiwa kujipanga na kutumia soko la Marekani kujitangaza ili kupata masoko mengine duniani kote



“Soko la cocoa ni kubwa duniani, wakulima nchini wazidi kuzalisha kwa wingi na kwa ubora, kampuni ya Askinosie Chocolate Ltd itakuwa balozi mkubwa katika masoko ya Marekani na nchi nyingine duniani,”alisema Mbilinyi.



Naye mwakilishi na Rais wa Kampuni ya Askinosie Chocolate Ltd, Shawn Askinosie alisema ujumbe wao ulikuja kuona Cocoa inayolimwa nchini na imeridhika kwa kuwa ni tofauti na inayolimwa sehemu nyingine na soko lake ni kubwa duniani kote.

No comments:

Post a Comment