Tuesday, August 10, 2010

WITO KWA VIONGOZI WA CHADEMA

Hongereni sana kwa kazi kubwa mnayofanya ya kuikomboa nchi yetu.




Kama Mtanzania naomba, PAMOJA NA MAMBO MENGINE, mniruhusu kupendekeza yafuatayo ili yawasaidie katika kutimiza ndoto ya kushinda uchaguzi mwaka huu wa 2010.



1. ANZISHENI NA FUNGUENI VITUO NA SEHEMU MAALUMU KILA KONA YA NCHI YETU ZA KUKUSANYA MICHANGO YA FEDHA TASLIMU TOKA KWA WATANZANIA AMBAO HAWAWEZI KWENDA BENKI KUWEKA FEDHA KWENYE AKAUNTI ZA CHADEMA. Katika mpango huu lengo linapendekezwa liwe ni kukusanya ANGALAU shilingi elfu moja kila wiki toka kwa kila Mtanzania. Sehemu hizo zinapendekezwa ziwe wazi kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa tisa mchana ili fedha itakayokusanywa siku husika iweze kupelekwa benki siku hiyohiyo kabla ya saa kumi jioni. Sehemu hizi ziwe na MAKASHA maalumu yaliyo na kufuri maalumu ambapo kila mchangiaji atakuwa anatumbukiza mchango wake. Kwa upande huo huo mnaweza pia kuongea na benki za CRDB na NMB ili katika kila tawi la benki hizo kuwe pia na HAYO MAKASHA MAALUMU ambapo kila mchangiaji badala ya kupanga foleni atakwenda tu kuweka mchango wake katika KASHA MAALUMU na kisha kuondoka. KILA IJUMAA AU JUMAMOSI YA WIKI HUSIKA MAKASHA HAYO YAWE YANAFUNGULIWA NA KISHA FEDHA ZILIZOPATIKANA KUWEKWA BENKI KWENYE AKAUNTI HUSIKA NA TAARIFA RASMI KUTOLEWA KWA WATANZANIA WOTE.



2. CHADEMA inunue muda wa angalau saa 5 kila wiki katika redio zetu hasa TBC Taifa, Radio One na RFA ili kuweza kuzungumza na Watanzania moja kwa moja kila siku kwa angalau nusu saa. Na kila siku asubuhi kwa muda usiozidi dakika 7, Dr. Slaa awe anazungumza na Watanzania kupitia Televisheni na Radio.



3. Pindi kampeni zitakapoanza rasmi CHADEMA iwe inafanya matembezi ya mshikamano kila Jumamosi ya Kilomita MBILI ambapo kila mshiriki ataombwa awe anachangia shilingi elfu tano tu toka kwake na toka kwa wadhamini wake.



NITASIKITIKA SANA KAMA JAKAYA ATASHINDA UCHAGUZI MWAKA HUU. BINAFSI NIMEMWANDIKIA SANA KWA NJIA WA EMAIL NA BARUA ZA KAWAIDA KAMA RAIS WANGU. ILA NASIKITIKA SANA MAWAZO YANGU HAYAJAFANYIWA KAZI. NITASHUKURU SANA KAMA ATAWEKA HADHARANI EMAILS NILIZOMWANDIKIA NA BARUA YANGU YA TAREHE 03/02/2006 ILI RAIS AJAE AWEZE KUYAFANYIA KAZI HAYO MAWAZO, AMBAYE KWANGU MIMI NI WEWE DR. W. SLAA

No comments:

Post a Comment