Dr Azavel Lwaitama Kaionya TBC1 na UMAFYA WAKE
Nilisikitikia sana walichofanya Wahariri wa TBC1..Mimi nilikuwa uwajani pale Jangwani...na vijana wa TBC1 walikuwepo pale kama mimi na walichuwa picha na sauti kama mimi.... umati ule hata mimi sikuutegemea...nilikumbuka mwezi Agosti 2007 paleplae Jangwani umati ulipompokea Mheshimiwa Zito baada ya kupewa adhabu ya kusimamishwa kuhudhuria Bugeni eti kwa kumtukana Waziri Karamagi kuhusu Buzwagi...
Mimi si mwanachama wa chama cha sisa chchote tangu mwaka 1973...Nilikuja kuona mwenyewe kulikoni...Walikuwa watu wengi sana...na hakukuwepo mabasi wala malori yaliyo wasomba kuwaleta pale...wengi walimiminika pale kwa miguu tangu asubuhi na hasa mara baada ya helokopta ilipozunguka uwanjani pale mara mbili hivi kwenye saa kama 2 na nusu au tisa hivi... kijana mmoja aliye pokea msafara wa Dr. Slaa toka uwanja wandege alisema waliambiwa helikopta hile ilishinikizwa kushuka na kutoendelea kuruka ruka juu ya uwaja kutoa amasa watu wajiunge na umati uwe mkubwa Jangwani...wapo watu wazima eti walioogopa watu wasiwe wengi wataofika uwajani kushuhudia kulikoni eti?
Midundo ya Sugu na wenzake ilikuna roho...sala za viongozi wa kidini..mmoja wa kikikrito na mwingine wa kiislamu zilinifanya nikiri kuwa dini si lazima ipumbaze akili...hotuba za viongozi mbali mabali kama Mheshimiwa Alfi, Rwakatare, Prof Baregu, Marando, Zito, na Mbowe zilisisitiza kuhusu hoja ya watanzania wote bila kujali uanachama wao wa vyama vya siasa kumchangua Dr. Slaa Raisi wa Jamhuri ya Tanzania ili kuondoa jeuri na kiburi potofu kinachotawala fikra za viongozi wa chama cha kijamaa kinacho ongozwa na washabiki wa ubepari uchwara na chenye kusimamia serikali yenye mwelekeo wa ubepari wa radha ya soko holela...serikali ambayo kwa kweli inaitaji kuongolewa kwa kihali na kwa amani katika uchanguzi wa mwaka huu Oktoba kwa vile ineshindwa kuongoza uchumi wa nchi hii kwa njia yenye kuleta tija si tu wajamaa kama mimi bali hata kwa mabepari wasiopenda vurugu na taratibu zisizogubikwa na tuhuma za rushwa kubwa kubwa...
.Poleni wale wote TBC1mliowaadilifu maana sitoshangaa kama TBC1 tayari mmeisha pewa maelekezo yaliyojitokeza kwenye gazeti la serikali la Habari Leo na leo kwenye kichwa cha habari kisemacho eti wanachi wana hoji kulikoni CHADEMA wanaendesha kampeni kabla ya kipenga cha kampeni za uchaguzi kupigwa...wameisha sahau TBC1 walitumia pesa za umma kutangaza moja kwa moja kampeni kabla za kipenga za chama tawala tangu JK kuchukua fomu toka chama chake na kuzikabidhi kwa mwanae na rafiki zake, kuzirudisha kwa shangwe na vifijo, mkutano mkuu wa chama chake kukamilisha uteuzi, na juzi juzi JK kuchukua fomu za Tume ya Uchanguzi akisindikizwa na mjane wa Baba wa Taifa...
Na si tu TBC1...luninga nyingi za eti mashirika binafsi zilijituma kutotangaza mno mapokezi ya kishujaa ya Dr. Slaa.... labda wanadhani hiyo itapunguza uwezekano wa Watanzania wengi kuanza kuwa na ujasiri wakusema sasa basi kuendelea kutawaliwa na watu jeuri na wenye kuburi potofu kiletwacho na kutawala kwa muda mrefu kupita kiasi bila sababu za maana... Labda watawala wetu wanaogopa kuwa kwa kuuona umati ule wa Jangwani ukiwa mtulivu kabisa bila kuwepo na polisi wengi hata kidogo...na sauti zile zenye hoja zenye hekima na unyenyekevu mkubwa za akina Zito, Marando, Baregu, Alfi, Rwakatare, Mbowe, na mwenyewe aliyebatizwa Kamanda wa Ardhini, mnyenyekevu kuliko wote Dr. Slaa... Sijui...Mimi nimetoka pale na matumaini makubwa kuwa kumbe Watanzania hawa hawa wanaweza wakasema BASI.....
