Wakaazi na wenyeji wa mji wa Arusha nchi yetu iko kwenye matayarisho ya uchaguzi mkuu October 2010.Nimeona ni vyema na haki tukawajadili wagombea ubunge wa vyama vitatu ambavyo nini hakika wataleta ushindani mkali.
Mgombea ubunge wa CCM
Mama Batilda Salha Buriani kazaliwa mwaka 1965
chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1985 – 1988 B.A [Public Admin & International Relation ]
Mwaka 1990 – 1991 alichukua shahada ya pili katika chuo kikuu Sussex M.A [Development Studies]
mwaka 1992 – 1997 alichukua shahada ya uzamivu [Phd] chuo kikuu London .
Bi Batilda mpaka sasa ni waziri wan chi makamu wa Rais mazingira.
Mapungufu yaMama Batilda Salha Buriani ni mengi lakini nitajaribu kuyatupia macho machache wengine mnaweza kuongeza kadri mnavyomfahamu.
Bi Batilda Salha Buriani wakati akiwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Bunge na uratibu [ chief Whip ]aliwahi kumlima barua ya onyo kali Mama Anna kilango Malechela kwa kosa kubwa la kuzungumzia mradi wa Richmond bungeni.Hili ni kosa kubwa sana kwani baadae ilikuja kujulikana mradi wa RICHIMOND ulikuwa wa kifisadi,kwa maneno mengine Mama Batilda ni miongoni mwa wabunge/ mawaziri waliokuwa wakitetea ufisadi ndani ya serekali,bungeni na chama .
Mama Batilda Salha Buriani kampeni zake ziligubikwa na rushwa na nguvu ya ajabu nyuma yake ilikuwa ikihakikisha anashinda tiketi ya kugombea ubunge kupitia CCM.Vyombo vya dola hasa UWT/TAKUKURU vilihakikisha hakuna wa kumzuia kushinda.Wakaazi wengi wa mji wa Arusha wanajua Mama B Salha Buriani alisaidiwa sana na Mbunge wa Monduli Bwana E N Lowassa kwa faida za kisiasa siku za usoni.Mama Batilda alihudhuria uzinduzi wa nyimbo za kwaya KKKT mwanzoni mwa mwaka huu,wengi tulijua alikuwa akijiandaa kugombea ubunge wa Arusha mjini.E N Lowassa mara nyingi amekuwa akimtumia Askofu Thomas Laizer kwa manufaa yake ya siasa kitu ambacho tayari kimeanza kulalamikiwa na waumini wengi wa KKKT.
Mradi wa ujenzi wa barabara Arusha – Musoma kupitia mbuga ya wanyama ya Serengeti ni udhaifu mkubwa wa Mama Batilda Salha Buriani kama waziri anae shughulikia mazingira.Mama Batilda kaamua kukaa kimya pengine kufunika kombe mwanaharamu apite lakini akae akijua wakaazi wengi wa mji wa Arusha wanapata mapato mengi kwasababu ya utalii.Ujenzi wa barabara kupitia mbuga ya wanyama ya Serengeti kutaharibu mazingira pia kunaweza kusababisha uhamaji wa nyumbu kukoma kabisa.Inashangaza mtu wa aina hii anataka kuwa mbunge wa mji unaongoza katika shughuli za utalii Tanzania.
Ikiwa Mama Batilda Salha Buriani atachaguliwa kuwa mbunge wa Arusha,hakika utakuwa ni ushindi mkubwa wa wanamtandao bila shaka nguvu ya wanamtandao itaongezeka maradufu.Mama Batilda atakuwa ni mbunge wa aliyempachika na wala hataweza kuwakilsha vyema wapiga kura wa Arusha mjini.
Mgombea Ubunge wa CHADEMA
Godbless Lema elimu yake haijulikani kabisa na ni moja ya mambo yaliyochangia kupunguza kura zake katika uchaguzi wa mwaka 2005.Anadai anacheti cha Computer lakini hatakia kutaja jina la chuo alichosoma wala mwaka aliomaliza.Anadai alimaliza kidato cha sita lakini hataki kutaja jina la shule aliyosoma wala mwaka na alama alizopata ??????????.