Litakalo saidia sana ni kwa viongozi wa CHADEMA kuendelea kusema kuwa watu wamchague mtu safi na mwenye kutaka mabadiliko ((na hasa ya kupunguza madaraka ya rais ))) bila na kuongeza ushawishi wa nguvu ya umma…..bila kuangalia mtu safi huyu anatoka chama gani…wapo watu safi na makini ndani ya CCM kama Waziri Mkuu Pinda, Prof Tibaijuka ,Spika Sitta, Dr. Mwakyembe, Dr. Magufuli na Prof Mwandosa na hata wafanyabiashara wazalendo kama Dr. Diallo wa Ilemera kule Mwanza, pamoja na waledi kama Mheshimiw Hamad Rashid na Juma Haji Duni wa CUF…. hakuna ubaya kuwapa moyo Watanzania wa aina hii na wapiga kura wao kwa kutangaza kama mkakati kuwa wakichanguliwa serikali ya Dr. Slaa itafikiria kuwaweka kwenye serikali ya Dr. Slaa ambayo itakuwa ya kitaifa…Toa ushauwishi kuwa hata CHADEMA ikichukua dola wabunge wake ambao hawatakuwa serikalini wataendelea kuichachafya na kuitoa kamasi serikali iliyopo madarakani ili itoe huduma safi kwa wanachi….,
Napendekeza CHADEMA itoe kanda ya video ya mihadhara yote ya safari ya kusaka wadhamini ya nabii Slaa...hasa huu mhadhara wa Jangwani... na kuiuza nakala maelfu kwa maelfu ya kanda hiyo ya video kwa bei ndogo ili kila mwanachi apate kuisikiliza. Pia CHADEMA na watanzania wenye nia njema na uchungu na nchi hii wanunue nakala za kanda ya video hii na waionyeshe kwenye kumbi mbali mbaliTUCTA ambapo aliwasihi wafanyakazi kutumia busara za mabayuwayu na si zile za kongota pia ingepatina na kusambazwa na CHADEMA kama sehemu ya UJUMBE MAHUSUSI KWA WANANCHI.....
Sisemi haya kwa ushabiki waina yoyote kabisa kwa CHADEMA maana kwa kweli mimi chama changu damu damu ni CCM pale itakapoangushwa na kutenganishwa na uongozi wa serikali. Ni hapo tu itapata nafasi ya kupokea mawazo ya wenda wazimu kama mimi ili kujitafakari upya ikiwa upinzani wakati huo ikitafuta kurudi kwenye utetezi wa itikadi yake ya kijaamaa ya enzi za Azimio la Arusha. CCM ya aina hiyo itawafukuza mabepari walijichomeka kwa rushwa ndani ya uongozi wake na ni hapo ndipo itaweza kutoa upinzani madhubutu kwa utawala wa kibepari wenye uzalendo wa CHADEMA kama chama tawala.....
Mimi nasema : mwaka huu haki ya Mungu CCM ya mafisadi ya leo hii inaweza ikashangaa kama KANU ya RAIS MOI ..nilichokiona kwa macho yangu pale Jangwani ni maajabu yenye kuleta faraja kwamba labda Watanzania wanaanza kujitambua na kuona manufaa ya sera ya demokrasia ya vyama vingi ambayo, muhimu kuliko zote ni kutoa nafasi ya kung’olewa kwa amani, utulivu na mshikamano kwa serikali ya chama tawala kila kikitawala kwa muda mrefu kupindukia hadi viongozi wake na wapambe wao kuanza kuwadharau wananchi na kuwatolea vitisho kana kwamba wao wamewekwa madarakani kutawala milele kwa janja janja....
Azaveli Lwaitama
No comments:
Post a Comment