Godbless Lema haijulikani anafanyakazi gani haswa, mara nyingi anapenda kujiita mfanyabiasha za madini na wakati mwingine anadai kununua vitu mbali mbali Dubai & Japan.Hana ofisi ya biashara inayojulikana muda wake mwingi anapenda kukaa mitaani kuzungumzia mambo asiyoyajua vyema kwa kujidai anayajua kuliko mtu mwingine.
Godbless Lema ni dalali mzuri wa siasa za upinzani anajua kucheza karata zake vizuri sana huku akiyatanguliza maslahi yake binafsi.Bwana Lema anahusika bila shaka yoyote alifanikisha deal ya kumuondoa Diwani wa TLP Sombeti Bwana Mawazo na kumpeleka CCM kwa ujira wa pikipiki za mafisadi na kiwanja.Baada ya kutimuliwa TLP akakimbilia CHADEMA na amefanikwa kujinyanyua hadi akapitishwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA .wanamageuzi bado wanakumbuka jinsi alivyoiondoa kesi ya kupinga ushindi wa Mheshimiwa Felex Mrema mahakamani bila kuwashirikisha viongozi wa chama wakati chama kilitoa fedha za kugharamia kesi.Ilikuja kubainika Bwana Lema alipewa kitu kidogo ili kuiondoa kesi mahakamani.
Godbless Lema akifaniwa kuwa mbunge wa Arusha mjini ataongeza idadi wa viti vya wabunge wa upinzani jambo ambalo ni jema na afya kwa demokrasia ya Tanzania lakini hatakuwa na mchango wa maana bungeni kama akina Dr Slaa na Zitto Kabwe sana sana ataongeza idadi tu.
Godbless Lema anategemea zaidi umaarafu wa CHADEMA kuchaguliwa anatamani sana wapiga kura wasahau alivyorubuniwa na CCM mara mbili.
[1] Kumpeleka Mawazo CCM.
[2] Kufuta kesi ya kupinga ushindi wa Felex Mrema .
[3] Atapenda wapiga kura wasihoji elimu yake.
[4] Atapenda wapiga kura wasihoji kazi yake.
[5] Atapenda wapiga kura wampigie kura kwasababu ya umaarafu wa CHADEMA na Dr Slaa.
Mgombea ubunge wa TLP
Bwana Max Lyimo kazaliwa mwaka 1964
Bachelor of Science Degree Chuo kikuu cha Dar
Masters of Business Administration Chuo kikuu huria Tz
Kuingia kwa Bwana M Lyimo kugombea ubunge wa Arusha mjini ni changamoto ambayo CCM na CHADEMA hawakutarajia hasa ikizingatiwa TLP katika chaguzi zote imekuwa ikileta upinzania mkubwa kwa CCM.
Udhaifu pekee wa Bwana Lyimo ni kutojulikana na wakaazi wengi wa mji wa Arusha na vitongoji vyake,chama chake kinatakiwa kutilia mkazo mkubwa kumtambulisha hasa ikizingatiwa kuongezeka kata za Moshono,Olkeriani na nk pia cha cha TLP ambacho kilikumbwa na mgogoro tofauti na cha CHADEMA ambacho muda mwingi walikuwa wakikijenga chama kupitia operesheni Sangara.
Bwana M Lyimo akichaguliwa kuwa mbunge wa Arusha ataongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni.Bwana Lyimo hatategemea umaarufu wa chama chake ambao haupo kwasasa.Nimemsikiliza Bwana Lyimo mara moja tu katika mkutano wake wa kujitambulisha eneo la soko kuu.Ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kujenga hoja.Anaweza kuwa mpambanaji kama akina Dr Slaa na zitto Kabwe.
Nategemea michango na mijadala ya kujenga ili jimbo la Arusha mjini lipate mbunge makini,mwadilifu,mbunifu na zaidi ya yote mwenye kuangalia maslahi ya taifa bila kujali jimbo
No comments:
Post a Comment